Misaada ya Kujifunza
TJS, Mathayo 13


TJS, Mathayo 13:39–44. Linganisha na Mathayo 13:39–42; ona pia M&M 86:1–7

Kabla ya mwisho wa ulimwengu (maangamizo ya waovu), wajumbe waliotumwa toka mbinguni watawakusanya wenye haki kutoka miongoni mwa waovu.

39 Mavuno ni mwisho wa ulimwengu, au maangamizo ya waovu.

40 Wavunaji ni malaika, au wajumbe waliotumwa toka mbinguni.

41 Vivyo hivyo, kwa sababu, makapi yanakusanywa na kuchomwa katika moto, ndivyo itakavyokuwa mwisho wa dunia, au maangamizi ya waovu.

42 Kwani katika siku ile kabla Mwana wa mtu hajaja, atawatuma mbele malaika wake na wajumbe wa mbinguni.

43 Na watakusanya kutoka kwenye ufalme wake vitu vyote ambavyo vinachukiza, na wale wanaofanya uovu, na atawatupa miongoni mwa waovu; na hapo patakuwa na kilio na kusaga meno.

44 Kwani ulimwengu utaunguzwa na moto.