2010–2019
Unyenyekevu na Upole wa Moyo
Aprili 2018


Unyenyekevu na Upole wa Moyo

Unyenyekevu ni ufafanuzi wa sifa ya Mkombozi na unatofautishwa na uitikivu wa kimaadili, kuwa radhi kuwa mnyonge, na kizuizi binafsi cha nguvu.

Mimi ninafurahia fursa hii takatifu ya kuwakubali viongozi wetu wa Kanisa, na kwa moyo mkunjufu ninamkaribisha Mzee Gong na Mzee Soares kwenye Akidi ya Mitume Kumi na Wawili. Huduma ya wanaume hawa waaminifu itawabariki watu binafsi na familia ulimwenguni kote, na nina shauku kuhudumia na kujifunza kutoka kwao.

Ninaomba Roho Mtakatifu atafundisha na kutuelimisha tunapojifunza pamoja kuhusu kipengele muhimu cha asili takatifu ya Mwokozi1 ambayo kila mmoja wetu hana budi kujitahidi kuiga.

Nitatoa baadhi ya mifano ambayo inasisitiza hali hii ya Kikristo kabla kufafanua sifa halisi baadaye katika ujumbe wangu. Tafadhali sikilizeni kwa makini kila mfano na fikirini pamoja nami majibu ya kufaa kwa maswali nitakayotoa.

Mfano #1. Kijana Tajiri na Amuleki

Katika Agano Jipya, tunajifunza kuhusu kijana tajiri ambaye alimwuliza Yesu, “Mwalimu Mwema, nifanye kitu gani kizuri, ili niweze kupata uzima wa milele?”2 Mwokozi kwanza ilimuasa atii amri. Mwalimu alimpa sharti la ziada mahususi kwa yule kijana kwa mahitaji yake maalumu na mazingira.

“Yesu akamwambia, “Ukitaka kuwa mkamilifu, enenda ukauze ulivyo navyo, na uwape maskini, na utakuwa na hazina mbinguni: na njoo unifuate.

“Lakini aliposikia usemi ule, aliondoka zake kwa huzuni: kwani alikuwa na utajiri mkubwa.”3

Fananisha mwitikio wa kijana tajiri na uzoefu wa Amuleki, kama ulivyoelezwa katika Kitabu cha Mormoni. Amuleki alikuwa mchapa kazi na mwenye mafanikio akiwa na ndugu wengi na marafiki.4 Alijielezea mwenyewe kama mtu ambaye aliitwa mara nyingi lakini hakusikia; mtu aliyejua mambo ya Mungu lakini asingeweza kuyafahamu.5 Kimsingi mtu mwema, Amuleki alivutiwa na mambo ya kilimwengu sawa kabisa na kijana tajiri aliyesimuliwa katika Agano Jipya.

Hata kama hapo mwanzo aliufanya mgumu moyo wake, Amuleki alitii sauti ya malaika, alimpokea nabii Alma nyumbani mwake, na akampa chakula. Aliamshwa kiroho wakati wa ziara ya Alma na aliitwa kuhubiri injili. Amuleki kisha akatelekeza “dhahabu yake yote, na fedha, na vitu vyake vya thamani … kwa neno la Mungu, [na alikuwa] akikataliwa na wale ambao walikuwa marafiki zake kitambo, na pia na baba yake na jamaa yake.6

Unafikiri nini kinaelezea tofauti kati ya majibu ya tajiri kijana Tajiri na Amuleki?

Mfano no.1 Pahorani

Wakati wa hatari ya vita uliosimuliwa katika Kitabu cha Mormoni, ubadilinishaji wa nyaraka ulitokea kati ya Moroni, kapteni wa majeshi ya Wanefi, na Pahorani, hakimu mkuu na mtawala wa nchi. Moroni, ambaye jeshi lake lilikuwa linateseka kwa sababu ya kukosa msaada wa kutosha kutoka serikalini, alimwandikia Pahorani “kwa njia ya lawama”7 na alimshutumu na viongozi wenzake kwa uzembe, uvivu, kutojali, na hata kuwa wasaliti.8

Pahorani kirahisi angeweza kumchukia Moroni na madai yake yasiyo sahihi, lakini hakufanya hivyo. Alijibu kwa huruma na akaelezea uasi dhidi ya serikali ambao Moroni hakuwa anaujua. Na kisha Pahorani anatangza:

“Tazama, nakwambia, Moroni, kwamba sijawi shangwe na mateso yako makuu, ndio, inaisikitisha roho yangu. …

“Na sasa kwenye barua yako, umenilaumu, lakini hainijalishi; sijakasirika, lakini nina furaha kwa ujasiri wa moyo wako.”9

Unafikiri ni nini kinaelezea jibu zito la Pahora kwa mashitaka ya Moroni?

Mfano no.1 Rais Russell M. Nelson na Rais Henry B. Eyring

Katika mkutano mkuu miezi sita iliyopita.Rais Russell M. Nelson alisimulia jibu lake kwa mwaliko wa Rais Thomas S.Monson kujifunza, kutafakari, na kutumia kweli zilizomo katika Kitabu cha Mormoni. Alisema, “Nimejaribu kufuata ushauri wake. Miongoni mwa vitu vingine, nimeweka orodha ya Kitabu cha Mormoni ni nini, kinathibisha, nini kinakanusha, nini kinatimiza, nini kinafafanua, na nini kinafunua. Kuangalia Kitabu cha Mormoni kupitia lensi hizo imekuwa ni zoezi la umaizi na msukumo! Ninapendekeza kwa kila mmoja wenu.”10

Rais Henry B. Eyring vilevile alisisitiza umuhimu katika maisha yake ya ombi la Rais Monson. Alisema:

“Nimesoma Kitabu cha Mormoni kila siku kwa zaidi ya miaka 50. Kwa hiyo labda ningeweza kufikiri kimantiki kwamba maneno ya Rais Monson yalikuwa ya kwa mtu mwingine. Hata hivyo, Kama wengi wenu, Nilihisi hamasa ya Nabii na ahadi yake ikinialika kufanya bidii zaidi. …

“Tokeo la furaha kwangu, na kwa wengi wenu, limekuwa kile nabii alichoahidi.”11

Unafikiri nini kinaelezea majibu ya dhati na ya mara moja kwa mwaliko wa Rais Monson kwa viongozi hawa wawili wa Kanisa la Bwana?

Simaanishi kwamba majibu yenye nguvu ya kiroho ya Amuleki, Pahorani, Rais Nelson na Rais Eyring yanaelezwa kwa aina moja tu ya tabia ya kama Kristo Kwa hakika, sifa nyingi zinazohusiana na uzoefu ziliongoza kwenye kupevuka kiroho kulikooneshwa katika maisha ya watumishi hawa waadilifu wanne. Lakini Mwokozi na manabii Wake wamesisitiza sifa muhimu kwamba sisi wote tunahitaji uelewa kamili zaidi na kujitahidi kushirikisha katika maisha yetu.

Unyenyekevu

Tafadhali tazama sifa alizotumia Bwana kujielezea Mwenyewe katika maadiko yafuatayo: “Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu.”12

Kwa kuelimisha, Mwokozi alichagua kusisitiza unyenyekevu kutoka miongoni mwa sifa zote na maadili kwa uwezekano angeweza kuchagua.

Mpangilio unaofanana uko wazi katika ufunuo uliopokelewa na nabii Joseph Smith mwaka 1829. Bwana alitangaza, “Jifunze kwangu, na sikiliza maneno yangu; enenda katika unyenyekevu wa Roho wangu, na utapata amani kwangu.”13

Unyenyekevu ni ufafanuzi wa sifa ya Mkombozi na unatofautishwa na uitikivu wa kimaadili, kuwa radhi kuwa myonge, na kizuizi binafsi cha nguvu. Sifa hii inatusaidia kuelewa kikamilifu zaidi majibu pekee ya Amuleki, Pahorani, Rais Nelson, na Rais Eyring.

Kwa mfano, Rais Nelson na Rais Eyring kiadilifu na kwa haraka walijibu kutiwa kwao moyo na Rais Monson kusoma na kujifunza Kitabu cha Mormoni. Ingawa wote wawili walikuwa wanahudumia nafasi muhimu za wazi Kanisani na walikuwa wamejifunza maandiko kwa kina kwa miongo mingi, walionesha katika majibu yao kutosita au hisia ya kujikweza wenyewe.

Amuleki kwa hiari yake alijitoa kwa mapenzi ya Mungu, alikubali wito kuhubiri injili, na kuacha nyuma yake mazingira ya starehe na mahusiano ya kawaida. Na Pahorani alibarikiwa na taswira na kujizuia kwa nguvu kutenda kuliko kuitikia kama alivyoeleza kwa Moroni changamoto zinazotokea kutoka uasi dhidi ya serikali.

Sifa ya kama Kristo ya unyenyekevu mara nyingi imeeleweka vibaya katika ulimwengu wetu wa siku hizi. Unyenyekevu ni imara, sio dhaifu; tendaji, sio baridi; jasiri, haiogopi; iliyozuiliwa, isiyo na ziada; sio jivuna, isiyo jiongezea; na mzuri, isiyo na ujeuri. Mtu mnyenyekevu hakasiriki kirahisi, hajidai, au sio dhalimu na haraka hukubali mafanikio ya wengine.

Kwa kuwa unyenyekevu kwa kawaida unaonesha utegemezi kwa Mungu na daima kuhitaji mwongozo Wake na msaada, tabia inayotofautisha unyenyekevu ni usikivu maalumu wa kiroho kujifunza vyote kutoka Roho Mtakatifu na kutoka watu ambao wataonekana wenye uwezo mdogo, wenye uzoefu, au vinginevyo wale wasioonekana kuwa na mchango mkubwa. Kumbuka jinsi Naamani, kapteni wa jeshi la mfalme wa Shamu, alishinda kiburi chake na kwa unyenyekevu alikubali ushauri wa watumishi wake kumtii nabii Elisha na kujiosha katika mto Yordani mara saba.14 Unyenyekevu ni kanuni ya ulinzi kutoka upofu wa kuwa na kiburi ambao mara nyingi unajitokeza kutoka umaarufu, nafasi, uwezo, utajiri, na sifa za uongo.

Unyenyekevu—Tabia ya kama Kkristo na Karama ya Kiroho

Unyenyekevu ni tabia iliyojengwa kutoka tamaa, matumizi ya kiadilifu ya utashi wa uhuru wa kuchagua, na kujitahidi siku zote kubakiza ondoleo la dhambi zetu.15 Pia ni karama ya kiroho ambayo tunafaa kuitafuta.16 Hatuna budi kukumbuka, hata hivyo, azma ambazo baraka kama hizo zinatolewa, hata kwa kuwanufaisha na kuokoa watoto wa Mungu.17

Tunapokuja kwa na kumfuata Mwokozi, tunawezeshwa kwa nyongeza na kwa faida kuwa zaidi kama Yeye. Tumewezeshwa na Roho pamoja na nidhamu ya kujizuia na suluhisho na kujitweza kwa upole. Vivi hivi, unyenyekevu ni kile kinatufanya tuwe kama wanafunzi wa Bwana na sio tu kitu fulani tunachofanya.

Musa “alikuwa msomi katika hekima zote za Wamisri, na alikuwa uwezo mkubwa katika maneno na katika matendo.”18 Bado, “alikuwa mnyenyekevu sana, zaidi ya wanaume wote ambao walikuwa juu ya uso wa dunia.”19 Maarifa yake na uwezo vingeweza kusababisha awe mwenye kiburi. Badala yake, tabia na karama ya Kiroho ya unyenyekevu ambavyo alikuwa amebarikiwa navyo vilipunguza ufidhuli katika maisha yake na vilimtukuza Musa kama chombo cha kukamilisha azma za Mungu.

Bwana kama Mfano wa Unyenyekevu

Mifano ya adhimu sana na yenye maana ya unyenyekevu inapatikana katika maisha ya Mwokozi Mwenyewe.

Mkombozi Mkuu, aliye “alishuka chini ya vitu vyote”20 na aliteseka, kuvuja damu, na alikufa “kutusafisha na udhalimu wote,”21 kwa wema aliosha miguu yenye vumbi ya wafuasi Wake.22 Unyenyekevu kama ule ni sifa bainifu ya Bwana kama mtumishi na kiongozi.

Yesu anatoa hitimisho la mfano wa mwitikio adilifu na utayari wa kujitoa kama alivyoteseka maumivu makali katika Gethsemane.

“Alipofika mahali pale aliwaambia [wafuasi Wake], Ombeni kwamba msiingie majaribuni.

“Mwenyewe … Akapiga magoti, akaomba,

“Akisema, Ee Baba, ikiwa ni mapenzi yako, uniondolee kikombe hiki: walakini si mapenzi yangu, bali yako yatendeke.”23

Unyenyekevu wa Mwokozi katika uzoefu huu muhimu wa milele wenye maumivu makali unaonesha kwa kila mmoja wetu umuhimu wa kuweka hekima ya Mungu juu ya hekima zetu.

Uendelevu wa kujitoa kwa hiari kwa Bwana na kijizuia kwa nguvu ni vyote heshima inayovutia na kufundisha kwa ajili yetu wote. Wakati kombania yenye silaha ya walinzi wa hekalu na askari wa Kirumi walipowasili Gethsemane kumshika na kumtia na kumtia mbaroni Yesu, Petro aliufuta upanga na kulikata sikio la kulia la mtumishi wa kuhani mkuu.24 Mwokozi ndipo alipogusa sikio la mtumishi na kumponya.25 Tafadhali ona kwamba alinyoosha mkono wake na kumbariki ambaye angekuwa mtekaji wake kwa kutumia uwezo uleule wa kimbinguni ambao ungeweza kumzuia Yeye asitekwe na kusulibiwa.

Fikiria pia jinsi Bwana alivyoshitakiwa na kutiwa hatiani mbele ya Pilato asulibiwe.26 Yesu alikwisha tangaza wakati wa kusalitiwa “Ama wadhani ya kuwa mimi siwezi kumsihi Baba yangu, naye ataniletea sasa hivi zaidi ya majeshi kumi na mawili ya malaika?”27 Bado, “Mwamuzi wa Milele wa wanaoishi na waliokufa”28 kikweli kinzani alihukumiwa mbele ya mteuliwa wa kisiasa wa muda. “Asimjibu [Yesu] hata neno moja, hata liwali akastaajabu sana.”29 Unyenyekevu wa Mwokozi unashuhudiwa katika jibu lake lenye nidhamu, kujizuia kwa nguvu, na kutokuwa tayari kutumia uwezo Wake usio na mwisho kwa manufaa yake binafsi.

Ahadi na Ushuhuda

Mormoni anatambua unyenyekevu kama msingi ambao kutoka kwake uwezo wote wa Kiroho na karama hutokea.

“Kwa hivyo, ikiwa mtu ana imani lazima ahitaji kuwa na tumaini; kwani bila imani hakuwezi kuwepo na tumaini lolote.

“Na tena, tazama ninawaambia kwamba hawezi kuwa na imani na tumaini, isipokuwa awe mnyenyekevu, na mpole katika moyo.

Ikiwa hivyo, imani na tumaini lake ni bure, kwani hakuna yeyote anayekubaliwa mbele ya Mungu, isipokuwa yule aliye myenyekevu na mpole katika moyo; na mtu akiwa myenyekevu na mpole katika moyo, na kukiri kwa uwezo wa Roho Mtakatifu kwamba Yesu ni Kristo, lazima awe na hisani; kwani kama hana hisani yeye si kitu; kwa hivyo lazima awe na hisani.”30

Mwokozi alitangaza, “Heri wenye upole; Maana hao watairithi nchi.”31 Unyenyekevu ni kipengele muhimu cha asili takatifu na unaweza kupokelewa na kukuzwa katika maisha yetu kwa sababu ya na kupitia kwa Upatanisho wa Mwokozi.

Ninashuhudia kwamba Yesu Kristo ni Mkombozi aliyefufuka na anaishi. Na ninaahidi kwamba ataongoza, kulinda, na kutuimarisha tunapotembea katika unyenyekevu wa roho Yake. Ninatangaza ushahidi wangu wa uhakika wa kweli hizi katika jina takatifu la Bwana Yesu Kristo, amina.