2010–2019
Baraka za Kuabudu
Oktoba 2016


Baraka za Kuabudu

Kuabudu ni muhimu na ni kitovu cha maisha yetu ya kiroho. Ni kitu ambacho tunapaswa kutamania, shughulikia kwa dhati na tujitahidi kufanya.

Ziara Yake

Mojawapo ya matukio mazuri ya ajabu yaliyorekodiwa katika maandiko ni historia ya huduma ya Mwokozi kwa watu wa bara la Amerika kufuatia kifo Chake na Ufufuko. Watu walikuwa wameathirika na uharibifu mkubwa sana kiasi cha kwamba ulisababisha “uso wa ardhi yote [uligeuzwa].”1 Kumbukumbu ya matukio haya inaonyesha kwamba kufuatia machafuko hayo watu wote walilia kwa muda mrefu,2 na kwenye huzuni yao kubwa, walihitaji zaidi uponyaji, amani, na ukombozi.

Wakati Mwokozi alishuka kutoka mbinguni, umati uliinama miguuni Mwake mara mbili. Mara ya kwanza ilifanyika baada ya Yeye kutangaza, kwa mamlaka takatifu:

“Tazama, Mimi ni Yesu Kristo ambaye manabii walishuhudia atakuja ndani ya ulimwengu.

“Na tazama mimi ni nuru na uzima wa ulimwengu.”3

Kisha aliwaalika wale waliokuwepo “inukeni na mje kwangu, ili msukume mikono yenu na muitie kwenye ubavu wangu, na pia kwamba mguse alama za misumari katika mikono yangu na katika miguu yangu, ili mjue mimi ni Mungu wa Israeli, na Mungu wa ulimwengu wote, na nimeuawa kwa ajili ya dhambi za ulimwengu.…

“Na wakati walipokuwa wameenda wote na kujishuhudia wenyewe, walipaza sauti kwa toleo moja wakisema:

“Hosana! Heri liwe jina la Mungu Aliye Juu Sana!”4

Na kisha, kwa mara ya pili, “Na waliinama chini miguuni mwa Yesu.” Lakini safari hii na lengo, kwani tunagundua kwamba “walimwabudu.”5

Siku Hizi

Mapema mwakani nilikuwa na jukumu la kutembelea kigingi kule magharibi mwa Marekani. Ilikuwa Jumapili ya kawaida, mkutano wa kawaida, na waumini wa kawaida wa Kanisa. Nilitazama watu wakiingia katika jumba la mikutano na kwa unyenyekevu wakiketi kwenye viti vilivyokuwa wazi. Dakika ya mwisho, mazungumzo ya sauti ya chini yalisikika kote ukumbini. Kina mama na kina baba walijaribu—wakati mwingine bila mafanikio—kuwatuliza watoto wenye nguvu. Kawaida.

Lakini, kabla ya mkutano kuanza, maneno yaliyojaa msukumo yalinijia akilini mwangu.

Waumini hawa hawakuwa wamekuja tu kutekeleza jukumu au kusikiliza wasemaji.

Walikuwa wamekuja kwa ajili ya sababu muhimu zaidi.

Walikuwa wamekuja “kuabudu.

Mkutano ulipokuwa ukiendelea, niliwachunguza kwa makini waumini mbali mbali katika mkusanyiko. Walikuwa na sura kama za mbinguni, mtazamo wa staha na amani. Kitu fulani kuwahusu kilichangamsha moyo wangu. Tukio walilokuwa wakipitia Jumapili hiyo lilikuwa la ajabu sana.

Walikuwa wakiabudu.

Walikuwa wakishuhudia mbinguni.

Niliweza kuona haya katika nyuso zao.

Na nilifurahia na kuabudu pamoja nao. Na nilipofanya hivyo, Roho alinisemeza moyoni. Na siku hiyo, nilijifunza kitu kunihusu, kuhusu Mungu, na sababu ya kuabudu kwa kweli maishani mwetu.

Kuabudu katika Maisha Yetu ya Kila Siku

Watakatifu wa Siku za Mwisho ni wa kipekee tunapozungumzia kuhusu kuhudumu katika miito ya Kanisa. Lakini mara nyingine tunaweza kufanya kazi yetu kama kawaida, kama kwamba tunatekeleza jukumu tu. Mara nyingine kuhudhuria kwetu katika mikutano ya sakramenti na huduma katika ufalme kunaweza kukosa sifa takatifu ya kuabudu. Na bila hiyo, tunakosa tukio lisilo kifani la kiroho na la milele—ambalo ni haki yetu kama watoto wa Baba mpendwa wa Mbinguni.

Mbali na kuwa kibahati, tukio la furaha, kuabudu ni muhimu na kitovu cha maisha yetu ya kiroho. Ni kitu ambacho tunapaswa kutamania, shughulikia kwa dhati na tujitahidi kufanya.

Kuabudu ni Nini?

Wakati tunapomuabudu Mungu, tunamkaribia kwa upendo, unyenyekevu, na kuabudu kwa heshima. Tunamtambua na kumkubali kama mfalme wetu mkuu, Muumba wa ulimwengu, Baba yetu mpendwa na anayetupenda milele.

Tunamheshimu na tunamstahi.

Tunajisalimisha Kwake.

Tunainua mioyo yetu kwa maombi ya ujasiri, tunapenda neno Lake, tunafurahia neema Yake, na tunajitolea kumfuata kwa uaminifu.

Kumuabudu Mungu ni sehemu muhimu sana katika maisha ya mwanafunzi wa Yesu Kristo kiasi cha kwamba ikiwa tutakosa kumpokea mioyoni mwetu, tutamtafuta bila mafanikio katika mabaraza yote makanisani, na hekaluni.

Wanafunzi wa kweli wanavutiwa “kumwabudu yeye aliyezifanya mbingu, na dunia, na bahari, na chemi chemi za maji—wakililingana jina la Bwana mchana na usiku.”6

Tunaweza kujifunza mengi kuhusu ibada ya kweli kwa kuchunguza jinsi wengine—watu ambao pengine hawakuwa tofauti sana nasi—walipitia, walitenda, na kuabudu katika uwepo wa mtakatifu.

Ajabu, Shukrani, na Matumaini

Mwanzoni mwa karne ya 19, Wakristo walikuwa wametupilia mbali fikra ya kwamba Mungu bado alizungumza na binadamu. Lakini katika majira ya kuchipuka ya 1820, hilo lilibadilika milele wakati mvulana mnyenyekevu wa shamba aliingia katika kijisitu na akapiga magoti kusali. Kutoka siku hiyo, mfululizo wa maono ya ajabu, ufunuo, na matokeo ya mbinguni yamejaa duniani, ukiwapa wenyeji ufahamu wa thamani kuhusu asili na mipango ya Mungu na uhusiano Wake na binadamu.

Oliver Cowdery alielezea siku hizo kama “kamwe hazitasahaulika. … Ni shangwe gani! ni mshangao gani! ni mastaajabu gani!”7

Maneno ya Oliver yanaelezea vitu vya asili vinavyoambatana na ibada ya kweli ya aliye mtukufu—hisia ya mastaajabu makuu na shukrani ya ajabu.

Kila siku, lakini hasa siku ya Sabato, tuna nafasi ya ajabu kushiriki mshangao na mastaajabu ya mbinguni na kumsifu Mungu kwa wema Wake mtakatifu na huruma Yake ya kupindukia.

Hii itatuelekeza kutumaini. Hivi ndivyo vitu vya asili vya ibada.

Nuru, Ufahamu, na Imani.

Wakati wa siku tukufu ya Pentekoste, Roho Mtakatifu aliingia katika mioyo na akili ya wanafunzi wa Kristo, akiwajaza na nuru na ufahamu.

Kufikia siku ile hawakuwa na uhakika kile walichohitaji kufanya. Yerusalemu palikuwa mahali pabaya kwa mwanafunzi wa Mwokozi, na lazima walijiuliza jambo gani lingewakuta.

Lakini wakati ambapo Roho Mtakatifu alijaza mioyo yao, shaka na kusitasita kulitoweka. Kupitia tukio tukufu zaidi la kuabudu kikweli, Watakatifu wa Mungu walipokea nuru ya mbinguni, ufahamu, na ushuhuda ulioimarika. Na hilo lilisababisha imani.

Kuanzia wakati huo, Mitume na Watakatifu walitenda kulingana na mwelekeo wa ujasiri. Kwa ujasiri walihubiri Kristo Yesu kwa ulimwengu wote.

Wakati tunapoabudu katika roho, tunaalika nuru na ukweli katika nafsi zetu, ambayo huimarisha imani yetu. Hivi pia ni vitu vya asili vya ibada ya kweli.

Uanafunzi na Hisani

Katika Kitabu cha Mormoni tunajifunza kwamba kutoka wakati ambapo Alma Mdogo alipokombolewa kutokana na kuteseka matokeo ya uasi wake mwenyewe, alibadilika kabisa. Kwa ujasiri “walisafiri katika nchi yote ya Zarahemla … na miongoni mwa watu wote …  , wakijibidiisha kuponya majeraha yote ambayo alikuwa [yeye] amelifanyia kanisa.”8

Kuendelea kuabudu kwake kwa Mwenyezi Mungu kulichukua mtindo wa uanafunzi wenye nguvu.

Ibada ya kweli inatubadilisha kuwa wanafunzi wa kweli na wenye bidii wa Bwana wetu mpendwa na Mwokozi, Yesu Kristo. Tunabadilika na kuzidi kuwa kama alivyo Yeye.

Tunakuwa wenye kuelewa zaidi na wenye kujali. Wenye kusamehe zaidi. Wenye kupenda zaidi.

Tunaelewa kwamba haiwezekani kusema kwamba tunampenda Mungu tukiwa wakati huo huo tunawachukia, kuwafukuza, au kuwapuuza watu wengine walio karibu nasi.9

Ibada ya kweli inasababisha uamuzi dhabiti wa kutembea katika njia ya uanafunzi. Na hiyo hatimaye huleta hisani. Hii pia ni sehemu asili za ibada.

Ingia Milangoni Mwake kwa Shukrani

Wakati ninapotafakari kuhusu kile kilichoanza kama Jumapili asubuhi ya kawaida, katika lile jumba la kawaida la mikutano, katika kile kigingi cha kawaida, hata leo ninaguswa na lile tukio la kiroho la ajabu ambalo milele litabariki maisha yangu.

Nilijifunza kwamba hata ikiwa sisi ni wasimamizi wa kipekee wa muda wetu, miito, na majukumu—hata kama tunaweza kutimiza kila jambo katika orodha yetu ya mtu “mkamilifu”, familia, au kiongozi—ikiwa tutakosa kumuabudu Mkombozi wetu mwenye huruma, Mfalme wa mbinguni, na Mungu mtukufu, tunakosa furaha nyingi na amani ya injili.

Wakati tunapomuabudu Mungu, tunamtambua na kumpokea na staha sawa kama wale watu wa kale katika bara za Amerika. Tunamkaribia na hisia zisizoeleweka za mshangao na mastaajabu. Tunashangaa kwa shukrani wema wa Mungu. Na hivyo basi, tunapata matumaini.

Tunatafakari neno la Bwana, na hayo yanajaza nafsi zetu na nuru na ukweli. Tunaelewa taswira za kiroho ambazo tu zaweza kuonekana kupitia nuru ya Roho Mtakatifu.10 Na hivyo basi, tunapata imani.

Tunapoabudu, nafsi zetu zinasafishwa na tunajitolea kufuata nyayo za Mwokozi wetu mpendwa, Yesu Kristo. Na kutokana na uamuzi huu, tunapata hisani.

Tunapoabudu, mioyo yetu inavutwa kutoa sifa kwa Mungu wetu mbarikiwa asubuhi, mchana, na usiku.

Tunamtakasa na kumsifu daima—katika majumba yetu ya mikutano, nyumbani, hekaluni, na kazi zetu zote.

Tunapoabudu, tunafungua mioyo yetu kwa uwezo wa kuponya wa Upatanisho wa Yesu Kristo.

Maisha yetu yanakuwa ishara na dhihirisho ya ibada yetu.

Kina ndugu na kina dada zangu, matukio ya kiroho yana uhusiano mdogo sana na kile kinachofanyika karibu nasi na yanahusiana katika kila kitu na kile kinachotendeka mioyoni mwetu. Ni ushuhuda wangu kwamba ibada ya kweli itabadilisha mikutano ya kawaida ya Kanisa na kuifanya kuwa karamu za ajabu za kiroho. Itaimarisha maisha yetu, itapanua kuelewa kwetu na kuimarisha ushuhuda wetu. Tunapoelekeza mioyo yetu kwake Mungu, kama Mtunga Zaburi wa kale, sisi “tutaingieni malangoni mwake kwa kushukuru; Nyuani mwake kwa kusifu; [tuna] shukrani kwake, tunalihimidi jina lake.

“Kwa kuwa Bwana ndiye mwema; rehema zake ni za milele; na uaminifu wake hudumu vizazi na vizazi.”11

Kupitia ibada ya kweli na dhati, tunakua na kukomaa kwa matumaini, imani, na hisani. Na kupitia mchakato huo, tunajaza nuru ya mbinguni katika nafsi zetu ambayo inapenyeza maisha yetu na maana tukufu, amani ya kudumu, furaha ya milele.

Hii ni baraka ya kuabudu maishani mwetu. Ninashuhudia haya katika jina takatifu la Yesu Kristo, amina.