2010–2019
Ukuhani na Nguvu za Upatanisho wa Mwokozi
Oktoba 2017


Ukuhani na Nguvu za Upatanisho wa Mwokozi

Ili makusudi ya Baba wa Mbinguni yaweze kutimizwa, nguvu za Kristo za upatanisho zinahitaji kupatikana kwa watoto wa Mungu. Ukuhani hutoa nafasi hizo.

Piga twasira pamoja nami ya roketi ikiwekwa sawa kwenye jukwaa la kurushia ili iweze kutayarishwa kwa kurushwa. Sasa, piga taswira ikiwashwa. Mafuta, katika mwako uliodhibitiwa, unabadilishwa na kuwa hewa ya moto ambayo inatapikwa nje, ikitoa msukumo muhimu kuendesha roketi kwenda angani. Hatimaye, fikiria shehena au mzigo ambao umebebwa juu ya rocketi. Thamani ya shehena inaeleweka kikamilifu tu inapofika kule inakotakiwa kuwa na kufanya kazi kama inavyotakiwa. Huhitaji kuwa mwana sayansi wa roketi kuelewa kwamba setelaiti ya thamani kubwa ya mawasiliano duniani ni ya thamani ndogo ikiwa imekaa ghalani. Kazi maalumu ya roketi ni kupeleka shehena tu.

Jioni hii ningependa kufananisha ukuhani ambao tunao na roketi na nafasi ya kunufaika kutoka nguvu za upatanisho za Mwokozi na shehena ambayo roketi inapeleka.

Kwa sababu ya dhabihu ya upatanisho Wake,Yesu Kristo ana uwezo na mamlaka kukomboa binadamu wote. Kufanya nguvu Zake za upatanisho zipatikane, amenaibisha sehemu ya nguvu Zake na mamlaka kwa wanaume duniani. Hizi nguvu zilizonaibishwa na mamlaka huitwa ukuhani. Huruhusu wenye ukuhani kumsaidia Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo katika kazi yao, kuleta wokovu na kuinuliwa kwa watoto Wake. Hufanya hivyo kwa sababu zinawapa watoto Wake nafasi ya kupokea baraka za nguvu za upatanisho za Mwokozi.

Nguvu za upatanisho wa Yesu Kristo ni muhimu kwa sababu hakuna kati yetu anayeweza kurudi nyumbani kwetu Mbinguni bila msaada. Katika maisha ya hapa duniani, siku zote tunafanya makosa na kukiuka amri za Mungu. Tunakuwa na madoa ya dhambi na hatuwezi kuruhusiwa kurudi kuishi katika uwepo wa Mungu. Tunahitaji nguvu za upatanisho za Mwokozi ili kwamba tuweze kupatanishwa na Baba wa Mbinguni. Yesu Kristo alivunja kamba za kifo kimwili, kuruhusu ufufuko kwa wote. Anatoa msamaha wa dhambi, kwa masharti ya utii wa sheria na ibada za injili. Kupitia Yeye, kuinuliwa hutolewa. Nafasi ya kunufaika kutokana na nguvu za upatanisho za Mwokozi ni shehena ya muhimu sana ya uumbaji.

Ili makusudi ya Baba wa Mbinguni yaweze kutimizwa, nguvu za upatanisho za Kristo zinahitaji kupatikana kwa watoto wa Mungu.1 Ukuhani hutoa nafasi hizo. Ndiyo roketi. Ukuhani ni muhimu kwa sababu ibada muhimu na maagano duniani hutawaliwatu kwa mamlaka yake. Kama ukuhani ukishindwa kuleta nafasi ya kunufaika kutokana na nguvu za upatanisho wa Mwokozi, ni nini itakuwa kazi yake? Je, itakuwa tu ni kitu cha kuvuta nadhari changamani? Mungu anadhamiria ukuhani utumike tu zaidi ya darasa Jumapili au kama nafasi ya huduma. Anadhamiriakwa ajili ya kupeleka shehena.

Dosari ndogondogo katika roketi zinaweza kusababisha kushindikana kwa safari. Vizingio na vifaa vilivyochoka vinaweza kusababisha roketi kutofanya kazi vizuri. Kulinda ukuhani kutokana na vizingio na vifaa vilivyochoka kiisitiari, Mungu analinda vyote utunikiaji na matumizi.2 Utunukiaji wa Ukuhani unalindwa na funguo za Ukuhani, ambazo ni haki ya urais inayopewa mwanaume.3 Matumizi ya Ukuhani vilevile yanalindwa na funguo za ukuhani bali pia kwa maagano ambayo mwenye Ukuhani hufanya. Matumizi ya ukuhani basi yanatawaliwa na yote funguo za ukuhani na maagano. Wajibu wa ukuhani kwa mtu hutolewa kibinafsi na hauwezi kuwapo bila yeye;4 ukuhani sio chanzo kisicho na umbo maalum cha nguvu huru.

Wote ukuhani wa Haruni na Melkizedeki hupokelewa kwa agano.5 Mungu anaamua masharti na mwanaume anakubali.Kuzungumza kwa mapana, wenye ukuhani wanafanya maagano kumsaidia Mungu katika kazi Yake. Mapema katika kipindi hiki cha mwongozo wa Mungu, Yesu Kristo alielezea kwamba agano la ukuhani “linadhibitishwa juu yenu kwa ajili yenu na sio kwa ajili yenu tu, bali kwa ajili ya ulimwengu wote … kwa sababu hawaji kwangu.“6

Hii inafundisha kwamba madhumuni ya ukuhani ni kuwaalika wengine waje kwa Kristo kwa kuwasaidia kupokea injili ya urejesho. Tuna ukuhani ili kwamba tuweze kuwasaidia watoto wa Baba wa Mbinguni wapunguziwe mzigo wa dhambi na kuwa kama Yeye. Kupitia ukuhani, nguvu za uungu zimedhihirika katika maisha ya wote wanaofanya na kushika maagano ya injili na kupokea ibada husika.7 Hii ndiyo njia kila mmoja wetu huja kwa Kristo, anatakaswa, na anapatanishwa na Mungu. Nguvu za upatanisho wa Kristo huwezesha kupatikana kupitia ukuhani, ambao unapeleka shehena.

Maagano na Mungu ni ya maana muhimu sana na ni ya taadhima. Mtu hana budi kujitayarisha kwa, kujifunza kuhusu, nakuingia maagano kama haya na kuyaiheshimu. Agano linakuwa ahadi ya binafsi. Kufafanua zaidi maandishi ya Robert Bolt mwandishi wa tamthilia Muingereza, mtu anafanya maagano tu wakati anataka kujipa sharti mwenyewe kwa njia ya pekee kwa ahadi.Anafanya utambuzi kati ya ukweli wa ahadi na uadilifu wake mwenyewe. Wakati mtu anafanya agano, anajishikilia mwenyewe, kama maji, katika mikono yake iliyoumika. Na kama atafungua vidole vyake, hahitaji kutegemea kujikuta mwenyewe tena. Mvunjaji agano hana tena nafsi ya kuweka sharti au kudhamini toleo.8

Mwenye ukuhani wa Haruni anaahidi kuepuka uovu, kusaidia wengine kupatana na Mungu, na kujitayarisha kupokea Ukuhani wa Melkizedeki.9 Majukumu haya matakatifu yanatimizwa wakati anafundisha, kubatiza, kuwaimarisha waumini wa Kanisa, na kuwaalika wengine kukubali injili.Hizi ni kazi za “roketi” yake Kama malipo, Mungu anaahidi matumaini, msamaha, huduma ya malaika, na funguo za injili ya toba na ubatizo.10

Mwenye ukuhani wa Melkizedekianaahidi kutimiza wajibu unaohusiana na Ukuhani wa Haruni na kutukuza wito wake katika Ukuhani waMekizedeki.11 Anafanya hivyo kwa kushika amri zinazohusiana na agano. Amri hizi ni pamoja kuwa na “bidii kusikiliza maneno ya uzima wa milele” kwa kuishi kwa “kila neno ambalo linatoka kwenye mdomo wa Mungu,”12 likibeba ushuhuda wa Yesu Kristo na kazi Yake ya siku za mwisho,13 sio kujisifu yeye mwenyewe,14 na kuwa rafiki ya Mwokozi, kumwamini Yeye kama ambavyo rafiki angefanya.15

Kama malipo, Mungu anaahidi kwamba mwenye Ukuhani wa Melkizedeki atapokea funguo za kuelewa siri za Mungu. Atakuwa mkamilifu ili kwamba anaweza kusimama katika uwepo wa Mungu.Ataweza kukamilisha wajibu wake katika kazi ya wokovu.Yesu Kristo atatayarisha njia mbele ya mwenye ukuhani na atakuwa pamoja naye. Roho Mtakatifu atakuwa ndani ya moyo wa mwenye ukuhani na malaika watambeba. Mwili wake utaimarishwa na kufanywa upya. Atakuwa mrithi kwa baraka za Ibrahimu na, pamoja na mke wake, mrithi pamoja na Yesu Kristo kwenye ufalme wa Baba wa Mbinguni.16 Hizi ni “ahadi za thamani na zilizozidi kwa ukubwa.”17 Hakuna ahadi kubwa zinazoweza kufikiriwa.

Kwa kila mtu anayepokea Ukuhani wa Melkizedeki, Mungu anadhibitisha agano Lake na huahidi kwa kiapo.18 Kiapo hiki kinafungamana tu kwa Ukuhani wa Melkizedeki,19 na ni Mungu anaeapa kiapo, sio mwenye Ukuhani.20 Kwa sababu hii hali ya kipekee inahusisha nguvu Zake tukufu na mamlaka, Mungu hutumia kiapo, akitumia kadiri awezavyo lugha yenye nguvu sana, kutuhakikishia juu ya ahadi Zake za asili zinazofunga na zisizobadilika.

Matokeo makali yanatokea kutokana na kuvunja maagano ya ukuhani nakwa pamoja kuzigeuka.21 Kuwa holelaholela au wa kutojali katika wito wa ukuhani ni kama kuweka vifaa vilivyochoka kwenye sehemu ya roketi. Inahatarisha agano la ukuhani kwa sababu inaweza kuongoza kwenye kushindwa kwa safari.Kutotii Amri za Mungu huvunja agano. Kwa mvunja agano wa kudumu, asiyetubu, ahadi zilizoahidiwa zinaondolewa.

Nilikuja kuelewa kwa undani zaidi uhusiano kati ya roketi ya “ukuhani” na “nafasi ya kunufaika kutokana na shenena ya nguvu za upatanisho wa Kristo” miaka kadha iliyopitaWakati wa mwisho wa wiki, nilipangiwa kazi mbili. Moja ilikuwa kuanzisha kigingi cha kwanza katika nchi, na ingine ilikuwa ni kumsaili kijana na, kama yote yangekwenda vizuri, kumrudishia ukuhani na baraka zakeza hekaluni. Huyu mtu mzima wa miaka 30 alikuwa amejiunga na kanisa katika miaka yake ya mwisho ya ujana. Alihudumia misheni kwa heshima. Lakini aliporudi nyumbani, alipotea njia, na alipoteza uumini wake wa Kanisa. Baada ya miaka kadhaa, “alijitambua,”22 na kwa msaadawa viongozi wenye upendo wa ukuhani na waumini wenye huruma, alitubu na akarudishwa kwa ubatizo katika kanisa.

Baadaye, aliomba kuwa na ukuhani na baraka zake za hekaluni zirejeshwe. Tulipanga miadi ya Jumamosi saa nne asubuhi kwenye jumba la mikutano. Wakati nilipofika kwa ajili ya saili za mapema, tayari alikuwa pale. Alikuwa na dukuduku mno kuwa na ukuhani mara ingine tena, ni kwamba hakuweza kungojea.

Wakati wa usaili wetu, nilimwonyesha barua nikielezea kwamba RaisThomas S. Monsonamechunguza binafsi maombi yake na kuruhusu usaili. Huyu kijana kwa upande mwingine mvumilivu alilia. Na kisha nilimwambia kwamba tarehe ya usaili wetu haitakuwa na maana rasmi katika maisha yake. Alionekana kushangazwa. Nilimfahamisha kwamba baada ya mimi kurejesha baraka zake, rekodi yake ya ushiriki ingeonesha tu ubatizo wake wa kwanza, kudhibitishwa, kutawazwa ukuhani, na tarehe ya endomenti. Alipaliwa tena.

Nilimwomba asome kutoka Mafundisho na Maagano:

“Tazama, yule ambaye ametubu dhambi zake, huyu anasamehewa, na Mimi, Bwana, sizikumbuki tena.

Kwa hili mnaweza kujua kama mtu ametubu dhambi zake—tazama, ataziungama na kuziacha.”23

Machozi yalijaa machoni mwake kwa mara ya tatu. Kisha, niliweka mikono yangu juu ya kichwa chake na katika jina la Yesu Kristo na kwa mamlaka ya Ukuhani wa Malkizedeki, na kwa ithini ya Rais waKanisa, nikarejesha ukuhani wake na baraka zake za hekaluni.

Furaha iliyokuja juu yetu ilikuwa kubwa sana. Alijua alikuwa kwa mara ingine ameruhusiwa kushikilia na kutumia ukuhani wa Mungu. Alijua kwamba baraka zake za hekaluni zilikuwa tena zikifanya kazi sawasawa.Alikuwa anadundadunda katika hatua zake na nuru angavu imemzunguka. Nilijivunia kwa ajili yake na nilihisi jinsi Baba wa Mbinguni alivyojivuna kwa ajili yake pia.

Baada ya hapo, kigingi kilianzishwa. Mikutano ilihudhuriwa vizuri na Watakatifu waaminifu, wenye shauku, na urais wa kigingi wa ajabu uliidhinishwa. Hata hivyo, kwangu mimi tukio la kihistoria la kuanzisha hiki kigingi cha kwanza katika inchi ilifunikwa na furaha niliyohisi katika kurejesha baraka kwa kijana huyu.

Nimekuja kutambua kwamba kusudi la kuanzisha kigingi, au kutumia ukuhani wa Mungu kwa njia yoyote, ni kumsaidia Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo katika kazi yao—kutoa nafasi kwa ajili ya wokovu na kuinuliwa kila mmoja wa watoto wa Mungu. Kama roketi ambayo kusudi lake ni kupeleka shehena, ukuhani unapeleka injili ya Yesu Kristo, kuwezesha wote kufanya maagano na kupokea ibada zinazohusika. “Damu ya upatanisho wa Kristo”24 inaweza palepale kutumika katika maisha yetu tunapopata uzoefu wa ushawishi wa kutakasa wa Roho Mtakatifu na kupokea ahadi ambazo Mungu huahidi.

Katika kuongeza kutii amri na ibada za injili ninyi wenyewe, ninawalika mfanye na kushika maagano ya ukuhani. Pokeeni kiapo cha Mungu na ahadi Zake. Tukuzeni wajibu wenu katika ukuhani kumsaidia Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo.Tumieni ukuhani kusaidia kupeleka fursa ya kunufaika kutokana na nguvu za upatanisho wa Mwokozi kwa niaba ya mtu mwingine!Mtakapofanya hivyo, baraka kubwa zitakuja kwenu na familia zenu.Ninashuhudia kwamba Mkombozi yu hai na anaelekeza kazi yake, katika jina la Yesu Kristo,amina