2010–2019
Shahidi wa Mungu
Oktoba 2016


Shahidi wa Mungu

Ninapendekeza kwamba uache kuhisi hatia kuhusu upungufu wowote unaohisi kuwa nao katika kushiriki injili. Badala yake, omba “kusimama kama [shahidi] wa Mungu.” Huu ni ushawishi wa nguvu zaidi kuliko hatia.

Kiasi kikubwa cha kazi muhimu ya Mungu hakionekani machoni mwa ulimwengu. Ingawaje katika karne ya sita kabla ya Kristo kulikuwa na wasomi maarufu kama vile Konfisiasi kule Uchina na Buddha, Mashariki mwa India, uwezo wa ukuhani wa Mungu ulikuwa juu ya Danieli, Nabii aliyekuwa akiishi utumwani wakati wa utawala wa mfalme wa Babeli, Nebukadreza.

Akiwa amefadhaika usiku, Mfalme Nebukadreza aliwataka waganga na wachawi wake wote wamweleze kuhusu ndoto yake na tafsiri ya ndoto. Bila shaka, hawangeweza kumwelezea mfalme kile alichokuwa ameota na walilalamika. “Hapana mtu duniani awezaye [kulionyesha neno hili la mfalme; kwa maana hapana mfalme, aliyetaka] neno kama hili .”1 Mfalme Nebukadreza alighadhabika sana kwa sababu ya kushindwa kwao na kwa hasira akatangaza kwamba washauri wake wangeuawa.

Danieli, mmoja kati ya watu wenye hekima wa Mfalme, alisali kwa ajili ya “rehema ya … Mungu … kwa habari ya siri hiyo”2

Muujiza ulitendeka. Siri ya kile mfalme alikuwa ameota ilifunuliwa kwa Danieli.

Danieli alipelekwa mbele ya Mfalme. “Je! Waweza kunijulisha ile ndoto niliyoiona, na tafsiri yake?.”

Danieli akajibu:

“Wenye hekima, wala wachawi, wala waganga [ hawawezi kukufunulia ndoto yako]. …

“Lakini yuko Mungu mbinguni [anayeweza kufunua mambo haya, naye] amemjulisha … Mfalme Nebukadreza mambo yatakayokuwa siku za mwisho. …

“Mungu wa mbinguni,” Danieli alisema [atausimamisha] ufalme, [jiwe likachongwa bila kazi ya mikono, likawa milima mikubwa, likaijaza dunia yote] ambao kamwe hautaangamizwa … [lakini utasimama] milele na milele.

“… “Na ndoto hii,” Danieli alisema, “ni ya hakika, na tafsiri yake … ni thabiti.”3

Akiwa ndoto yake imeelezwa na kutafsiriwa, mfalme alizungumza kwa ujasiri, “Mungu wenu ndiye Mungu wa miungu, na Bwana wa wafalme.”4

Kutokana na msaada wa kimiujiza wa Mungu kwa Danieli kulifuatia wakati uliotabiriwa wa injili ya Yesu Kristo kurejeshwa duniani, “ufalme … [ambao ungeijaza] dunia yote … ambao kamwe hautaangamizwa … [lakini utasimama] milele na milele.

Idadi ya waumini wa Kanisa katika siku za mwisho ingekuwa chache, kama alivyotabiri Nefi, walakini wangekuwa kote usoni mwa dunia, na nguvu na ibada za ukuhani zingepatikana kwa wale wote waliotamani, wakiijaza dunia jinsi Danieli alivyotabiri.5

Mwaka wa 1831 Nabii Joseph Smith alipokea ufunuo huu: “Funguo za ufalme wa Mungu [na kukusanyika kwa Israeli kutoka pande nne za dunia] zimekabidhiwa kwa mwanadamu duniani, na kutoka huko injili itaenea hata miisho ya dunia, kama vile jiwe lililochongwa mlimani bila kazi ya mikono litabiringika, hadi litaijaza dunia yote.”6

Jukumu Letu Wote

Kukusanyika kwa Israeli ni muujiza. Ni kama fumbo kubwa ambalo sehemu zake zitawekwa mahala pake kabla matukio matukufu ya Ujio wa pili. Kama vile tunavyoweza kutatizwa na mlima wa sehemu za fumbo, Watakatifu wa siku za awali ni lazima waliona wajibu wa kueneza injili duniani kote kama jukumu lisilowezekana. Lakini walipoanza, mtu mmoja, sehemu moja ya fumbo kwa wakati mmoja, wakipata vigezo, wakifanya juhudi ili kuitekeleza kazi hii tukufu vyema. Kidogo kidogo, jiwe lililochongwa bila kazi ya mikono likaanza kubingirika; kutoka kwa mamia hadi kwa maelfu, hadi makumi ya maelfu, na hivi sasa mamilioni ya Watakatifu wa Siku za mwisho wenye agano katika kila nchi wanaunganisha sehemu za fumbo la kazi hii ya kushangaza na ya maajabu.

Picha
Fumbo kubwa sana

Kila mmoja wetu ni sehemu ya fumbo, na kila mmoja wetu anatoa usaidizi kupanga sehemu zingine muhimu. Wewe ni muhimu katika kazi hii kuu. Upeo wetu mbele ni wazi. Tunaweza kuona muujiza ukiendelea na mkono wa Mungu ukituongoza tunapojaza mapengo yaliyobaki. Kisha, “Yehova Mkuu atasema kazi imekamilika,”7 na Yeye atarejea kwa ukuu na utukufu.

Picha
Kila mmoja wetu ni sehemu ya fumbo

Rais Thomas  S. Monson alisema: “Sasa ni wakati wa waumini na wamisionari kuja pamoja, kufanya kazi pamoja … kuleta nafsi Kwake. … Atatusaidia katika juhudi zetu ikiwa tutatenda kwa imani ili kutimiza kazi Yake.”8

Jukumu takatifu lililoteuliwa ambalo kwa wakati mmoja lilikuwa juu ya wamisionari pekee hivi sasa liko juu yetu sisi wote. Sisi wote tunataka kushiriki injili iliyorejeshwa, na kwa shukrani, maelfu wanabatizwa kila wiki. Lakini hata na baraka hii ya ajabu, shauku yetu kwa kina kaka na dada zetu na hamu yetu kumridhisha Mungu inaleta umuhimu wa kuvutia kushiriki na kuimarisha ufalme wa Mungu kote duniani.

Vipimo vya Hatia

Hata kuwa na hamu kubwa ya kushiriki injili, unaweza kuwa na furaha kidogo kwa sababu ya ufanisi wa juhudi zako za awali. Unaweza kuhisi kama rafiki aliyesema, “Nimezungumza na familia yetu na marafiki kuhusu Kanisa, lakini wachache wameonyesha hamu ya kutaka kujua, na kila nilipokataliwa, ninasita zaidi. Ninajua ninapaswa kufanya zaidi, lakini nimekwama, na ninahisi hatia kubwa.”

Acha nione kama ninaweza kutoa usaidizi.

Hatia ina jukumu muhimu kwa maana inatusaidia kufanya mabadiliko tunayohitaji kufanya, lakini kuna kikomo pale ambapo hatia itatusaidia.

Hatia ni kama betri katika gari linalotumia petroli. Italiwasha gari, itaanzisha injini, na iwashe taa za mbele, lakini haitatoa nguvu kwa safari ndefu iliyo mbele. Betri, peke yake, haitoshi. Na wala pia hatia.

Ninapendekeza kwamba uache kuhisi hatia kuhusu upungufu wowote unaohisi kuwa nao katika kushiriki injili. Badala yake, sali kama Alma alivyofundisha, kwa ajili ya nafsi za “kusimama kama [shahidi] wa Mungu nyakati zote na katika vitu vyote, na katika mahali popote … ili [wengine] waweze kukombolewa na Mungu, na kuhesabiwa pamoja na wale wa ufufuko wa kwanza, [na] mpokee uzima wa milele.”9 Huu ni ushawishi wa nguvu zaidi kuliko hatia.

Kuwa shahidi wa Mungu katika nyakati zote na katika mahali popote kunaonyesha jinsi tunavyoishi na jinsi tunavyozungumza.

Kuwa wazi kuhusu imani yako katika Kristo. Wakati nafasi inapojitokeza, zungumza kuhusu maisha Yake, mafundisho Yake, na zawadi Yake kwa wanadamu isiyolinganishwa. Shiriki kweli hizi zenye nguvu kutoka Kitabu cha Mormoni. Ametupa ahadi hii: “Mtu … atakayenikiri mbele ya watu, nami nitamkiri mbele za Baba yangu wa mbinguni.”10 Ninawaahidi ya kwamba mtakapozidi kusali na kwa dhati kwa ajili ya nafasi ya “kusimama kama mashahidi wa Mungu,” nafasi hizo zitakuja, na wale wanaotafuta nuru zaidi na ufahamu utawekwa mbele yenu. Mnapojibu misukumo ya kiroho, Roho Mtakatifu atayapeleka maneno yako katika moyo wa mwingine, na siku moja Mwokozi atakukiri mbele ya Baba Yake.

Juhudi ya Kikundi

Kazi ya kiroho ya kumsaidia mtu kuingia katika ufalme wa Mungu ni juhudi ya kundi. Washirikisheni wamisionari mapema muwezavyo, na msali ili mmpate usaidizi kutoka mbinguni. Lakini kumbuka, wakati wa uongofu wa mwingine haukutegemei wewe kabisa.11

Kamla Persand alikuwa anatoka kisiwa cha Mauritius, alikuwa anasoma katika shule ya udaktari kule Bordeaux Ufaransa, wakati tulipokutana naye mnamo Februari ya 1991. Tulikuwa tumesali kama familia ili tuweze kushiriki injili na mtu aliyekuwa anatafuta ukweli, na tulimfundisha nyumbani kwetu. Nilipata nafasi ya kumbatiza, lakini hatukuwa vishawishi vikuu zaidi katika kujiunga na Kanisa kwa Kamla. Marafiki, wamisionari, na hata waumini walikuwa “mashahidi wa Mungu” nchini mwake, na siku moja kule Ufaransa, wakati ulioofaa kwake Kamla, alifanya uamuzi wa kubatizwa. Sasa, miaka 25 baadaye, baraka za uamuzi huo zimemzingira kila pembe, na mwanawe ni mmisionari kule Madagascar.

Picha
Kamla Persand na familia yake

Tafadhali usione kama kwamba juhudi zako za kushiriki upendo wa Mwokozi na mwingine kama mtihani wa kufaulu/kufeli alama zako zikiamuliwa na namna marafiki zako wanavyopokea hisia zako chanya au mwaliko wako wa kukutana na wamisionari.12 Kwa macho yetu ya kimwili, hatuwezi kutathmini athari za juhudi zetu, au kutengeneza ratiba. Wakati tunaposhiriki upendo wa mwokozi na mwingine, alama yetu daima ni A+.

Baadhi ya serikali zimewekea vikwazo kazi ya wamisionari, hii imewafanya waumini wetu adili kuonyesha hata ujasiri mkubwa zaidi kwa kuwa “mashahidi wa Mungu nyakati zote na katika mahali popote.”

Nadezhda kutoka Moscow mara nyingi huwapa wengine Kitabu cha Mormoni katika sanduku la zawadi pamoja na peremende zikiwa zimekizingira. “Nitawaambia,” alisema, “hiyo ni zawadi nzuri kabisa ningeweza kuwapa.”

Muda mfupi baada ya kubatizwa kule Ukraine, Svetlana alipata msukumo wa kushiriki injili na bwana fulani aliyemwona kila mara katika basi. Wakati bwana huyu aliposhuka kwenye kituo chake, alisema, “Unaweza kutaka kujua zaidi kumhusu Mungu?” Bwana huyo alisema, “Ndiyo.” Wamisionari walimfundisha Viktor, na alibatizwa. Yeye na Svetlana baadaye waliunganishwa katika Hekalu la Freiberg Germany.

Kuweni waangalifu; baraka zenu zaweza kuja katika njia usiyotarajia.

Miaka saba iliyopita, mimi na Kathy tulikutana na Diego Gomez na familia yake nzuri Jijini Salt Lake. Walihudhuria maonyesho ya hekalu pamoja nasi lakini kwa upole walikataa mwaliko wetu kujifunza zaidi kuhusu Kanisa. Mwezi Mei iliyopita nilipokea simu ya kushangaza kutoka kwake Diego. Matukio katika maisha yake yalikuwa yamemnyenyekeza. Alikuwa amewapata wamisionari yeye mwenyewe, akawa amefundishwa, na alikuwa tayari kwa ubatizo. Juni tarehe 11 iliyopita, niliingia katika maji ya ubatizo pamoja na rafiki yangu na mwanafunzi mwenzi Diego Gomez. Kuongoka kwake kulifuata ratiba yake na kulifanyika kwa usaidizi na msaada wa wengi waliojitokeza kumsaidia kama “mashahidi wa Mungu.”

Picha
Diego Gomez pamoja na kundi

Mwaliko kwa Vijana

Kwa vijana wetu wa ajabu na vijana wazima kote duniani, ninawapa mwaliko maalum na mwito muwe “mashahidi wa Mungu.” Wale walio karibu nanyi wako radhi kwa uchunguzi wa kiroho. Unakumbuka fumbo? Usije kazini mikono mitupu, lakini kwa teknolojia na mitandao ya kijamii chini ya utawala wako. Tunawahitaji; Bwana anawahitaji mchangie zaidi katika kazi hii kuu.

Picha
Fumbo katoka simu tamba

Mwokozi alisema, “Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu.”13

Sio kwa bahati kwamba unaishi Afrika, Asia, Uropa, Kaskazini, Kati, au Kusini mwa Amerika, Pasifiki, au mahala pengine katika Dunia ya Mungu kwa sababu injili sharti iende katika “kila nchi, ukoo, ndimi, na watu.”14

“Mungu wa mbinguni [ameusimamisha] ufalme, [ jiwe lililochongwa bila kazi ya mikono, likawa mlima mkubwa, likaijaza dunia yote] kamwe ambao hautaangamizwa …[lakini utasimama] milele na milele.”

“… “Ndoto hii ni ya hakika, na tafsiri yake … ni thabiti.”15

Ninafunga na maneno kutoka Mafundisho na Maagano: “Mlinganeni Bwana, ili ufalme wake uweze kuenea juu ya dunia, ili wakazi wake waweze kuupokea, na kujitayarisha kwa ajili ya siku zijazo, siku ambazo Mwana wa Mtu atashuka kutoka mbinguni, aliyevikwa katika mng’aro wa utukufu wake, kukutana na ufalme wa Mungu ambao umewekwa duniani.16 Katika jina la Yesu Kristo, amina.

Muhtasari

  1. Danieli 2:10.

  2. Danieli 2:18 AM.

  3. Danieli 2:26–28, 44–45; ona piamistari ya 34–35.

  4. Danieli 2:47 AM.

  5. Ona 1  Nefi 14:12–14.

  6. Mafundisho na Maagano 65:2; ona pia Mafundisho na Maagano 110:11.

  7. Teachings of Presidents of the Church: Joseph Smith (2007), 444; ona pia Boyd K. Packer, “The Standard of Truth Has Been Erected,” Liahona, Nov. 2003, 27.

  8. Thomas S. Monson, “Welcome to Conference, Liahona, Nov. 2013, 4.

  9. Mosia 18:9.

  10. Mathayo 10:32.

  11. Mwezi mmoja uliopita nilikua kule Santa Maria, Brazil. Ndugu João Grahl aliniambia kwamba, kama mvulana, alikuwa ameshiriki kanisa kwa muda wa miaka miwili, akitaka kubatizwa, lakini baba yake hangemruhusu. Siku moja aliwaambia dada zake, ambao walikuwa na hamu sawa, kwamba walihitaji kupiga magoti na kusali ili Mungu aguse moyo wa baba yao. Walipiga magoti na kusali na wakaenda shuleni.

    Waliporudi nyumbani siku hiyo, cha kushangaza, mjomba wao, ndugu ya baba yao, alikuwa amewasili kutoka mji wa mbali. Alikuwa nyumbani kwao akizungumza na baba yao. Mjomba wao akiwa chumbani, watoto mara nyingine walimuuliza baba yao ikiwa wangeweza kubatizwa. Mjomba wao alisimama na kuwekelea mkono wake mabegani mwa ndugu yake mdogo na kusema, “Reinaldo, ni kweli. Waruhusu wabatizwe.” Isijulikane kwa yeyote kati yao, mjomba wao alikuwa amebatizwa miezi kadhaa iliyopita.

    Mjombake alitiwa msukumo amtembelee ndugu yake nyumbani kwake, na kwa sababu “alisimama kama shahidi wa Mungu” siku hiyo, wapwa zake walikubaliwa kubatizwa. Wiki chache baadaye, Reinaldo na mkewe walibatizwa. Mungu alijibu sala za watoto wale kwa njia ya kimiujiza kupitia mtu ambaye alikuwa radhi kuwa “shahidi wa Mungu.”

  12. “Utafanikiwa unapoalika, bila kujali matokeo ni nini” (Clayton M. Christensen, TThe Power of Everyday Missionaries [2012], 23; ona pia everydaymissionaries.org).

  13. Mathayo 28:19.

  14. Mosia 15:28.

  15. Danieli 2:44–45; ona piamistari ya 34–35.

  16. Mafundisho na Maagano 65:5.