2010–2019
Kila siku ya milele
Oktoba 2017


Milele Kila Siku

Unyenyekevu kuhusu sisi ni kina nani, na nia ya Mungu kwa ajili yetu ni muhimu.

Tangu huduma yangu katika Misheni ya Uingereza kama kijana, nimefurahishwa na ucheshi wa Kiingereza. Wakati mwingine unabainishwa na kujipinga wenyewe, staha, mtazamo wa unyenyekevu katika maisha. Mfano wa hili ni jinsi majira ya joto yanavyosimuliwa. Majira ya joto ya Uingereza kwa kiasi ni mafupi na hayatabiriki. Kama mwandishi mmoja katika njia ya wastani alisema, “Ninapenda majira ya joto ya Uingereza, ndiyo wakati wa mwaka niupendao.1 Kibonzo changu nikipendacho cha Kiingereza kilipigwa picha kitandani mwake kikiamka kimechelewa asubuhi na kuwatangazia mbwa wake, “Oh Jamani! Nafikiri tumechelewa kuamka na tumekosa majira ya joto.”2

Kuna analojia katika ucheshi huu kwenye maisha yetu katika hii dunia nzuri. Maandiko yako wazi kwamba uwepo wetu wa thamani hapa duniani ni muda mfupi sana. Ingeweza kusemwa kwamba kutoka mtazamo wa milele, muda wetu duniani unakimbia kama majira ya joto ya Uingereza.3

Wakati mwingine azma za mtu na uwepo wake hasa pia vinaelezwa katika masharti ya unyenyekevu hasa. Nabii Musa alikuwa amelelewa katika kile baadhi leo wanaweza kuita ukoo wa majaliwa. Kama ilivyorekodiwa katika Lulu ya Thamani Kuu, Bwana, anamtayarisha Musa kwa kazi yake aliyopangiwa ya kinabii, akimpa maelezo ya jumla ya ulimwengu na watoto wote wa watu ambao wapo na walioumbwa.4 Musa kwa jinsi fulani jibu lake lilikuwa la kushangaza, “Sasa … Najua kwamba binadamu si kitu, kitu ambacho sikudhania”5

Baadaye, Mungu, kwa kile sawa na kupinga hisia zozote za kutokuwa na maana ambazo Musa aliweza kuwa nazo, alitangaza azma yake ya kwelii: “Kwani tazama, hii ndiyo kazi yangu na utukufu wangu—kuleta kutokufa na uzima wa milele wa mwanadamu.”6

Sisi wote tuko sawa mbele ya Mungu. Fundisho Lake li wazi. Katika Kitabu cha Mormoni, tunasoma, “Wote ni sawa kwa Mungu,” ikijumuisha “weusi kwa weupe, wafungwa na walio huru, wake kwa waume.”7 Vivyo hivyo, wote wamealikwa kuja kwa Bwana.8

Yoyote anayedai ukubwa katika mpango wa Baba kwa sababu ya tabia kama mbari, jinsia, utaifa, lugha, au hali za kiuchumi ni makosa kimaadili na haelewi azma ya kweli ya Bwana kwa watoto wote wa Baba.9

Kwa bahati mbaya, katika siku zetu takribani katika kila sehemu ya jamii, tunaona kujigamba na jeuri ya kutamba wakati unyenyekevu na kuwajibika kwa Mungu kumeathirika. Sehemu kubwa ya jamii imepoteza minyororo yake na haielewi kwa nini tupo katika dunia hii. Unyenyekevu wa kweli, ni muhimu kutimiza azma ya Bwana kwa ajili yetu, ni nadra kuonekana.10

Ni muhimu kuelewa ukubwa wa unyenyekevu wa Kristo, uadilifu, tabia, na akili kama ilivyooneshwa kwa mfano katika maandiko. Ni ujinga kudharau umuhimu wa muendelezo wa kujitahidi katika hizi tabia za kikristo na sifa siku hadi siku, hasa unyenyekevu.11

Maandiko yako wazi kwamba wakati maisha haya kwa kiasi ni mafupi, kwa kweli ni muhimu.Amuleki, ambaye alikuwa mmisionari mwenza wa Alma katika Kitabu cha Mormoni, alisema, “Maisha haya ndiyo wakati wa watu kujitayarisha kukutana na Mungu; ndio tazama wakati wa maisha haya ndiyo siku ya watu kufanya kazi wanayohitaji.”12 Hatutaki, kama kibonzo changu, kulala maisha haya yote.

Mfano wa Mwokozi wa unyenyekevu na dhabihu kwa binadamu wote ni tukio kubwa sana katika historia. Mwokozi, hata kama mshiriki wa Uungu, alikuwa tayari kuja duniani kama mtoto mchanga wa hali ya chini na kuanza uwepo ambao ulijumuisha kufundisha nakuponya kaka zake na dada zake na hatimaye maumivu yasiyoelezeka katika Gethsemane na juu ya msalaba ili kukamilisha Upatanisho Wake. Kitendo hiki cha upendo na unyenyekevu kwa upande wa Kristo ujulikana kama kujishusha Kwake13 Alifanya hivi kwa kila mwanaume na mwanamke Mungu alioumba au atakaoumba.

Baba yetu wa Mbinguni hataki watoto Wake kukatishwa tamaa au kuacha utafutaji wao wa utukufu wa selestia.Wakati tunapotafakari kwa kweli kuhusu Mungu Baba na Kristo mwana, Wao ni kina nani, na kile walivyokamilisha kwa niaba yetu, inatujaza sisi na staha, mshangao, shukrani, na unyenyekevu.

Unyenyekevu ni muhimu katika kumsaidia Bwana Kuendeleza Kanisa Lake

Alma aliuliza swali katika siku zake ambalo linafaa leo: “Ikiwa mmepata mabadiliko ya moyo, na ikiwa mmesikia kuimba wimbo wa upendo wa ukombozi, nitauliza, mnaweza kuhisi hivyo sasa?”14 Alma aliendelea “Mngesema, kama mngeitwa kufa wakati huu, … kwamba mlikuwa wanyenyekevu vya kutosha?”15

Kila wakati ninaposoma kuhusu Alma Kijana akiacha wajibu wake kama mkuu wa nchi ili kuhubiri neno la Mungu,16 nimevutiwa. Alma kwa uwazi alikuwa na ushuhuda mkubwa wa Mungu Baba na Yesu Kristo na alihisi kuwajibika Kwao kikamilifu na bila kusita. Alikuwa na kipaumbele sahihi na unyenyekevu kuachia hadhi na nafasi kwa sababu alitambua kwamba kumhudumia Bwana kulikuwa muhimu zaidi.

Kuwa na unyenyekevu wa kutosha katika maisha yetu ili kusaidia kuendeleza Kanisa ni thamani kubwa hasa. Mfano katika historia ya Kanisa inaonesha. Mnamo June ya mwaka 1837, Nabii Joseph alipata mwongozo wakati akiwa Hekalu la Kirtland kumwita mtume Heber C. Kimball kupeleka injili ya Yesu Kristo “Uingereza … na kufungua mlango wa wokovu kwa taifa hilo.”17 Mtume Orson Hyde na wachache wengine walipangiwa kufuatana naye. Jibu la Mzee Kimball lilikuwa la ajabu. “Wazo la kuchaguliwa kwenye misheni muhimu kama hii lilikuwa takribani zaidi ya vile ningeweza kuhimili. … [Mimi] nilikuwa tayari karibu kuzama chini ya mzigo ambao ulikuwa umewekwa juu yangu.”18 Hata hivyo, alikubali misheni kwa imani kamilifu, moyo, na unyenyekevu.

Wakati mwingine unyenyekevu ni kukubali wito wakati tunajiona hatutoshi. Wakati mwingine unyenyekevu ni kuhudumia kwa imani tunapojiona tuna uwezo wa kupangiwa shughuli ya hali ya juu. Viongozi wanyenyekevu kwa maneno na kwa mfano wamegundua kwamba sio pale tunapohudumia, bali jinsi gani tunavyohudumu kwa imani.19 Wakati mwingine unyenyekevu ni kushinda hisia zinazoumiza wakati tunahisi viongozi au Waumini wametutendea visivyo.

Mnamo Julai 23, mwaka 1837, Nabii Joseph alikutana na Mzee Thomas B, Mash, Rais wa Akidi ya wale Kumi na Wawili. Mzee Mash alionekana kukerwa kwamba Nabii alikuwa amewaita washiriki wawili wa Akidi yake kwenda Uingereza bila kushauriana naye. WakatiJoseph alipokutana na Mzee Mash, hisia zote za kuumiza ziliwekwa pembeni, na Nabii alipokea ufunuo wa ajabu. Sasa ni sehemu ya 112 ya Mafundisho na Maagano.20 Inatoa maelekezo ya ajabu kutoka mbinguni kuhusu unyenyekevu na kazi ya umisionari.Aya ya 10 inasema,”Jinyenyekeze,” na Bwana wako atakuongoza kwa mkono, na kukupa jibu la sala zako.”21

Ufunuo huu ulitokea siku ile ile hasa ambayo Wazee Kimball, Hyde, na John Goodson, wakijawa na unyenyekevu, walikuwa wanatangaza Urejesho wa injili ya Yesu Kristo katika Kanisa la Vauxhall lililopo Preston, Uingereza.22 Hii ilikuwa mara ya kwanza Wamisionari kutangaza injili ya urejesho nje ya Amerika Kaskazini katika kipindi hiki. Nguvu yao ya umisionari ilileta matokeo takribani mara moja ubatizo wa waongofu na ikaleta waumini wengi waaminifu.23

Sehemu za baadaye za ufunuo zinatoa mwongozo kwa juhudi za umisionari katika siku zetu. Zinasema katika sehemu, “Yeyote mtakayemtuma katika jina langu … atakuwa na uwezo wa kufungua mlango wa ufalme wangu kwa taifa lolote … ilimradi watajinyenyekeza wenyewe mbele zangu, na kukaa katika neno langu, na kusikiliza sauti ya Roho wangu.24

Unyenyekevu ambao ulikuwa tayari katika juhudi hii isiyoelezeka ya umisionari ulimruhusu Bwana kuanzisha Kanisa Lake katika njia ya ajabu.

Kwa shukrani, tunaendelea kuona hii katika Kanisa leo. Waumini, pamoja na kizazi kinachochipuka, wanaacha muda wao na kuahirisha masomo na ajira kutumikia misheni. Waumini wengi wakubwa wanaacha ajira na kufanya dhabihu zingine ili kumhudumia Mungu katika nafasi yoyote wanayoitwa. Haturuhusu masuala binafsi kutuvuruga au kutupotosha kukamilisha azma yake.25 Huduma ya Kanisa inahitaji unyenyekevu. Tunahudumia kwa unyenyekevu jinsi tulivyoitwa kwa moyo wetu, akili, na nguvu. Katika kila daraja la Kanisa, ni muhimu kuelewa sifa kama ya Kristo ya unyenyekevu.

Kila siku Unyenyekevu ni Muhimu katika Kusaidia Kutayarisha Watu binafsi Kukutana na Mungu

Lengo la kumheshimu Bwana na kujitoa wenyewe kwa mapenzi yake26 haithaminiwikatika jamii ya leo kama ilivyokuwa hapo zamani. Baadhi ya viongozi wa Kikristo wa imani zingine wanaamini tunaishi katika ulimwengu wa Kikristo uliopita.27

Kwa vizazi, maadili ya unyenyekevu yenye msingi wa kidini na maadili ya kiraia ya staha na kutoeleza ukweli vimekuwa viwango vikuu.

Katika ulimwengu wa leo, kuna ongezeko la mkazo juu ya kiburi, kujiongezea, na kile kinachoitwa “uhalisia” ambao wakati mwingine unaongoza kwenye kukosa unyenyekevu wa kweli. Baadhi wanapendekeza thamani ya uadilifu kwa furaha leo inajumuisha “kuwa halisi, kuwa mwenye nguvu, kuwa wenye kuzalisha—na cha muhimu zaidi usitegemee watu wengine … kwa sababu majaliwa yako … yapo mikononi mwako mwenyewe.”28

Maandiko yanasisitizia njia tofauti.Yanapendekeza kwamba hatuna budi kuwa wafuasi wa kweli wa Kristo.Hii inalazimisha kuanzisha hisia ya nguvu ya uwajibikaji kwa Mungu na njia ya unyenyekevu maishani. Mfalme Benyamini alifundisha kwamba mwanadamu wa kawaida ni adui kwa Mungu na alisisitizia kwamba tunahitaji kukubali wenyewe “ushawishi wa Roho Mtakatifu.”Alielezea, miongoni mwa vitu vingine, kwamba hii inahitaji kuwa “mtiifu, mpole, mnyenyekevu, mvumilivu, [na] mwenye upendo tele.”29

Baadhi wanatumia vibaya uhalisia kama kusherekea binadamu wa kawaida na sifa ambazo ni kinyume na unyenyekevu, upole, huruma, msamaha na ungwana. Tunaweza kusherekea upekee wetu binafsi kama watoto wa Mungu bila kutumia uhalisia kama kisingizio cha tabia isiyofanana na kama ya Kristo.

Katika utafutaji wetu wa unyenyekevu, mtandao wa kisasa unazua changamoto katika kuepuka kiburi. Mifano miwili ni njia ya kujikweza “nitazame” au kushambulia wengine kwa kujigamba katikavyombo vya habari vya kijamii. Mfano mmoja zaidi ni “kujikweza kwa unyenyekevu.” Inafafanuliwa kama “staha iliyobashiriwa au maelezo yanayojipinga [au picha] ambayo azma yake ya kweli ni kuvutia usikivu kwa kitu fulani ambacho kimojawapo ni kiburi.”30 Manabii siku zote wameonya kuhusu kiburi na usisitizaji wa vitu visivyofaa vya ulimwengu.31

Ufifiaji uliosambaa wa mijadala ya kiraia pia unasikitisha. Kanuni ya milele ya uhuru wa kujiamulia huhitaji kwamba tuheshimu chaguzi nyingi ambazo hatukubaliani nazo. Mizozo na ubishi mara nyingi huvunja “mipaka ya heshima ya kawaida.”32 Tunahitaji zaidi staha na unyenyekevu.

Alma anaonya dhidi “kuwa na majivuno katika mioyo yenu,”“kudhania kwamba nyinyi ndiyo mlio bora kuliko wengine,” na kuwatesa walio wanyenyekevu ambao “wanatembea kulingana na mpango mtakatifu wa Mungu.”33

Nimepata wema wa kweli miongoni mwa watu wa imani zote ambao ni wanyenyekevu na wanaohisi kuwajibika kwa Mungu. Wengi wao wanamuunga mkono nabii Mika wa Agano la Kale, aliyetangaza, ”Bwana anataka nini kwako, ila kutenda haki, na kupenda rehema na kwenda kwa unyenyekevu na Mungu wako?”34

Wakati tu wanyenyekevu kikweli, tunaomba msamaha na kusamehe wengine. Tunaposoma katika Mosia, Alma alifundisha kwamba tunapotubu kila mara, Bwana atatusamehe makosa yetu.35 Kwa upande mwingine, kama ilivyooneshwa katika Sala ya Bwana,36 wakati tusipowasamehe makosa wengine tunajiletea wenyewe hukumu.37 Kwa sababu ya Upatanisho wa Yesu Kristo, kupitia toba dhambi zetu zinasamehewa.Wakati hatuwasamehe wale ambao wanatukosea, kwa kweli tunakataa Upatanisho wa Mwokozi.Kuwa na kinyongo na kukataa kusamehe na kukataa njia ya kujinyenyekeza katika mauhusiano yetu katika njia ya kuwa kama Kristo kwa kweliinatuletea hukumu. Kuwa na kinyongo ni sumu kwa roho zetu.38

Wacha mimi pia ni waonye dhidi ya aina yoyote ya ufidhuli. Bwana, kupitia nabii Moroni, huonesha tofauti wazi kati ya wenye kujigambana wanyenyekevu: “Wajinga wanadhihaki, lakini wataomboleza; na rehema yangu inatosha kwa wapole.” Bwana alitangaza zaidi, “Ninawapatia watu udhaifu ili katika udhaifu wao wawe wanyenyekevu; na neema yangu inatosha watu wote ambaohujinyenyekeza mbele yangu; kwani wakijinyenyekeza mbele yangu, na kuwa na imani ndani yangu, ndipo nitafanya vitu dhaifu kuwa vya nguvu kwao.”39

Unyenyekevu pia ni pamoja na kuwa mwenye shukrani kwa ajili ya baraka nyingi na msaada mtakatifu.Unyenyekevu sio mafanikio fulani makubwa yanayotambulika au hata kushinda changamoto fulani kubwa. Ni isharaya nguvu za kiroho.Ni kuwa na utulivu wa kujiamini kwamba siku hadi siku na saa baada ya saa tunaweza kumtegemea Bwana, kumhudumia Yeye, na kufanikisha azma Zake. Ni maombi yangu kwamba katika ulimwengu huu wenye ushindani tutaendelea kujitahidi kwa unyenyekevu wa kweli kila siku. Shairi kipenzi linasema hivi:

Majaribu ya ukubwa ni njia

Mtu hukutana na milele na Kila Siku.40

Ninatoa ushahidi wa kweli wa Mwokozi na Upatanisho Wake na umuhimu uliozidi wa kumhudumia Yeye kinyenyekevu kila siku.Katika jina la Yesu Kristo, amina

Muhtasari

  1. Kathy Lette, in “Town and Country Notebook,” ed. Victoria Marston, Country Life, June 7, 2017, 32; emphasis added.

  2. Annie Tempest, “Tottering-by-Gently,” Country Life, Oct. 3, 2012, 128.

  3. OnaZaburi 90:4.. Yawe ni mafupi au marefu kulingana na miaka ya duniani, maisha yetu ni mafupi sana kutoka na matazamo wa milele. wakati wote ni kama siku moja kwake Mungu, na wakati hupimwa tu na watu.Alma 40:8 Mtume Petro alitangaza, “Lakini, wapenzi, msilisahau neno hili, kwamba kwa Bwana siku moja ni kama miaka elfu, na miaka elfu ni kama siku moja”(2 Petro 3:8

  4. (Ona Musa 1:6–9. Huyu ni Kristo akiongea kwa mamlaka ya kiungu (onaTeachings of Presidents of the Church: Joseph Fielding Smith[2013], 47, tanbihi 11).

  5. Musa 1:10.

  6. Musa 1:39.

  7. 2 Nefi 26: 33; ona pia Mafundisho na Maagano 1:34–35; 35:16; Tamko Rasmi 2

  8. Mafundisho na Maagano 20:37 huanza, “Wale wote wenye kunyenyekea wenyewe mbele za Mungu.” Kisha inaeleza masharti ya ubatizo Ona pia Mathayo 11:28.

  9. Ona Mafundisho na Maagano 8:37.

  10. Tunajua kama hatutatubu, tukappokea maagizo, na kufuata njia ya gano ambayo utuandaa kwa ajili ya milele, “siku ya kiza (huja) ambapo hamna kazi itafanyika.”(Alma 34:33).

  11. Ona 3 Nefi 27:27.

  12. Alma 34:32

  13. Ona 1 Nefi 11:26–33; 2 Nefi 9:53; Yakobo 4:7; Mafundisho na Maagano 122:8.

  14. Alma 5:26.

  15. Alma 5:27.

  16. Ona Alma 4:19.

  17. Joseph Smith, in Heber C. Kimball, “History of Heber Chase Kimball by His Own Dictation,” ca. 1842–1856, Heber C. Kimball Papers, 54, Church History Library; see also Orson F. Whitney, Life of Heber C. Kimball, an Apostle; the Father and Founder of the British Mission (1888), 116.

  18. Heber C. Kimball, “History of Heber Chase Kimball by His Own Dictation,” 54; see also Orson F. Whitney, Life of Heber C. Kimball, 116.

  19. President J. Reuben Clark Jr. taught: “In the service of the Lord, it is not where you serve but how. In the Church of Jesus Christ of Latter-day Saints, one takes the place to which one is duly called, which place one neither seeks nor declines” (in Conference Report, Apr. 1951, 154).

  20. Ona The Joseph Smith Papers, Documents, Volume 5: October 1835–January 1838, ed. Brent M. Rogers and others (2017), 412–17. Vilate Kimball reported in a letter to her husband, Heber C. Kimball, that she had copied the revelation from “Elder Marshs book as he wrote it from Josephs mouth” (Vilate Murray Kimball to Heber C. Kimball, Sept. 6, 1837, Heber C. Kimball, Correspondence, Church History Library).

  21. Mafundisho na Maagano 112:10; mkazo umeongezewa.

  22. Ona Orson F. Whitney, Life of Heber C. Kimball, 136–37.

  23. Ona Orson F. Whitney, Life of Heber C. Kimball, 149.

  24. Mafundisho na Maagano 112:21-22; mkazo umeongezewa.

  25. “While we do not ask to be released from a calling, if our circumstances change it is quite in order for us to counsel with those who have issued the call and then let the decision rest with them” (Boyd K. Packer, “Called to Serve,” Ensign, Nov. 1997, 8).

  26. Ona “Humility,” in chapter 6 of Preach My Gospel: A Guide to Missionary Service (2004), 120.

  27. Ona Charles J. Chaput, Strangers in a Strange Land (2017), 14–15; ona pia Rod Dreher, The Benedict Option (2017).

  28. Carl Cederstrom, “The Dangers of Happiness,” New York Times, July 19, 2015, 8.

  29. Mosia 3:19

  30. English Oxford Living Dictionaries, “humblebrag,” en.oxforddictionaries.com/definition/humblebrag.

  31. Kwa njia fulani hii inapiga mwangwi maeneo ya Alma ambayo yanaeleza wale ambao walikuwa wamepata “ kila aina ya vitu vya thamani, ambavyo walikuwa wamepata kwa sababu ya bidii yao; … [lakini] na walijivuna kwa macho yao” (Alma 4:6). Inaonekana wazi kwamba “majivuno ya unynyekevu” bado ni majivuno.

  32. David Brooks, “Finding a Way to Roll Back Fanaticism,” New York Times, Aug. 15, 2017, A23.

  33. Alma 5:53, 54.

  34. Mika 6:8

  35. Ona Mosia 26:30.

  36. Ona Mathayo 6:12, 15.

  37. Ona Mosia 26:31.

  38. As Nelson Mandela said, “Resentment is like drinking poison and then hoping it will kill your enemies” (in Jessica Durando, “15 of Nelson Mandela’s Best Quotes,” USA Today, Dec. 5, 2013, usatoday.com).

  39. Etheri 12:26, 27; mkazo umeongezewa.

  40. Edmund Vance Cooke, “The Eternal Everyday,” Impertinent Poems (1907), 21.