2010–2019
Sauti ya Bwana
Oktoba 2017


Sauti ya Bwana

Ninashuhudia kwamba kwenye mkutano mkuu huu, tumesikia sauti Ya Bwana. Mtihani kwa kila mmoja wetu ni jinsi gani tunaitikia.

Kwanza, neno la ukarimu kwa watoto wadogo. Ndio, hiki ni kikao cha mwisho, na ndio, mimi ndiye msemaji wa mwisho.

Hivi majuzi,nikiwa katika ziara katika Hekalu la Provo City Centre, nilivutiwa na mchoro wenye kichwa“First Vision from Afar.” Mchoro unaonyesha mwanga na nguvu kutoka mbinguni wakati Baba na Mwana walipomtembelea kijana mdogo Joseph Smith.

Picha
First Vision from Afar

Bila kuulinganisha na tukio takatifu lililoleta Urejesho, ninaweza kufikiria ono sawa na hilo ambalo lingeweza kuakisi mwanga na nguvu za kiroho za Mungu zikishuka katika mkutano mkuu huu na, matokeo yake, nguvu na nuru hiyo ieneayo duniani kote.

Picha
Nuru na nguvu za kiroho zikishuka kwenye mkutano mkuu huu
Picha
Nguvu na nuru hiyo ieneayo duniani kote

Nawatoleeni ushahidi wangu kwamba Yesu ndiye Kristo, kwamba anaongoza shughuli za kazi hii takatifu, na kwamba mkutano mkuu ni mojawapo ya nyakati muhimu sana ambapo anatoa maelekezo kwa Kanisa Lake na kwetu binafsi.

Kufundishwa Kutoka Juu

Siku kanisa lilipoanzishwa, Bwana alimteua Joseph Smith nabii, mwonaji na mtume wa Bwana Yesu Kristo1 na akaliambia kanisa:

“Kwani neno lake mtalipokea, kama vile linatoka kinywani mwangu, katika uvumilivu wote na imani yote.

“Kwani kwa kufanya mambo haya milango ya jahanamu haitawashinda; na Bwana Mungu atazitawanya nguvu za giza kutoka mbele zenu, naye atasababisha mbingu zitetemeke kwa ajili yenu.2

Baadaye, washiriki wote wa Urais wa Kwanza na Akidi ya Mitume Kumi na Wawili walikubaliwa na kutawazwa kama manabii, waonaji na wafunuzi.3

Sasa tunapokutana chini ya uongozi wa Rais Thomas S. Monson, tunatarajia kusikia, “mapenzi ya Bwana, … mawazo ya Bwana, … sauti ya Bwana, na nguvu za Bwana katika kukomboa.”4 Tunaamini katika ahadi yake: “Iwe kwa sauti yangu mwenyewe au kwa sauti ya watumishi wangu, yote ni sawa.”5

Katika vurugu na mkanganyiko katika dunia yetu ya leo, kutumaini na kuamini katika maneno ya Urais wa Kwanza na Akidi ya Mitume Kumi na Wawili ni muhimu katika ukuaji na uvumilivu wa kiroho.6

Tumekuja pamoja kwa mkutano huu wa ajabu. Mamilioni ya Watakatifu wa Siku za Mwisho katika zaidi ya nchi 200, wakizungumza zaidi ya lugha 93, wanahudhuria vikao hivi au kusoma jumbe za mkutano mkuu.

Tunakuja tukiwa tumesali na kujiandaa. Kwa wengi wetu, kumekuwa na hofu nzito na maswali ya dhati. Sisi tunataka kufanya upya imani yetu katika Mwokozi, Yesu Kristo, na kuimarisha uwezo wetu wa kuzuia majaribu na kuepuka fadhaa. Tunakuja kufunzwa kutoka Juu.

Nia na Mapenzi ya Bwana

Kwa Urais wa Kwanza na Mitume Kumi na Wawili, ambao kwa kawaida hunena katika kila mkutano, jukumu kubwa la kuandaa jumbe zao ni wajibu na imani takatifu.

Miaka iliyopita kabla ya kutumikia kama Kiongozi Mwenye Mamlaka, Nilimuuliza Mzee Dallin H. Oaks kama aliandaa ujumbe tofauti kwa kila mkutano wa kigingi. Alijibu kuwa hafanyi hivyo lakini aliongeza, “Lakini jumbe zangu za mkutano mkuu ni tofauti. Ninaweza kupitia miswada 12 hadi 15 ili kuwa na hakika kuwa ninasema kile Bwana angetaka niseme.”7

Ni lini na vipi mwongozo wa ujumbe wa mkutano mkuu huja?

Bila mada zilizopangwa, tunaona mbingu kimaridadi zikiratibu maudhui na mawazo ya kweli za milele katika kila mkutano mkuu.

Mmoja ya ndugu zangu aliniambia kuwa somo lake la mkutano huu lilitolewa kwake mara baada ya ujumbe wake wa Aprili iliyopita. Mwingine alisema wiki tatu zilizopita kwamba bado alikuwa akisali na kusubiri kutoka kwa Bwana. Mwingine alipoulizwa ni kwa muda gani imechukua kuandaa ujumbe mahususi hasa, alijibu, “Miaka ishirini na tano.”

Wakati mwingine wazo kiini linaweza kuja haraka, lakini maudhui na maelezo bado huhitaji ukwezi mkubwa sana wa kiroho. Kufunga na kusali, kusoma na imani kila mara ndiyo sehemu ya mchakato. Bwana hataki kujisingizia kufifize sauti Yake kwa Watakatifu Wake.

Mwongozo wa ujumbe wa mkutano mkuu mara nyingi huja usiku au mapema saa za asubuhi, wakati hotuba liko mbali na mawazo ya akili. Ghafla, umaizi usiotarajiwa na, wakati mwingine, maneno maalum na sehemu za maneno huja kama ufunuo halisi.8

Unaposikiliza, jumbe unazopokea zinaweza kuwa halisi au zinaweza kuwa maalum kwa ajili yako.

Nikinena miaka mingi iliyopita katika mkutano mkuu, nilizungumza kuhusu sehemu ya maneno ambayo iliingia akilini mwangu nikiwa ninajiuliza kama nilikuwa tayari kuhudumu misheni. Kirai kilikuwa “Hujui kila kitu, lakini unajua vya kutosha!”9 Msichana aliyekuwa kwenye mkutano mkuu siku hiyo aliniambia kuwa alikuwa akiomba kuhusu ombi la ndoa, akijiuliza ni kiasi gani alimjua yule kijana. Niliponena maneno “Hujui kila kitu, lakini unajua vya kutosha,” Roho alimdhihirishia kwamba alimjua vizuri ya kutosha. Wameoana kwa furaha kwa miaka mingi.

Nakuahidi kwamba unapoiandaa roho yako, na kuja kwa matarajio kuwa utasikia sauti ya Bwana, mawazo na hisia zitakuja katika mawazo yako ambazo zimeandaliwa mahususi kwa ajili yako. Tayari umeshahisi katika mkutano huu, au utahisi unaposoma jumbe ndani ya wiki zijazo.

Kwa Sasa na Miezi Ijayo

Rais Monson amesema:

“Chukua muda kusoma jumbe za mkutano mkuu.”10

“Zifakari [hizo] Nimepata … kuwa ninapata hata zaidi kutoka kwenye hotuba hizi zenye mwogoz pale ninapozisoma kwa kina zaidi.”11

Mafundisho ya mkutano mkuu ni fikira ambazo Bwana angekuwa nazo kwa ajili yetu kwa wakati huu katika miezi ijayo.

Mchungaji “huenda mbele ya [kondoo zake], na kondoo humfuata: kwa kuwa wanajua sauti yake.”12

Mara nyingi sauti Yake hutuongoza kubadili kitu katika maisha yetu. Anatualika kutubu. Anatualika kumfuata Yeye.

Fikiria kuhusu kauli hizi kutoka kwenye mkutano mkuu huu.

Rais Henry B. Eyring asubuhi hii: “Ninawatolea ushahidi wangu kwamba Mungu Baba yu hai na anataka wewe uje nyumbani Kwake. Hili ndilo Kanisa la Yesu Kristo la kweli. Anakujua, Anakupenda, na Anakuangalia.13

Rais Dieter F. Uchtdorf jana: “Mimi nashuhudia kwamba tunapoanza au tunpoendelea na safari hii ya ajabu ambayo inaongoza hadi kwa Mungu, maisha yetu yatakuwa mazuri … na Bwana atatutumia sisi kwa njia za ajabu kuwabariki wale wanaotuzunguka na kuleta malengo ya milele.14

Rais Russell M. Nelson jana mchana: “Ninaahidi kwamba unapojizamisha kila siku ndani ya Kitabu cha Mormoni unaweza kukingwa dhidi ya maovu ya siku, hata janga la kunasa sana la ponografia na uraibu mwingine wa kutia akili ganzi.”15

Mzee Dallin H. Oaks jana: “Ninashuhudia kwamba tangazo juu ya familia ni kauli ya ukweli wa milele, mapenzi ya Bwana kwa watoto wake.”16

Mzee M. Russell Ballard: “Tunapaswa kuwakumbatia watoto wa Mungu kwa huruma na kuondoa chuki yoyote ikiwemo tofauti ya rangi, jinsia, na utaifa.17

Kwa sababu tuna dakika moja zaidi, ningependa kuongezea mawazo mchache kumhusu Mzee Robert D. Hales. Urais wa Kwanza ulikuwa umemwambia Mzee Hales kwamba angetoa ujumbe mfupi katika kikao cha Jumapili asubuhi kama afya yake ingemruhusu. Hali afya yake haikumruhusu, yeye aliandaa ujumbe, ambao alikamilisha wiki iliyopita na kuushiriki nami. Kutokana na kufariki kwake takriban saa tatu zilizopita, nitashiriki nanyi msitari mitatu kutoka kwenye hotuba yake.

Nikmnukuu Mzee Hales: “Tunapochagua kuwa imani, tunajiandaa kusimama mbele za Mungu. … Baada ya Usulubisho wa Mwokozi, Yeye aliwatokea tu ‘wale ambao wamekuwa waaminifu katika ushuhuda juu [Yake] wakati walipoishi katika mwili wenye kufa.’ [M&M 138:12]. Wale ‘ambao walikataa shuhuda … za … manabii wa kale [hawakuweza] kuona uwepo [wa Mwokozi], wala kuutazama uso wake.’ [M&M 138:21.] … Imani yetu hutuandaa kuwa katika uwepo wa Bwana.”

Bwana ni mkarimu jinsi gani kumpatia msukumo Rais Russell M. Nelson mwishoni mwa kikao cha asubuhi hii kuondoka haraka kutoka katika jengo hili, kukosa mlo wake wa mchana, na kuharakisha kwenda kitandani kwa Mzee Hales, ambapo angewasili na kuwepo, pamoja na malaika Mary Hales wakati Mzee Hales alipohitimu kuondoka dunia hii.

Kuitikia Sauti ya Bwana

Ninashuhudia kwamba kwenye mkutano huu, tumesikia sauti Ya Bwana.

Hatupaswi kuwa na hofu wakati maneno ya watumishi wa Bwana yanaenda kinyume na fikra za ulimwengu, na, mara nyingine, fikra zetu. Daima imekuwa hivi. Nimepiga magoti hekaluni pamoja na Ndugu zangu. Ninashuhudia wema wa nafsi yao. Matamanio yao makuu ni kumpendeza Bwana na kuwasaidia watoto wa Mungu kurejea katika uwepo Wake.

Wale wa sabini; Uaskofu; Urais Mkuu wa Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama, Wasichana, Msingi; na viongozi wa vikundi saidizi vingine wameongeza mwongozo mkubwa kwenye mkutano huu, kama ilivyo kwa muziki mzuri na sala za dhati.

Kunalo sanduku tunu la maelekezo ya mbinguni yanayosubiri uvumbuzi wako katika jumbe za mkutano mkuu. Mtihani kwa kila mmoja wetu ni jinsi gani tunaitikia kwa kile tunachosikia, kile tunasoma, na kile tunahisi.

Hebu nishiriki tukio hili kuhusu kuitikia maneno ya kinabii kutoka kwa maisha ya Rais Russell M. Nelson

Mnamo mwaka wa 1979, miaka mitano kabla ya mwito wake kama Kiongozi Mkuu Mwenye mamlaka, kaka Nelson alihudhuria mkutano kabla ya mkutano mkuu. “Rais Spencer W. Kimball aliwapa changamoto wote waliokuwepo kuongeza hatua dhabiti katika kupeleka injili duniani kote. Mojawapo ya nchi ambazo hususan Rais Kimball alliitaja ilikuwa ni China, akisema ‘Tunapaswa kuwa wa hudumu kwa Wachina. Tunapaswa kujifunzalugha yao. Tunapaswa kuwaombea na kuwasaidia.’”18

Picha
Rais Russell M. Nelson akiwa daktari mpasuaji

Katika umri miaka wa 54, Ndugu Nelson alikuwa na hisia wakati wa mkutano kwamba anapaswa kusoma lugha ya Mandarini. Ingawa alikuwa daktari mpasuaji wa moyo mwenye shughuli nyingi, kwa haraka alipata huduma za mkufunzi

Si muda mrefu baada ya kuanza masomo yake, Dkt. Nelson akihudhuria mkutano na bila ya kutazamiwa alijikuta akikaa karibu na “daktari mpasuaji mchina wa hadhi ya juu, Dkt. Wu Yingkai. … Kwa sababu [Ndugu Nelson] alikuwa akisoma Mandarin, alianza [] maongezi [na Dkt. Wu].”19

Picha
Dkt. Russell M. Nelson na Dkt Wu Yingkai

Nia ya Dkt. Nelson kumfuata nabii ilipelekea Dkt. Wu kutembelea Jiji la Salt Lake na Dkt. Nelson kusafiri kwenda China kutoa mhadhara na kufanya operesheni za upasuaji.

Upendo wake kwa watu wa China na upendo na heshima kwake, uliongezeka.

Februari 1985, miezi kumi baada ya kuitwa kwenye Akidi ya Mitume Kumi na Wawili, Mzee Nelson alipokea simu ya kushangaza kutoka China ikimuomba Dkt Nelson kuja Beijing kufanya operesheni ya moyo wa muimbaji maarufu wa opera wa China. Kwa kutiwa moyo na Rais Hinckley, Mzee Nelson alirudi China. Operesheni ya upasuaji ya mwisho aliyowahi kufanya ilikuwa ni katika Jamhuri ya Watu wa China.

Picha
Rais Russell M. Nelson akituzwa

Miaka miwili iliyopita, Oktoba 2015, Rais Russell M. Nelson kwa mara ingine tena alipatiwa heshima kwa tamko rasmi, akiitwa “rafiki wa zamani wa China.”

Basi jana tulimsikia kwa sasa mwenye umri wa miaka 93 Rais Russell M. Nelson akiongea kuhusu ombi la Rais Thomas S. Monson kwa “kila mmoja wetu [katika mkutano wa Aprili iliyopita] kwa maombi kusoma na kutafakari Kitabu cha Mormoni kila siku.”

Kama alivyofanya kama mpasuaji wa moyo mwenye shughuli nyingi, wakati alipomwajiri mkufunzi wa Mandarin, Rais Nelson mara moja alichukuwa ushauri wa Rais Monson na akaufanyia kazi katika maisha yake mwenyewe. Zaidi ya kusoma tu, alisema kwamba “alitengeneza orodha ya Kitabu cha Mormoni ni nini, nini kithibitisha, nini kinakanusha, nini kinatimiza, nini kinafafanua, na nini kinafunua.20

Na basi, cha kupendeza asubuhi ya leo, kama shahidi wa pili, Rais Henry B. Eyring pia alizungumza kuhusu mjibizo wake kwa onyo la Rais Monson. Je, Unakumbuka maneno haya? “Kama wengi wenu, nilisikia maneno ya nabii kama sauti ya Bwana kwangu. Na, pia kama wengi wenu, niliamua kutii maneno hayo.21

Na tuone hii kama mifano katika maisha yetu wenyewe.

Ahadi na Baraka

Naahidi kwamba unapoisikiliza sauti ya Bwana kwako kwenye mafundisho ya mkutano huu, na kutenda kulingana na msukumo huo, utahisi mkono wa mbinguni juu yako, na maisha yako na ya wale wanaokuzunguka yatabarikiwa.22

Wakati wa mkutano huu, tumefikiria kumhusu nabii wetu mpendwa. Tunakupenda, Rais Monson. Ninahitimisha kwa maneno yake kutoka kwenye mimbari hii. Naamini ni baraka kwamba yeye angetaka kumpa kila mmoja wetu leo, kama angeweza kuwa pamoja nasi. Alisema: “Tunapoondoka kutoka kwa mkutano huu, nawaombeeni baraka za mbinguni juu kila mmoja wenu. Ninaomba Baba yetu wa Mbinguni awabariki ninyi na familia zenu. Acha jumbe na roho wa mkutano huu apate kudhihirika katika yote mtendayo—nyumbani kwenu, kazini kwenu, mikutanoni mwenu na katika kuja na kuondoka kwenu kote.”

Alimalizia: “Nawapenda. Ninawaombeeni. Mungu awabariki. Na ahadi zake za amani zikawe nanyi sasa na mara zote.”23

Katika jina la Yesu Kristo, amina.

Muhtasari

  1. Ona Mafundisho na Maagano 21:1.

  2. Mafundisho na Maagano 21:5-6.

  3. Joseph Smith alirekodi kuwa yafuatayo yalitokea wakati wa kuweka wakfu Hekalu la Kirtland mnamo Machi 27, 1836:

    “Nilitoa hotuba fupi, na kuita akidi kadhaa, na mkusanyiko ya Watakatifu, kuwatambua Urais wa [Kwanza] kama Manabii na Waonaji na kuwakumbuka katika sala zao. Wote waliingia agano kufanya hivyo, kwa kuinuka.

    “Na ndipo nikaita akidi na kusanyiko la Watakatifu kuwatambua Mitume Kumi na Wawili waliokuwepo kama Manabii, Waonaji na Wafunuzi na mashahidi wa kipekee kwa mataifa yote ya dunia, wakiwa na funguo za ufalme, kufungua na kusababisha kuwa, kati yao, na kutoa ushirikiano kupitia sala zao, ambapo walikubaliana na hili kwa kusimama” ( Mafundisho ya Manabii wa Kanisa : Joseph smith[2007], 199).

  4. Mafundisho na Maagano 68:4.

  5. Mafundisho na Maagano 1:38

  6. Rais Henry B. Eyring aliwahi kusema:

    “Uchaguzi wa kutotaka kuchukua ushauri wa kinabii hubadili mahali tuliposimamia. Inakuwa ni hatari sana. Kushindwa kuchukua ushauri wa kinabii hupunguza nguvu zetu za kuchukua ushauri wenye mwongozo baadae. Muda muafaka wa kuchagua kumsaidia Nuhu kujenga safina ulikuwa ni mara ya kwanza alipouliza. Kila muda alipouliza baada ya hapo, kila kushindwa kuitikia kungeweza kupunguza umakini katika Roho. Na ndio kila muda ombi lake lingeoneka la kipumbavu zaidi, mpaka mvua ilipokuja. Na ilikuwa wameshachelewa.

    “Kila muda katika maisha yangu ambapo nimechagua kuchelewa kufuata ushauri wenye mwongozo au kuamua kwamba nilikuwa sihusiki, nilikuja kujua kuwamba nilijiweka katika njia ya kudhuru. Kila muda nilipousikiliza ushauri wa manabii, kuhisi ukithibitishwa katika sala, na halafu kuufuata, niligundua kuwa nilisogelea usalama” (“Finding Safety in Counsel,” Ensign, May 1997, 25).

  7. Ona Neil L. Andersen, “Teaching Our Children to Love the Prophets,” Ensign, Apr. 1996, 47.

  8. Boyd K. Packer aliwahi kusema:

    “Nimeshamsikia Rais Harold B. Lee akianza kauli nyingi kuhusu masuala yanayohusiiana na ufunuo na usemi kwa hivi: ‘Katika saa za asubuhi mapema, nilipokuwa nikitafakari kuhusa suala hili …’ Alifanya hii kuwa desturi ya kufanya kazi katika saa mbichi, makini za mapema asubuhi juu ya shida zilizohitaji ufunuo.

    “Bwana alijua kitu fulani wakati Alipoelekeza katika Mafundisho na Maagano, ‘Acheni kulala kupita inavyotakiwa; laleni vitandani mwenu mapema, ili msichoke; amkeni mapema, ili miili yenu na akili zenu zipate kutiwa nguvu. (M&M 88:124.) …

    “Nimejifunza nguvu za msemo, ‘Lala mapema, amka mapema.’ Ninapokuwa na shinikizo, hautanipata nikichoma tambi usiku wa manane. Itakuwa bora kulala mapema na kuamka saa za asubuhi mapema wakati ambapo niweza kuwa karibu Naye ambaye huongza kazi hii” (Teach Ye Diligently [2005], 244-45).

  9. Neil L. Andersen, “Unajua vya kutosha,” Liahona, Nov. 2008.

  10. Thomas S. Monson, “Mpaka tukutane tena,” Liahona, May 2014.

  11. Thomas S. Monson, “Mungu awe Nanyi Daima Mpaka Tukutane Tena,” Liahona, Nov. 2012.

  12. Yohana 10:4.

  13. Henry B. Eyring, “Fear Not to Do Good,” Liahona, Nov. 2017, 103.

  14. Dieter F. Uchtdorf, “A Yearning for Home,” Liahona, Nov. 2017, 22, 24.

  15. Russell M. Nelson, “Kitabu cha Mormoni: Maisha Yako Yangekuaje Bila Hicho?Liahona, Nov. 2017, 63.

  16. Dallin H. Oaks, “The Plan and the Proclamation,” Liahona, Nov. 2017, 30.

  17. M. Russell Ballard, “Safai Inaendelea!Liahona, Nov. 2017, 106.

  18. Spencer J. Condie, Russell M. Nelson: Father, Surgeon, Apostle (2003), 215.

  19. Spencer J. Condie, Russell M. Nelson, 215.

  20. Russell M. Nelson, “Kitabu cha Mormoni: Maisha Yako Yangekuaje Bila Kitabu Hicho?”

  21. HenryB. Eyring, “Usiogope Kutenda Mema

  22. Gordon B. Hinckley aliwahi kusema:

    “Mtihani huja katika matumizi ya mafundisho yaliyotolewa. Ikiwa, baadaye, tunakuwa wakarimuzaidi, ikiwa tunakuwa jirani wema, ikiwa tunasogea karibu na Mwokozi, kwa azimio thabiti za kufuata mafundisho Yake na mfano Wake, basi mkutano mkuu huu umefanikiwa ajabu. Ikiwa, kwa upande mwingine, hamna maboresho katika maish yetu, basi wale ambao wazungumza washindwa kwa kiasi kikubwa.

    “Mabadiliko hayo yanaweza yasiweze kukisiwa katika siku moja, au wiki, au hata mwezi. Maazimio yanayofanywa kwa haraka na usahalika kwa haraka. Lakini katika mwaka mmoja kutoka sasa, ikiwa tunafanya vyema kuliko ilivyokuwa awali, basi juhudi za siku hizi haizkuwa bure” (“An Humble and a Contrite Heart,” Ensign, Nov. 2000, 88).

  23. Thomas S. Monson, “Maneno wakati wa kufunga,” Liahona, May 2010, 113.