2010–2019
Bwana anaongoza Kanisa Lake
Oktoba 2017


Bwana Anaongoza Kanisa Lake

Uongozi wa Bwana wa Kanisa Lake unahitaji imani kubwa na isiyoyumba kutoka kwa wote wanaomtumikia Duniani.

Kaka zangu mlio na ukuhani wa Mungu, jioni ya leo natamani kuongea kuhusu njia ya ajabu ambayo Bwana huongoza ufalme Wake hapa duniani. Tayari unajua misingi: Ninaomba kwamba Roho Mtakatifu ataithibitisha kwenu.

Kwanza, Yesu Kristo ni kichwa cha Kanisa katika ulimwengu wote.

Pili, Anaongoza Kanisa Lake leo kwa kuzungumza kwa wanaume walioitwa kama manabii, na Yeye hufanye hivyo kupitia ufunuo.

Tatu, Alitoa ufunuo kwa manabii Wake zamani, bado anafanya hivyo, na ataendelea kufanya hivyo.

Nne, Anatoa ufunuo wa kuthibitisha kwa wale wanaotumikia chini ya uongozi wa manabii Wake.

Kutoka katika misingi hiyo, tunagundua kwamba Uongozi wa Bwana wa Kanisa Lake unahitaji imani kubwa na isiyoyumba kutoka kwa wote wanaomtumikia duniani.

Kwa mfano, inahitaji imani kuamini kwamba Bwana aliyefufuliwa kila siku anaangalia kila kitu cha ufalme Wake. Inahitaji imani kuamini kwamba Yeye uwaita watu wasio wakamilifu katika nafasi za uaminifu. Inachukua imani kuamini kwamba Anajua watu Anaowaita kwa ukamilifu, vyote uwezo wao na uwezekano wao, na hivyo hafanyi makosa katika miito Yake.

Hilo linaweza kuleta tabasamu au kutikisa kwa kichwa kwa baadhi katika hii hadhira—wote wanaofikiri wito wao wenyewe wa kutumikia ulikuwa ni kosa pamoja na wale ambao wanaoona baadhi ya wanaowajua ambao wanaonekana kuwa sio halali kwa nafasi yao katika ufalme wa Bwana. Ushauri wangu kwa makundi yote mawili ni kuchelewesha hukumu hizo mpaka uweze kuona vizuri kile Bwana anaona. Hukumu unayohitaji kufanya, badala yake, ni kwamba wewe una uwezo wa kupokea ufunuo na kufanya jambo hilo bila hofu.

Inahitaji imani kufanya hivyo. Inahitaji hata imani kubwa zaidi kuamini kwamba Bwana ameiwata watumishi wasio wakamilifu kukuongoza wewe. Lengo langu leo jioni ni kujenga imani yako kwamba Mungu anakuongoza katika huduma yako Kwake. Na muhimu zaidi, tumaini langu ni kujenga imani yako kwamba Bwana anawahamasisha watu wasiokuwa wakamilifu aliowaita kama viongozi wako.

Unaweza kufikiria, kwanza, kwamba imani kama hiyo si muhimu kwa mafanikio ya Kanisa la Bwana na ufalme. Hata hivyo, unaweza kugundua—bila kujali wapi ulipo katika mlolongo wa huduma ya ukuhani, kutoka kwa nabii wa Bwana hadi mmiliki mpya wa Ukuhani wa Haruni—imani hiyo ni muhimu.

Hebu tuanze na imani kile inamaanisha kwa rais wa akidi ya walimu. Ni muhimu kwake kuwa na imani kwamba Bwana alimwita mwenyewe, akijua udhaifu na nguvu za mwalimu huyu. Anapaswa kuwa na imani kwamba mtu ambaye alitoa wito alipokea ufunuo kwa Roho wa Mungu. Washauri wake na washiriki wa akidi yake wanahitaji imani sawa ya kumfuata kwa kujiamini bila hofu.

Niliona ujasiri huo wakati mvulana aliketi pamoja na urais wake wa akidi ya mashemasi Jumapili moja asubuhi. Alikuwa katibu wao mpya aliyeitwa. Urais huo wa vijana ulishauriana pamoja. Walizungumza juu ya njia kadhaa ambazo wangeweza kutimiza ombi la Askofu la kumleta kanisani mvulana asiyehudhuria kanisa. Baada ya maombi na majadiliano, walimchagua katibu kwenda nyumbani kwa kijana ambaye hajawahi kuja katika mkutano na kumkaribisha.

Katibu hakumjua mvulana, lakini alijua kwamba mmoja wa wazazi wa mvulana hakuwa mhudhuriaji kanisa na yule mwingine hakuwa muumini na mwenye kupenda urafiki. Katibu alijisikia wasiwasi lakini si hofu. Alijua kwamba nabii wa Mungu alikuwa ameomba wenye ukuhani kumrudisha kondoo aliyepotea. Na alikuwa amesikia sala ya urais wake. Aliwasikia wakikubaliana juu ya jina la mvulana atakayekombolewa na jina lake mwenyewe.

Nilikuwa nikimwangalia wakati katibu akitembea kwenye mtaa kuelekea nyumba ya kijana asiyehudhuria kanisa. Alitembea polepole kama kwamba alikuwa akielekea katika hatari kubwa. Lakini akarudi tena katika nusu saa barabarani na mvulana, akitabasamu kwa furaha. Sijui yeye kama alijua wakati huo, lakini alikuwa amekwenda na imani kwamba alikuwa kwenye kazi ya Bwana. Imani hiyo imebaki naye na kukua zaidi katika miaka yake kama mmisionari, baba, kiongozi wa vijana, na askofu.

Hebu tuzungumze kuhusu imani hiyo ina maana gani kwa askofu. Askofu kwa wakati mwingine anaitwa kuwatumikia watu anaowafahamu vizuri. Waumini wa kata hujua kitu fulani cha udhaifu wake wa kibinadamu na uwezo wake wa kiroho, na wanajua kuwa wengine katika kata wangeweza kuitwa—wengine ambao wanaonekana kuelimika zaidi, wenye ujuzi, wanaofurahisha zaidi, au wanaoonekana hata vizuri zaidi.

Waumini hawa wanapaswa kujua wito wa kutumikia kama askofu ulitoka kwa Bwana, kwa ufunuo. Bila imani yao, askofu aliyeitwa na Mungu ataona vigumu kupata ufunuo anayohitaji kuwasaidia. Hataweza kufanikiwa bila imani ya waumini ili kumhimili.

Kwa furaha, kinyume chake pia ni kweli. Fikiria mtumishi wa Bwana, Mfalme Benyamini ambaye aliwaongoza watu wake kwenye toba. Mioyo ya watu ililainishwa na imani yao kwamba aliitwa na Mungu licha ya udhaifu wake kama binadamu na kwamba maneno yake yalitoka kwa Mungu Unakumbuka kile watu walisema: “Ndio, tunaamini maneno yote ambayo umetuzungumzia; … tunajua uhakika na ukweli wake, kwa sababu Roho wa Bwana Mwenyezi, ambaye ameleta mabadiliko makuu ndani yetu, au mioyoni mwetu, hata kwamba hatuna tamaa ya kutenda maovu tena, lakini kutenda mema daima”(Mosia 5:2).

Kwa kiongozi kufanikiwa katika kazi ya Bwana, imani ya watu kwamba yeye ameitwa na Mungu lazima ishinde mtazamo wao juu ya udhaifu wake na udhaifu wa kidunia. Unakumbuka jinsi Mfalme Benjamin alielezea jukumu lake mwenyewe la uongozi:

“Sijawaamuru kuja hapa ili mniogope, au kwamba mnidhanie kwamba mimi mwenyewe ni zaidi ya binadamu.

“Lakini mimi niko kama nyinyi, kwa unyonge wa kila aina mwilini na akilini; walakini nimechaguliwa na watu hawa, na kutakaswa na baba yangu, na nikaruhusiwa kwa mkono wa Bwana kwamba niwe mtawala na mfalme wa watu hawa; na nimelindwa na kuhifadhiwa kwa uwezo wake usio na kipimo, ili niwatumikie kwa uwezo wote, na nguvu ambazo Bwana amenipatia” (Mosia 2:10–11).

Kiongozi wako katika Kanisa la Bwana anaweza kuonekana kwako wewe ni dhaifu na mwanadamu au anaweza kuonekana kuwa mwenye nguvu na mwenye maono. Ukweli ni kwamba kila kiongozi ni mchanganyiko wa sifa hizo na zaidi. Kitu kinachosaidia watumishi wa Bwana ambao wanaitwa kutuongoza ni wakati tunapoweza kuwaona kama Bwana alivyofanya wakati aliwaita.

Bwana huwaona watumishi Wake kikamilifu. Anaona uwezo wao na matokeo yao ya baadaye. Na Yeye anajua jinsi asili yao inaweza kubadilishwa. Pia anajua jinsi wanavyoweza kubadilishwa kwa uzoefu wao na watu watakaoongoza.

Huenda ukawa na uzoefu wa kuimarishwa na watu ulioitwa kuwatumikia. Nilishawahi mara moja kuitwa kama askofu wa vijana wazima waseja. Sijui kama madhumuni ya Bwana yalikuwa zaidi ya mabadiliko gani ningeweza kumsaidia Yeye kufanya ndani yao au mabadiliko aliyojua wangelifanya ndani yangu.

Kwa kiwango nisichoelewa, wengi wa wale vijana katika kata hiyo walichukulia kama niliitwa na Mungu hususani kwa ajili yao. Waliona udhaifu wangu lakini waliupuuzia.

Nakumbuka kijana mmoja ambaye aliomba ushauri juu ya uchaguzi wake wa elimu. Alikuwa mwanafunzi wa mwaka kwanza katika chuo kizuri. Wiki moja baada ya mimi kutoa ushauri huu alipanga ahadi nami.

Alipoingia katika ofisi, alinishangaza kwa kuniuliza, “Askofu, tunaweza kuomba kabla ya kuzungumza? Na tunaweza piga magoti? Na ninaweza sali?

Maombi yake yalinishangaza. Lakini sala yake ilinishangaza hata zaidi Ilikuwa hivi: “Baba wa Mbinguni, Unajua kwamba Askofu Eyring alinipa shauri wiki iliyopita, na haukufanya kazi. Tafadhali mfunulie kujua nini nifanye sasa.”

Sasa unaweza tabasamu kwa hilo, lakini sikutabasamu. Alijua tayari kile Bwana alichotaka afanye. Lakini aliheshimu ofisi ya askofu katika Kanisa la Bwana na labda alitaka mimi niwe na nafasi ya kupata ujasiri zaidi wa kupokea ufunuo katika wito huo.

Ilifanya kazi. Mara tu tulipoinuka na kukaa chini, ufunuo ulikuja kwangu. Nilimuambia kile nilihisi Bwana angetaka yeye afanye. Alikuwa na umri wa miaka 18 tu wakati ho, lakini alikuwa mzima katika miaka ya kiroho.

Alijua kwamba hakuwa na haja ya kwenda kwa Askofu kwa shida kama hiyo. Lakini alikuwa amejifunza kumkubali mtumishi wa Bwana hata katika udhaifu wake wa kidunia. Hatimaye alikuwa rais wa kigingi. Alijibebea somo ambalo tulijifunza pamoja: ikiwa una imani kwamba Bwana anaongoza Kanisa Lake kwa njia ya ufunuo kwa watumishi wale wasiokuwa wakamilifu anaowaita, Bwana atafungua madirisha ya mbinguni kwao, kama atakavyokutendea.

Kutokana na uzoefu huo, nilibeba somo kwamba imani ya watu tunaowatumikia, wakati mwingine ni zaidi kuliko imani yetu wenyewe, hutuletea ufunuo katika huduma ya Bwana.

Kulikuwa na somo lingine kwangu. Ikiwa mvulana huyo angenihukumu kwa kushindwa kwangu kumpa ushauri mzuri mara ya kwanza, kamwe asingerudi kuuliza tena. Na kwa hiyo, kwa kuchagua kutonihukumu, alipokea uthibitisho aliotaka.

Lakini somo jingine kutokana na uzoefu huo limenisaidia vizuri. Kwa kadiri ninavyojua, hakuwahi kumwambia mtu yeyote katika kata kwamba sikumpa ushauri mzuri wakati wa kwanza. Ikiwa angefanya hivyo, ingeweza kupunguza imani ya wengine katika kata kuamini ufunuo wa Askofu.

Mimi ujaribu nisiwahukumu watumishi wa Bwana au kusema juu ya udhaifu wao dhahiri. Na ninajaribu kufundisha hilo kwa mfano kwa watoto wangu. Rais James E. Faust alishiriki kanuni ya imani ambayo ninajaribu kuifanya yangu mwenyewe. Ninaipendekeza kwenu:

“Sisi … tunastahili kuwakubali na kuwasaidia viongozi wetu, kwa sababu wao … ‘wameitwa na kuchaguliwa.’ Kila muumini wa Kanisa hili anaweza kupokea ushauri kutoka kwa askofu au rais wa tawi, rais wa kigingi au misheni, na Rais wa Kanisa na washirika wake. Hakuna hata mmoja wa ndugu hawa aliomba wito wake. Hakuna aliyekamilika. Hata hivyo wao ni watumishi wa Bwana, walioitwa na Yeye kupitia wale walio na haki ya ufunuo. Wale walioitwa, kukubaliwa, na kutengwa wana haki ya kuungwa mkono nasi.

“ … Kutoheshimu viongozi wa kanisa kumesababisha wengi kuteseka na kuanguka kiroho. Tunapaswa kutotia maanani udhaiifu wowote, chunjua, au chunusi za wanaume walioitwa kutusimamia, na kuimarisha ofisi wanayoshikilia” (Kuitwa na Kuchaguliwa, “Liahona, Nov. 2005, 54–55).

Shauri hilo linabariki watumishi wa Mungu katika hali zote.

Katika siku za mwanzo za Kanisa la Bwana, viongozi waliokuwa karibu na Nabii Joseph Smith walianza kuzungumza juu ya mafungufu yake. Hata kwa wote waliyoyaona na kujua kuhusu msimamo wake na Bwana, roho yao ya upinzani na wivu vilitambaa kama tauni. Mmoja wa wale kumi na wawili alituwekea kiwango chote cha imani na uaminifu tunapaswa kuwa nao ikiwa tutatumika katika ufalme wa Bwana.

Hii ndio ripoti: “Wazee kadhaa waliitisha mkutano katika hekalu kwa wale wote waliomchukulia Joseph Smith kuwa Nabii aliyeanguka. Walikusudia kumchagua David Whitmer kama kiongozi mpya wa Kanisa. … Baada ya kusikiliza hoja juu ya kumpinga Nabii, Brigham [Young] aliinuka, na kushuhudia, ‘Joseph alikuwa Nabii na nilijua hivyo, na kwamba wangewezakumshutumu na kumkashifu ili mradi wajiridhishe; wao wasingeweza kuharibu uteuzi wa Nabii wa Mungu, wangeweza tu kuharibu mamlaka yao wenyewe, kukata uzi ambao unawaunga wao kwa Nabiina kwa Mungu, na kujizamisha wenyewe jehanamu’” (Church History in the Fulness of Times Student Manual [Church Educational System manual, 2003], 2nd ed., 174; see also Teachings of Presidents of the Church: Brigham Young [1997], 79).

Kuna uzi ambao unatuunganisha kwa Bwana katika huduma yetu. Unaanza kutoka popote tulipoitwa kutumikia katika ufalme, hadi kupitia wale walioitwa kutusimamia katika ukuhani, na kwa nabii, ambaye amefungwa kwa Bwana. Inachukua imani na unyenyekevu kutumikia mahali ambapo tunaitwa, kuamini kwamba Bwana alituita sisi na wale wanaotuongoza, na kuwasaidia kwa imani kamili.

Kutakuwa na nyakati, kama ilivyokuwa katika siku za Kirtland, wakati tutahitaji imani na uadilifu wa Brigham Young kusimama mahali ambapo Bwana ametuita, waaminifu kwa nabii Wake na viongozi aliowaweka mahali.

Ninawatolea ushahidi wangu wa dhati na bado wa furaha kwamba Bwana Yesu Kristo yupo katika usukani. Analiongoza Kanisa Lake na watumishi Wake. Natoa ushahidi kwamba Thomas S. Monson ndiye mtu pekee mwenye funguo zote za ukuhani hapa duniani na anayezitumia wakati huu. Na ninaomba baraka juu ya watumishi wote wanyenyekevu ambao hutumikia kwa hiari na vizuri katika Kanisa lililorejeshwa la Yesu Kristo, ambaye Yeye binafsi anaongoza. Nashuhudia kwamba Joseph Smith alimuona Mungu Baba na Yesu Kristo. Walizungumza nae. Funguo za ukuhani zilirejeshwa kuwabariki watoto wote wa Baba wa Mbinguni. Ni lengo letu na tumaini letu kutumikia mahali petu katika kazi ya Bwana Katika jina la Yesu Kristo, amina.