2010–2019
Safari Inaendelea!
Oktoba 2017


Safari Inaendelea!

Safari ya kurudi kwa Baba yetu wa Mbinguni ni safari muhimu ya maisha yetu.

Miaka mia moja na sabini iliyopita, Brigham Young alitazama ng’ambo ya Bonde la Salt Lake kwa mara ya kwanza na kutangaza, “Hapa ndipo mahali sahihi!”1 Alijua eneo kwa sababu Bwana alimfunulia.

Mpaka 1869, zaidi ya watakatifu 70,000 walikuwa wamefanya safari kama hiyo. Bila kujali tofauti zao nyingi za lugha, tamaduni, na utaifa, walishiriki ushuhuda wa Baba, Mwana na Roho Mtakatifu, Urejesho wa injili ya Yesu Kristo, na tamaa ya kuijenga Sayuni—mahali pa amani, furaha, na uzuri kwa maandalizi ya Ujio wa Pili wa Mwokozi.

Picha
Jane Manning James

Mmoja wa Watakatifu hao kuwasili Utah alikuwa Jane Manning James—binti wa mtumwa aliyeachwa huru, muongofu wa Kanisa la urejesho, na mfuasi wa ajabu aliyekumbana na changamoto ngumu. Dada James alibaki Mtakatifu wa Siku za Mwisho mwaminifu mpaka kifo chake mnamo 1908.

Aliandika: “Nataka kusema hapa hapa, kwamba imani yangu katika injili ya Yesu Kristo, kama ilivyofundishwa na Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa siku za Mwisho, ni imara leo, la, kama inawezekana ni imara kuliko ilivyokuwa siku nilipobatizwa mara. Ninalipa zaka zangu na matoleo, ninashika neno la hekima, ninalala mapema na kuamka mapema, najaribu katika udhaifu wangu kuwa mfano mzuri kwa wote.”2

Dada James, kama Watakatifu Siku za Mwisho wengi sana, sio tu wanaijenga Sayuni kwa damu, jasho, na machozi lakini pia hutafuta baraka za Bwana kupitia kuishi misingi ya injili kadiri anavyoweza akisimama imara katika imani kwa Yesu Kristo—mponyaji mkuu kwa wote wanaomtafuta kwa uaminifu.

Watakatifu wa mwanzo hawakuwa wakamilifu, lakini walijenga msingi ambao juu yake tunajenga familia na jamii ambazo hupenda na kutunza maagano, ambayo imesisitizwa katika habari mbalimbali ulimwenguni kote kwa sababu ya wajibu wetu kwa Yesu Kristo na juhudi zetu za kujitolea kusaidia walio karibu na mbali sana.3

Rais Eyring, naomba niongeze shukrani kwa miongo ya maelfu ya malaika wa sharti za manjano wanaohudumu Texas, Mexico, na sehemu zingine.

Nina imani kubwa kwamba kama tukipoteza muunganiko wetu kwa wale waliotangulia mbele yetu, ikijumuisha waanzilishi baba zetu wa mwanzo na mama zetu, tutapoteza hazina yetu ya thamani sana. Nimezungumza kuhusu “Imani katika Kila Hatua” katika siku za nyuma na nitaendelea katika siku za baadae kwa sababu ninajua kwamba kizazi kinachochipuka lazima kiwe na aina ile ile ya imani waliyokuwa nayoWatakatifu wa mwanzo katika Bwana Yesu Kristo na injili Yake ya urejesho.4

Mababa zangu na mama zangu watanulizi walikuwa kati ya hao waanzilishi waaminifu ambao walisukuma mkokoteni, waliendesha magari ya kukokotwa na farasi, na kutembea kwenda Utah. Wao, kama Dada Jane Manning James, walikuwa na imani kubwa katika kila moja ya hatua zao wakati walipofanya safari zao wenyewe.

Shajara zao zimejaa maelezo ya ugumu, njaa, na ugonjwa na pia shuhuda za imani yao kwa Mungu na injili ya urejesho ya Yesu Kristo.

Walikuwa na vitu vichache vya dunia lakini walifurahia wingi wa baraka kutoka kwa undugu wa kaka na dada waliopatakatika Kanisa la Yesu Kristo. Walipoweza, waliwainua walioanguka na kuwabariki wagonjwa kupitia huduma mmoja kwa mwingine na kwa ukuhani wa Mungu.

Kina dada huko Cache Valley, Utah, waliwatumikia Watakatifu katika roho ya Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama kwa “kufanya kazi kwa umoja kusaidia wenye mahitaji.”5 Bibi yangu mkuu Margaret McNeil Ballard alitumikia pamoja na mumewe, Henry, alipokuwa akisimamiakama askofu wa Kata ya Logan Second kwa miaka 40. Margaret alikua rais wa kata wa Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama kwa miaka 30kati ya hiyo. Aliwachukua masikini nyumbani kwake, wagonjwa, na wajane na yatima, na hata aliwavisha wafu mavazi yao masafi ya hekaluni.

Japokuwa ni sawa na muhimu kukumbuka safari ya Wamormoni waanzilishi wa karne ya 19, tunapaswa kukumbuka kwamba “safari kupitia maisha inaendelea!” kwa kila mmoja wetu tunapothibitisha“imani yetu katika kila hatua.”

Picha
Waumini wanakusanyika katika mikusanyiko yao

Waongofu wapya hawakusanyiki tena kwenye makazi ya waanzilishi huko magharibi ya Marekani. Badala yake, waongofu hukusanyika kwenye maeneo yao, ambapo Watakatifu humwabudu Baba yetu wa Mbinguni katika jina la Yesu Kristo. Kwa mikutano zaidi ya 30,000 iliyoundwa ulimwenguni kote, wote wanakusanyika kwenye Sayuni yao wenyewe. Kama maandiko yanavyosema, “Kwani hii ndiyo Sayuni—wenye moyo safi.”6

Tunapotembea njia ya maisha, tunajaribiwa kuona kama “tutakumbuka kufanya yale yote [Bwana] ameamuru.”7

Wengi wetu tuko kwenye safari za kuvutia za ugunduzi—inayopelekea utoshelevu binafsi na kuangazwa kiroho. Baadhi yetu, hata hivyo, tuko kwenye safari inayopelekea kwenye huzuni, dhambi, uchungu na kufa moyo.

Katika muktadha huu , tafadhali jiulize: Nini hatma ya safari yako? Hatua zako zinakupeleka wapi? Na je safari yako inakupeleka kwenye “wingi wa baraka” Mwokozi ameahidi?8

Safari ya kurudi kwa Baba yetu wa Mbinguni ni safari muhimu ya maisha yetu, na inaendelea kila siku, kila wiki, kila mwezi, na kila mwaka tunapoongeza imani yetu Kwake na kwa Mwanawe Mpendwa, Yesu Kristo.

Ni sharti tuwe makini wapi hatua zetu katika maisha zitatupeleka. Ni sharti tuwe waangalifu na kupokea ushauri wa Yesu kwa wafuasi Wake alipojibu maswali haya: “Tuambie mambo haya yatakuwa lini? Na nini dalili ya kuja kwako, na ya mwisho wa dunia?

“Na Yesu akajibu na kuwaambia, Angalieni mtu [na naongeza mwanamke] asiwadanganye.”9

Leo narudia ushauri wa mwanzo kutoka kwa viongozi wa Kanisa.

  • Kina kaka na kina dada, shikeni mafundisho ya Kristo safi na kamwe msidanganywe na wale wenye hila na injili. Injili ya Baba na Mwana ilirejeshwa kupitia Joseph Smith, nabii wa kipindi hiki cha mwisho cha maongozi ya Mungu.

  • Msiwasikilize wale ambao hawajatawazwa na/au kutengwa kwenye wito wao Kanisani na hawatambuliki na ridhaa ya pamoja ya waumini wa Kanisa.10

  • Mjihadhari na mashirika, vikundi, au watu wanaodai majibu ya siri kwa maswali ya injili kwamba wanasema manabii na mitume wa leo hawana au hawaelewi.

  • Msiwasikilize wale wanaolaghai kwa njama za kupata utajiri. Waumini wetu wamepoteza pesa nyingi sana, hivyo kuweni makini.

Katika baadhi ya maeneo, wengi wa watu wetu wanatazama zaidi ya alama na kutafuta maarifa ya siri katika matendo ya gharama na desturi tetanishi za kupata uponyaji na msaada.

Kauli rasmi ya Kanisa, iliyotolewa mwaka mmoja uliopita, inasema: “Tunawasihi waumini wa Kanisa kujihadhari kuhusu kushiriki katika kikundi chochote ambacho kinaahidi—kwa mabadilishano ya pesa—miujiza ya uponyaji au kwamba hudai kuwa na mbinu ya kufikia nguvu za uponyaji nje ya mpangilio wa wenye ukuhani waliotawazwa.”11

Kitabu cha Muongozo cha Kanisa hutushauri: ‘Waumini wasitumie njia za tiba au afya ambazo zinazua maswali kimaadili au kisheria. Viongozi wa maeneo husika wanawashauri waumini walio na matatizo ya kiafya kuwaona wataalamu wenye weledi ambao wamepewa kibali katika cha ambamo wanafanya kazi.”12

Kina dada na kina dada kuweni na busara na mjihadhari kwamba desturi kama hizo zinaweza kuvutia kimhemko lakini kwa kiasi kikubwa kuthibitika kuwa hatarishi kimwili na kiroho.

Kwa babu zetu waanzilishi, uhuru na kujitegemea ilikuwa muhimu, lakini uelewa wao wa jumuia ulikuwa muhimu vile vile. Walifanya kazi pamoja na kusaidiana kushinda changamoto za kimwili na kimhemko za wakati wao. Kwa wanaume, kulikuwa na akidi ya ukuhani, na wanawake walihudumiwa na Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama. Matokeo haya hayajabadilika katika siku yetu.

Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama na akidi za ukuhani hukidhi mahitaji ya kiroho na ya muda ya waumini wetu.

Baki katika njia ya injili kwa kuwa na “imani katika kila hatua” ili uweze kurudi salama kwa Baba yetu wa Mbinguni na Bwana Yesu Kristo. Bwana ni Mwokozi wetu wa thamani. Yeye ndiye Mkombozi wa ulimwengu. Tunapaswa kutukuza jina Lake takatifu na kamwe tusilitumie vibaya kwa njia yoyote ile, tujitahidi kutii amri Zake. Tukifanya hivyo, atatubariki na kutuongoza kurudi salama nyumbani.

Ninamwalika kila mmoja ndani ya uvumi wa sauti yangu kukaribia na kumkumbatia yeyote anayefanya safari yake leo, bila kujali wamefika wapi katika safari yao.

Kumbukeni hakuna baraka kuu mtu yeyote anaweza kushiriki kuliko ujumbe wa Urejesho, ambao ukipokelewa na kuuishi, kuna ahadi ya furaha ya milele na amani—hata uzima wa milele. Acha tutumie nguvu zetu, uwezo, na shuhuda katika kuwasaidia wamisionari wetu kutafuta, kufundisha, na kubatiza watoto wa Mungu ili wawe na nguvu ya mafundisho ya injili ikiongoza maisha yao ya kila siku.

Tunapaswa kuwakumbatia watoto wa Mungu kwa huruma na kuondoa chuki yoyote ikiwemo tofauti ya rangi, jinsia, na utaifa. Acha isemekane kwamba tunaamini kiukweli baraka za injili ya urejesho ya Yesu Kristo zipo kwa kila mtoto wa Mungu.

Ninashuhudia kwamba “safari inaendelea,” na ninawaalika kubaki katika njia ya injili mnapoendelea kusonga mbele kwa kuwafikia watoto wote wa Mungu kwa upendo na huruma kwamba kwa kuungana tufanye mioyo yetu safi na mikono yetu safi kupokea “wingi wa baraka” zinazowasubiri wote wampendao Baba yetu wa Mbinguni na Mwanawe Mpendwa, ambazo kwazo kwa unyenyekevu ninaomba katika jina la Yesu Kristo, amina.