Misaada ya Kujifunza
TJS, Mathayo 17


TJS, Mathayo 17:10–14. Linganisha na Mathayo 17:11–13

Yesu anafundisha juu ya akina Elia wawili—mmoja kuandaa na mwingine kurejesha.

10 Naye Yesu akajibu na kuwaambia, Kweli Elia yu aja kwanza, na kurejesha mambo yote, kama manabii walivyoandika.

11 Na tena ninawaambia kwamba Elia amekwisha kuja, juu yake yeye ambaye imeandikwa. Tazama, nitamtuma mjumbe wangu, naye ataitengeneza njia mbele yangu; na hawakumtambua, na wakamtenda, yote waliyotaka.

12 Vivyo hivyo pia Mwana wa mtu atateswa nao.

13 Lakini ninakuambieni ninyi, Elia ni nani? Tazama, huyu ndiye Elia, ambaye nilimtuma kuitengeneza njia mbele yangu.

14 Basi wanafunzi wakafahamu kwamba aliwaambia juu ya Yohana Mbatizaji, na pia juu ya mwingine ambaye atakuja na kurejesha mambo yote, kama ilivyoandikwa na manabii.