2015
Sifa za Yesu Kristo: Bila Dhambi
Februari 2015


Ujumbe wa Mwalimu MTEMBELEAJI, Februari 2015

Sifa za Yesu Kristo: Bila Dhambi

Kwa maombi jifunze maneno haya na utafute kujua kitu cha kushiriki. Kuelewa maisha na wajibu wa Mwokozi kunawezaje kuongeza imani yako Kwake na kuwabariki wale unaowaongoza kupitia ualimu wa utembeleaji? Kwa taarifa zaidi, nenda reliefsociety.lds.org.

Picha
Nembo ya Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama

Imani, Familia, Usaidizi

Mwokozi wetu, Yesu Kristo, alikuwa ndiye pekee aliyeweza kufanya upatanisho kwa ajili ya wanadamu. “Yesu Kristo, Mwanakondoo bila dosari, alijitolea Mwenyewe kwenye meza ya kutolea dhabihu na kulipa gharama ya dhambi zetu,” alisema Rais Dieter F. Uchtdorf, Mshauri wa Pili katika Urais wa Kwanza.1 Kuelewa kwamba Yesu Kristo alikuwa hana dhambi kunaweza kutusaidia kuongeza imani yetu Kwake na kutia bidii kutii amri Zake, kutubu, na kuwa wasafi.

“Yesu alikuwa kiumbe cha mwili na roho, lakini hakukubali majaribio (ona Mosia 15:5),” alisema Mzee D. Todd Christofferson wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili. “Tunaweza kumgeukia kwa sababu anaelewa. Anaelewa masumbuko, na pia anaelewa jinsi ya kushinda masumbuko

“Nguvu ya Upatanisho Wake inaweza kufuta madhara ya dhambi ndani yetu. Tunapotubu, neema ya Upatanisho Wake inatuokoa na kutusafisha (ona 3 Nefi 27:16–20). Ni kana kwamba hatukuwa tumeanguka, kama hatukuwa tumekubali majaribu.

“Tunapojitahidi siku baada ya siku na wiki baada ya wiki kufuata njia ya Kristo, roho yetu hudhibitisha ufahari wake, vita ndani yetu inapungua, na majaribu yanakoma kutusumbua.”2

Maandiko ya Ziada

Mathayo 5:48; Yohana 8:7; Waebrania 4:15; 2 Nefi 2:5–6

Kutoka kwa Maandiko

Mwokozi alilipa gharama ya dhambi zetu kupitia Uana Wake mtukufu, Maisha Yake yasiyo na dhambi, mateso Yake na kumwaga damu Yake katika Bustani la Gethsemane, kifo Chake msalabani na Ufufuo Wake kutoka kaburini. Kupitia Upatanisho wa Yesu Kristo, tunaweza kuwa wasafi tena tunapotubu dhambi zetu.

Mfalme Benyamini alifundisha watu wake kuhusu Upatanisho wa Yesu Kristo na kisha aliuliza kama waliamini maneno yake. “Wote wakalia kwa sauti moja, wakisema: … Roho ameleta mabadiliko makuu ndani yetu, au mioyoni yetu, hata kwamba hatuna tamaa ya kutenda maovu tena, lakini kutenda mema daima. …

“Na tunataka tuagane na Mungu wetu ili tutende nia yake, na tuwe watiifu kwa amri zake kwa vitu vyote” (Mosiah 5:1–2, 5).

Sisi pia tunaweza kuwa na “mabadiliko makuu” kama watu wa Mfalme Benyamini, ambao “hawakuwa na tamaa ya kutenda maovu tena, lakini kutenda mema daima” (Mosia 5:2).

Muhtasari

  1. Dieter F. Uchtdorf, “You Can Do It Now!” Liahona,Nov. 2013, 56.

  2. D. Todd Christofferson, “That They May Be One in Us,” Liahona, Nov. 2002, 71.

Zingatia Hili

Je, kuwa msafi kunatofautiana vipi na kuwa mkamilifu?