2010–2019
Kuidhinishwa kwa Maofisa wa Kanisa
Oktoba 2016


Kuidhinishwa kwa Maofisa wa Kanisa

Kina kaka na kina dada, Rais Monson ameniomba niwasilishe kwenu majina ya Maofisa Wakuu na Wale Sabini wa Maeneo wa Kanisa kwa ajili ya kura yenu ya kuwakubali.

Inapendekezwa kwamba tumkubali Thomas Spencer Monson kama nabii, mwonaji, na mfunuzi na Rais wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho; Henry Bennion Eyring kama Mshauri wa Kwanza katika Urais wa Kwanza; na Dieter Friedrich Uchtdorf kama Mshauri wa Pili Katika Urais wa Kwanza.

Wale wote wanaoukubali wanaweza kuonyesha.

Wale wanaopinga, wanaweza kuonyeshe pia.

Inapendekezwa kwamba tumkubali Russell Marion Nelson kama Rais wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili na wafuatao kama washiriki wa Akidi hiyo: Russell M. Nelson, Dallin H. Oaks, M. Russell Ballard, Robert D. Hales, Jeffrey R. Holland, David A. Bednar, Quentin L. Cook, D. Todd Christofferson, Neil L. Andersen, Ronald A. Rasband, Gary E. Stevenson, na Dale G. Renlund.

Wale wanaokubali, wanaweza kuonyesha ishara.

Yeyote anayepinga anaweza kuonyesha ishara.

Inapendekezwa kwamba tuwakubali washauri katika Urais wa Kwanza na Akidi ya Mitume Kumi na Wawili kama manabii, waonaji, na wafunuzi.

Wale wote wanaokubali, tafadhali onyesheni.

Kinyume, kama kuna yeyote, kwa ishara hiyo hiyo.

Inapendekezwa kwamba tuwaapumzishe kwa shukrani kwa huduma yao nzuri Wazee Daniel L. Johnson, Jairo Mazzagardi, Kent F. Richards, na Francisco J. Viñas kama Kama Viongozi Wakuu Wenye Mamlaka na kuwapa wadhifa huo wakiwa wamestaafu. Tunatambua huduma ya Mzee Per G. Malm, ambaye aliaga Julai 26, 2016. Tunapenda kutuma salamu za upendo na rambi rambi zetu za dhati kwa Dada Malm, watoto wao, wajukuu wao.

Wale ambao wangependa kuungana nasi katika kutoa shukrani kwa Ndugu hawa kwa huduma yao ya ajabu, tafadhali onyesheni.

Inapendekezwa kwamba tummpuzishe Alan R. Walker kama Sabini wa Eneo. Wale wangependa kuonyesha shukrani zao kwake Ndugu Walker kwa huduma yake, tafadhali onyesheni hivyo.

Inapendekezwa kwamba tuwakubali wafuatao kama Sabini wa Eneo: Bhanu K. Hiranandani na Sandino Roman.

Wale wote wanaokubali, tafadhali waonyeshe.

Wale wanaopinga, ikiwa wapo.

Imependekezwa kwamba tuwaidhinishe Viongozi Wakuu, Sabini wa Eneo, na urais mkuu wa vikundi saidizi kama ilivyo sasa.

Wote wanaokubali, tafadhali waonyeshe ishara.

Kinyume, kama kuna yeyote, kwa ishara hiyo hiyo.

Rais Monson, upigaji kura umebainishwa. Tunawaalika wale wote ambao inawezekana kuwa wamepinga mapendekezo yoyote kuwasiliana na marais wao wa vigingi.

Kina kaka na kina dada, asanteni kwa imani na sala zenu endelevu kwa niaba ya viongozi wa Kanisa.