Misaada ya Kujifunza
Mzaliwa wa Kwanza


Mzaliwa wa Kwanza

Katika wakati wa mapatriaki wa kale, mtoto wa kiume wa kwanza ndiye aliyepokea haki ya uzaliwa wa kwanza (Mwa. 43:33) na hivyo alirithi uongozi wa familia mara baada ya kifo cha baba. Mzaliwa wa kwanza alipaswa kuwa mwenye kustahili ili kutwaa wajibu huu (1 Nya. 5:1–2) na angeweza kupoteza haki ya mzaliwa kwa kuwa mtu asiye wa haki.

Chini ya sheria ya Musa, mtoto wa kiume wa kwanza aliheshimika kama mali ya Mungu. Mzaliwa wa kwanza alipokea sehemu mbili ya mali ya baba yake (Kum. 21:17). Baada ya kifo cha baba yake, yeye aliwajibika kwa matunzo ya mama yake na dada zake.

Wanyama madume wazaliwa wa kwanza nao pia walikuwa mali ya Mungu. Wanyama waliokuwa safi walitumika kwa kutolea dhabihu, wakati wanyama walio kuwa siyo safi waliweza kukombolewa au kuuzwa au kuchinjwa (Ku. 13:2, 11–13; 34:19–20; Law. 27:11–13, 26–27).

Mzaliwa wa kwanza alisimama badala ya Yesu Kristo na huduma yake duniani, akiwakumbusha watu kwamba Masiya mkuu angelikuja (Musa 5:4–8; 6:63).

Yesu alikuwa mzaliwa wa kwanza kati ya watoto wa kiroho wa Baba yetu wa Mbinguni, Mzaliwa Pekee wa Baba katika mwili, na ndiye wa kwanza kufufuka kutoka kwa wafu katika Ufufuko (Kol. 1:13–18). Watakatifu waaminifu wanakuwa waumini wa Kanisa la Mzaliwa wa Kwanza milele (M&M 93:21–22).