2015
Acha Ushuhuda Wako Ung’ae
Februari 2015


Watoto

Acha Ushuhuda Wako Ung’ae

Kupokea ushuhuda ni kama kuwasha moto. Kama tu vile lazima tuongeze kuni ili moto uendelee kuwaka, lazima tuombe, tutubu, tuhudumie wengine, tusome maandiko, na tutii amri ili kusaidia kung’arisha shuhuda zetu.

Ili kujifunza zaidi kuhusu jinsi ya kujenga ushuhuda wetu, soma kila mmoja ya maandiko yaliyoorodheshwa hapa chini. Chora moto na miale mitano mikubwa. Weka rangi katika kila mwale kwa ajili ya kila andiko usomalo. Maandiko zaidi unayosoma, ndipo moto unang’aa zaidi — na ushuhuda wako!