Misaada ya Kujifunza
TJS, Mathayo 26


TJS, Mathayo 26:22, 24–25. Linganisha na Mathayo 26:26–28; TJS, Marko 14:20–25

Yesu kwanza anamega mkate wa sakramenti kisha anaubariki. Sakramenti ni ukumbusho wa mwili na damu ya Yesu.

22 Na walipokuwa wakila, Yesu alitwaa mkate na akaumega, na akaubariki, na akaumega akawapa wanafunzi wake, akisema, Twaeni mle, hii nikatika ukumbusho wa mwili wangu ambao nautoa kwa ajili yenu.

24 Maana hii ni katika ukumbusho wa damu yangu ya agano jipya, ambayo inamwagwa kwa ajili ya wengi kadiri watakavyoamini katika jina langu, kwa ajili ya ondoleo la dhambi zao.

25 Nami ninawapa amri, ya kwamba kumbukeni kufanya mambo mliyoyaona mimi nikifanya, na kunishuhudia mimi hata mwisho.