2010–2019
Kuidhinisha Maafisa wa Kanisa
Oktoba 2017


Kuidhinisha Maofisa wa Kanisa

Kina ndugu na kina dada, sasa nitawasilisha kwenu Viongozi Wenye Mamlaka, Sabini wa Eneo, na Urais Mkuu wa Makundi Saidizi wa Kanisa kwa kura yenu ya kuidhinisha.

Imependekezwa kwamba tumuidhinishe Thomas Spencer Monson kama nabii, mwonaji, na mfunuzi na Rais wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho; Henry Bennion Eyring kama Mshauri wa Kwanza katika Urais wa Kwanza; na Dieter Friedrich Uchtdorf kama Mshauri wa Pili wa Urais wa Kwanza

Wale wanaounga mkono, waoneshe.

Wale wanaopinga, kama kuna yeyote, anaweza kuonyesha ishara.

Inapendekezwa kwamba tumuidhinishe Russell Marion Nelson kama Rais wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili na wafuatao kama washiriki wa Akidi hiyo: Russell M. Nelson, Dallin H. Oaks, M. Russell Ballard, Robert D. Hales, Jeffrey R. Holland, David A. Bednar, Quentin L. Cook, D. Todd Christofferson, Neil L. Andersen, Ronald A. Rasband, Gary E. Stevenson, na Dale G. Renlund.

Wale wanaounga Mkono, tafadhaliwaoneshe.

Yeyote anayepinga anaweza kuonesha.

Imependekezwa kwamba tuwaidhinishe washauri katika Urais wa Kwanza na Mitume Kumi na Wawili kama manabii, waonaji, na wafunuaji.

Wote wanaounga mkono, tafadhali waoneshe.

Kinyume, kama kuna yeyote, kwa ishara hiyo hiyo.

Wazee Donald L. Hallstrom na Richard J. Maynes wamepumzishwa kutoka kwa hudumakama washiriki wa Urais wa Sabini.

Wote wanaotaka kuonyesha shukrani kwa ndugu hawa kwa huduma waliyofanya wanaweza kufanya hivyo kwa mkono ulioinuliwa.

Imependekezwa kwamba tuwaidhinishe Wazee Juan A. Uceda na Patrick Kearon, ambao wameitwa kuhudumu kama washiriki wa Urais wa Sabini.

Wale wanaotaka kuidhinisha Ndugu hawa katika kazi yao mpya, tafadhali dhihirisheni.

Yeyote anayepinga kwa ishara hiyo hiyo.

Inapendekezwa kwamba tuwapumzishe kwa shukrani kwa huduma yao nzuri Wazee Stanley G. Ellis, Larry R. Lawrence, na W. Craig Zwick Kama Viongozi Wakuu Wenye Mamlaka na kuwapa wadhifa huo wakiwa wamestaafu.

Wale ambao wangependa kuungana nasi katika kutoa shukrani kwa Ndugu hawa kwa huduma yao ya ajabu, tafadhali dhihirisheni.

Inapendekezwa kwamba tuwapumzishe wafuatao kama Sabini wa Eneo:Pedro U. Adduru, Detlef H. Adler, Angel H. Alarcon, Winsor Balderrama,Robert M. Call, Christopher Charles, Gene R. Chidester, Ralph L. Dewsnup, Ángel A. Duarte, Peter F. Evans, Francisco D. N. Granja, Yuriy A. Gushchin, Clifford T. Herbertson, Aniefiok Udo Inyon, Luiz M. Leal, Alejandro Lopez, L. Jean Claude Mabaya, Declan O. Madu, Alexander T. Mestre, Jared R. Ocampo, Andrew M. O’Riordan, Jesús A. Ortiz, Abenir V. Pajaro, Siu Hong Pon, Robert C. Rhien, Jorge Luis Romeu, Jorge L. Saldívar, Ciro Schmeil, Alin Spannaus, Moroni B. Torgan, Steven L. Toronto, Ricardo Valladares.

Wale wanaopendelea kuungana nasi kutoa shukrani kwa huduma yao bora, tafadhali dhihirisheni.

Inapendekezwa kwamba tumuidhinishe Torben Engbjerg kuhudumu kama Sabini wa Eneo.

Wote wanaopendelea, tafadhali dhihirisheni.

Wale wanaopinga, ikiwa kuna yeyote.

Imependekezwa kwamba tuwaidhinishe wale Viongozi Wakuu wengine, Sabini wa Eneo, na urais mkuu wa vikundi saidizi kama ilivyo sasa.

Wote wanaopendelea, tafadhali dhihirisheni.

Kinyume, kama kuna yeyote, kwa ishara hiyo hiyo.

Wale waliopinga mapendekezo yoyote yale wanapaswa kuwasiliana na rais wao wa kigingi.

Kina ndugu na kina dada, tunashukuru kwa imani na sala zenu za dhati kwa niaba ya viongozi wa Kanisa.