Maandiko Matakatifu
Mafundisho na Maagano 43


Sehemu ya 43

Ufunuo uliotolewa kupitia Joseph Smith Nabii, huko Kirtland, Ohio, Februari 1831. Kwa wakati huu baadhi ya waumini wa Kanisa walikuwa wakisumbuliwa na watu waliokuwa wakijifanya wao kuwa ni wafunuzi. Nabii alimwomba Bwana na kupokea mawasiliano haya yaliyoelekezwa kwa wazee wa Kanisa. Sehemu ya kwanza hushughulika na masuala ya utawala wa Kanisa; sehemu ya mwisho ina maonyo ambayo wazee lazima wayatoe kwa mataifa ya ulimwengu.

1–7, Mafunuo na amri huja tu kupitia mteule mmoja; 8–14, Watakatifu wanatakaswa kwa kutenda katika utakatifu wote mbele za Bwana; 15–22, Wazee wanatumwa kuhubiri toba na kuwatayarisha watu kwa ajili ya siku kuu ya Bwana; 23–28, Bwana huwaita watu kwa sauti Yake mwenyewe na kwa nguvu za asili; 29–35, Milenia na kufungwa kwa Shetani vitakuja.

1 Ee sikilizeni, ninyi wazee wa kanisa langu, na mtege sikio kwa maneno ambayo nitayasema kwenu.

2 Kwani tazama, amini, amini ninawaambia, kwamba mmeipokea amri kama sheria kwa kanisa langu, kupitia yule ambaye nimemteua kwenu kupokea amri na mafunuo kutoka mikononi mwangu.

3 Kwa hakika jueni—kwamba hakuna mwingine yeyote aliyeteuliwa kwenu kupokea amri na mafunuo hadi atakapochukuliwa, kama atakaa ndani yangu.

4 Lakini amini, amini, ninawaambia, kwamba hakuna mwingine yeyote atakayeteuliwa kupokea kipawa hiki isipokuwa iwe kupitia kwake; kwani kama kitachukuliwa kutoka kwake hatakuwa na uwezo isipokuwa kumteua mwingine mahali pake.

5 Na hii itakuwa sheria kwenu, kwamba msipokee mafundisho ya yeyote yatakayokuja mbele yenu kama mafunuo au amri;

6 Na hii ninaitoa kwenu ili msiweze kudanganyika, kwamba muweze kujua kwamba siyo wangu.

7 Kwani amini ninawaambia kwamba yule ambaye ametawazwa na Mimi ataingia mlangoni na atatawazwa kama nilivyowaambia hapo awali, kufundisha mafunuo yale ambayo mmeyapokea na mtakayopokea kupitia kwake yeye niliyemteua.

8 Na sasa, tazama, ninawapa ninyi amri, kwamba wakati mkikusanyika pamoja mtaelekezana na kuinuana ninyi kwa ninyi, ili muweze kujua namna ya kutenda na kulielekeza kanisa langu, namna ya kutenda juu ya mafundisho ya sheria na amri zangu, ambazo nimewapa.

9 Na hivyo ndivyo mtafundishwa katika sheria ya kanisa langu, na mtakaswe kwa kile mlichokipokea, nanyi mtajifunga wenyewe kutenda katika utakatifu wote mbele zangu—

10 Kwamba kadiri mtakavyofanya haya, utukufu utaongezwa kwenye ufalme ambao mmepokea. Kadiri msivyo yafanya haya, kitachukuliwa, hata ambacho mmekipokea.

11 Safisheni uovu ulioko miongoni mwenu; jitakaseni wenyewe mbele yangu;

12 Na kama mnataka utukufu wa ufalme, mkubalini mtumishi wangu Joseph Smith, Mdogo, na muungeni mkono yeye mbele yangu kwa sala ya imani.

13 Na tena, ninawaambia, kwamba kama mnataka siri za ufalme, mpatieni chakula na mavazi, na vitu vyote ahitajivyo kukamilisha kazi ambayo nimemwamuru;

14 Na kama hamtayafanya atabakia kwao waliompokea, ili niweze kuhifadhia watu walio safi mbele zangu.

15 Tena ninasema, sikilizeni ninyi wazee wa kanisa langu, ambao nimewateua: Hamjatumwa kufundishwa, bali kufundisha wanadamu mambo ambayo nimeyaweka mikononi mwenu kwa uwezo wa Roho wangu;

16 Na mtafundishwa kutoka juu. Jitakaseni na mtajaliwa uwezo, ili muweze kutoa kama nilivyonena.

17 Sikilizeni ninyi, kwani, tazama, siku ile kuu ya Bwana imekaribia.

18 Kwani siku yaja ambayo Bwana atatoa sauti yake toka mbinguni; mbingu zitatikisika na nchi itatetemeka, na parapanda ya Mungu italia kwa sauti yenye kuendelea na kwa sauti, na atasema kwa mataifa yaliyolala: ninyi watakatifu amkeni na muishi; ninyi wenye dhambi bakini na mlale hadi nitakapoita tena.

19 Kwa hiyo fungeni viuno vyenu msije kukutwa miongoni mwa waovu.

20 Piga kelele na usiache. Yaiteni mataifa kutubu, wazee kwa vijana, wafungwa na walio huru, mkisema: Jitayarisheni wenyewe kwa siku ile kuu ya Bwana;

21 Kwani kama Mimi, niliye mwanadamu, napiga kelele na kuwaita ninyi kutubu, na mnanichukia, mtasema nini wakati siku ile itakapokuja wakati ngurumo ya radi itakapotoa ngurumo kutoka miisho ya dunia, ikisema kwenye masikio ya wale wote walio hai, ikisema—Tubuni, na jitayarisheni kwa ajili ya siku ile kuu ya Bwana?

22 Ndiyo, na tena, wakati vimulimuli vya radi vitakapomulika kutoka mashariki hadi magharibi, na kutoa sauti zao kwa wale wote waishio, na kufanya masikio ya wote kuwaka ya wale wenye kusikia, zikisema maneno haya—Tubuni ninyi, kwani siku ile kuu ya Bwana imekuja?

23 Na tena, Bwana atatoa sauti yake kutoka mbinguni, akisema: Sikieni, Enyi mataifa ya dunia, na yasikilizeni maneno ya yule Mungu aliyewaumba ninyi.

24 Ee, ninyi mataifa ya dunia, ni mara ngapi nimetaka kuwakusanya pamoja kama vile kuku avikusanyavyo pamoja vifaranga vyake chini ya mabawa yake, lakini hamkutaka!

25 Na ni mara ngapi nimewaita ninyi kwa vinywa vya watumishi wangu, na kwa kutembelewa na malaika, na kwa sauti yangu mwenyewe, na kwa sauti ya ngurumo za radi, na kwa sauti ya radi, na kwa sauti za tufani, na kwa sauti za matetemeko ya ardhi, na kwa tufani ya mvua ya mawe, na kwa sauti za njaa, na madhara ya kila aina, na kwa sauti kuu ya parapanda, na kwa sauti ya hukumu, na kwa sauti ya huruma kwa siku nzima, na kwa sauti ya utukufu na heshima na utajiri wa uzima wa milele, na ningewaokoa kwa wokovu usio na mwisho, lakini hamkutaka!

26 Tazama, siku imekuja, wakati kikombe cha ghadhabu ya uchungu wa hasira yangu kimejaa.

27 Tazama, amini ninawaambia, kwamba haya ni maneno ya Bwana Mungu wenu.

28 Kwa hivyo, fanyeni kazi, fanyeni kazi katika shamba langu la mizabibu kwa mara ya mwisho—kwa mara ya mwisho waiteni wakazi wa dunia hii.

29 Kwani katika saa yangu mwenyewe nitakuja juu ya dunia katika hukumu, na watu wangu watakombolewa na watatawala pamoja nami duniani.

30 Kwani ile Milenia kuu, ambayo niliinena kwa vinywa vya watumishi wangu itakuja.

31 Kwani Shetani atakuwa amefungwa, na wakati atakapoachiliwa tena atatawala kwa kipindi kifupi tu, na hapo ndipo mwisho wa dunia utakapokuja.

32 Na yule ambaye anaishi katika haki atabadilishwa katika kufumba na kufumbua macho, na dunia itapita kama vile kwa moto.

33 Na waovu watakwenda zao katika moto usiozimika, na mwisho wao hakuna mtu aujuaye hapa duniani, wala kamwe hatajua, hadi watakapokuja mbele yangu katika hukumu.

34 Sikilizeni ninyi maneno haya. Tazama, Mimi ni Yesu Kristo, Mwokozi wa ulimwengu. Yatunzeni mambo haya katika mioyo yenu, na taadhima ya milele iwe akilini mwenu.

35 Kuweni makini. Shikeni amri zangu zote. Hivyo ndivyo. Amina.