2010–2019
Siku Moja Zaidi.
Aprili 2018


Siku Moja Zaidi.

Sote tunayo leo ya kuishi na ufunguo wa kuifanya siku yetu kuwa ya mafanikio ni kwa kuwa radhi kutoa dhabihu.

Miaka michache iliyopita, rafiki yangu alikuwa na mtoto mzuri aitwaye Brigham. Baada ya kuzaliwa kwake, Brigham alipatikana na hali ambayo mara chache hutokea iitwayo Hunter syndrome, ambayo ilimaanisha Brigham angekuwa na maisha mafupi. Siku moja Brigham na familia yake walitembelea bustani ya hekalu, Brigham alisema kirai maalum; mara mbili alisema, “Siku moja zaidi.” Siku iliyofuata, Brigham alifariki.

Picha
Brigham
Picha
Familia ya Brigham
Picha
Kaburi ya Brigham

Nimetembelea kaburi la Brigham mara kadhaa, na kila mara nifanyapo hivyo, hutafakari kirai “siku moja zaidi.” Ninashangaa nini kilimaanisha, ni athari gani kingekuwa nayo kwenye maisha yangu kujua kwamba ningekuwa na siku moja tu ya kuishi. Ningemchukulia kwa namna gani mke wangu, watoto wangu, na wengine? Ningekuwa mvumilivu na mpole kiasi gani? Ningeuchukulia kwa namna gani mwili wangu? Ni kwa dhati kiasi gani ningesali na kusoma maandiko? Nafikiri hiyo ni njia mojawapo au nyingine sote katika wakati fulani tutakuwa na utambuzi wa “siku moja zaidi”—utambuzi kwamba lazima tutumie muda tulionao kwa busara.

Katika Agano la Kale tunasoma kuhusu hadithi ya Hezekia, mfalme wa Yuda. Nabii Isaya alimtangazia Hezekia kwamba maisha ya Hezekia yako karibu kuisha. Wakati aliposikia maneno ya nabii, Hezekia akaanza kusali, kuomba, na kulia kwa uchungu. Katika wakati huo, Mungu aliongeza miaka 15 katika maisha ya Hezekia. (Ona Isaya 38:1–5.)

Kama tukiambiwa kuwa tuna maisha mafupi ya kuishi, nasi pia tunaweza kuomba kwa ajili ya siku zaidi za maisha katika ajili ya yale ambayo tulitakiwa kuyatenda au tumetenda au tumetenda tofauti.

Bila kujali muda Bwana, katika hekima Yake, anapanga kumpa kila mmoja wetu, kitu kimoja ambacho tunaweza kuwa na uhakika: sisi sote tuna “leo” ya kuishi, na funguo ya kufanya siku yetu kuwa ya mafanikio ni kwa kuwa tayari kujitolea.

Bwana alisema “Tazama, sasa inaitwa leo hadi kuja kwa Mwana wa Mtu, na hakika ni siku ya kujitoa dhabihu (M&M 64:23; mkazo umeongezwa).

Neno dhabihu linatokana na neno la Kilatini sacer, ambalo humaanisha “takatifu,” na facere, ambalo humaanisha “kufanya,” kwa maneno mengine kufanya vitu kuwa vitakatifu, kuvipa heshima.

“Dhabihu huleta baraka za mbinguni” (“Praise to the Man,” wimbo, namba. 27).

Ni kwa njia zipi dhabihu itafanya siku zetu kuwa za maana na kubarikiwa?

Kwanza, dhabihu binafsi hutuimarisha na kutupa thamani katika vitu tunavyojitolea.

Miaka kadhaa iliyopita katika jumapili ya mfungo, dada wa makamo tusiyemjua alikuja kwenye mimbari na kushiriki ushuhuda wake. Alituambia kwamba aliishi kwenye jiji liitwalo Iquitos, ambalo ni Peruvian Amazon. Alituambia kwamba tangu kipindi cha ubatizo wake, alikuwa na lengo la kupokea ibada za hekaluni katika hekalu la Lima, Peru. Kwa uaminifu alilipa zaka yake kamili na kuweka akiba kipato chake kidogo kwa miaka.

Shangwe yake ya kwenda hekaluni na kupokea ibada takatifu ilielezewa katika maneno haya: Leo ninaweza kusema kwamba mwishowe ninahisi utayari wa kwenda kupita pazia kulingana na mapenzi ya Mungu. Mimi ni mwanamke mwenye furaha sana duniani; nimeweka akiba fedha, hamwezi kuelewa ni kwa kipindi cha muda gani, kwenda hekaluni, na baada ya siku 7 mtoni na saa 18 kwa basi, mwishowe nilifika katika nyumba ya Bwana. Wakati wa kuondoka sehemu ile takatifu, nilijisemea nafsini mwangu, baada ya dhabihu yote ambayo ilihitajika kwangu ili kuja hekaluni, sitaacha chochote kinifanye nichukulie kiurahisi maagano niliyofanya; ingekuwa ni upotevu. Huku ni kujitolea kwa kweli!”

Nilijifunza kutoka kwa dada huyu mpendwa kwamba dhabihu binafsi ni nguvu ambayo haipimiki ambayo hutusukuma katika chaguzi na utayari wetu. Dhabihu binafsi husukuma matendo yetu, kujitolea kwetu na maagano hutoa maana katika vitu vitakatifu.

Pili, dhabihu tunayotoa kwa ajili ya wengine, na ambayo wengine hutoa kwa ajili yetu, huleta baraka kwa wote.

Wakati nikiwa mwanafunzi katika shule ya utaalamu wa meno, muonekano wa kifedha wa uchumi wetu haukuwa wa kuhamasisha. Mfumko wa bei kwa kasi ulipunguza thamani ya fedha kutoka siku moja hadi nyingine.

Nakumbuka mwaka ambao nilitakiwa kujisajili kwenye mafunzo ya upasuaji; nilihitajika kuwa na kila kifaa cha upasuaji kabla ya kusajiliwa muhula huo. Wazazi wangu waliweka akiba fedha iliyohitajika. Lakini usiku mmoja kitu cha ajabu kilitokea. Tulikwenda kununua kifaa, ndipo tukagundua kwamba kiasi cha fedha ambacho wazazi wangu waliweka akiba kwa ajili ya kununulia vifaa sasa kilikuwa kinatosha tu kununua koleo—na si chochote zaidi. Tulirudi nyumbani mikono mitupu na mioyo mizito kwa wazo la kupoteza muhula chuoni. Ghafla, hata hivyo, mama yangu alisema, Taylor, njoo pamoja nami; twende nje.”

Tulikwenda mjini ambapo kuna sehemu nyingi za kuuza na kununua vito vya thamani. Tulipofika katika duka moja, mama yangu alitoa kenye pochi yake begi dogo la mahameli lililokuwa na bangili nzuri ya dhahabu ikiwa na maneno yaliyosomeka “Kwa binti yangu mpendwa toka kwa baba yako.” Ilikuwa ni bangili ambayo babu yangu alimpa mama katika moja ya siku yake ya kuzaliwa. Kisha, mbele ya macho yangu, aliiuza.

Alipopokea fedha, aliniambia “Kama kuna kitu kimoja ambacho nina uhakika nacho, ni kwamba unaenda kuwa daktari wa meno. Nenda na kanunue vifaa vyote unavyohitaji. Sasa, unaweza kufikiria ni aina gani ya mwanafunzi nilikuwa toka wakati huo? Nilitaka kuwa bora sana na kumaliza masomo yangu mapema kwa sababu nilijua thamani kubwa ya dhabihu aliyokuwa akiitoa.

Nilijifunza kwamba dhabihu ambazo wapendwa wetu huzitoa kw ajili yetu hutuchangamsha kama maji baridi katikati mwa jangwa. Dabihu ya namna hiyo huleta tumaini na hamasa.

Tatu, dhabihu yoyote tunayotoa ni ndogo ikilinganishwa na dhabihu ya Mwana wa Mungu.

Ni thamani kiasi gani hata kama ni bangili pendwa ya dhahabu ikilinganishwa na dhabihu ya Mwana wa Mungu? Ni kwa vipi tuaweza kuiheshimu dhabihu hii isiyo na mwisho? Kila siku tunaweza kukumbuka kwamba tuna siku moja zaidi ya kuishi na kuwa waaminifu. Amuleki alifundisha: “Ndio, ningependa kwamba mje mbele na msishupaze mioyo yenu mara nyingine; kwani tazama, sasa ndio wakati na siku ya wokovu wenu; na kwa hivyo ikiwa mtatubu, na msishupaze mioyo yenu, mara moja mpango mkuu wa ukombozi utatimizwa kwenu” (Alma 34: 31). Kwa maneno mengine, kama tutatoa kwa Bwana dhabihu ya moyo uliovunjika na roho iliyopondeka, mara moja baraka za mpango mkuu wa furaha zitadhihirika maishani mwetu.

Mpango wa ukombozi unawezekana shukrani kwa dhabihu ya Yesu Kristo. Kama vile yeye Mwenyewe alivyoeleza, dhabihu ambayo “iliyosababisha Mimi mwenyewe, hata Mungu, mkuu kuliko yote, kutetemeka kwa sababu ya maumivu, na kutoka damu kwenye kila kinyweleo, na kuteseka mwili na roho—na kutamani nisinywe kikombe kichungu, na kusita” (M&M 19:18).

Na ni kwa sababu ya dhabihu hii, baada ya kufuata mchakato wa toba ya dhati, kwamba tunaweza kuhisi uzito wa makosa na dhambi zetu ukiinuliwa. Kiukweli, hatia, aibu, maumivu, na huzuni na kujiona duni kwetu vinachuliwa nafasi na dhamira safi, furaha, shangwe na tumaini.

Kwa wakati huohuo, tunapoheshimu na kuwa na shukrani kwa dhabihu Yake, tunaweza kupokea kwa kiwango kikubwa cha hamu ya kuwa watoto wazuri zaidi wa Mungu, kukaa mbali na dhambi, na kuishi maagano kuliko hapo awali.

Kisha, kama Enoshi baada ya kupokea msamaha wa dhambi zake, tutahisi hamu ya kujitoa dhabihu na kutafuta ustawi wa kaka zetu na dada zetu (ona Enoshi 1:9). Na tutakuwa tayari zaidi kila “siku moja zaidi” kufuata mwaliko wa Rais Howard W. Hunter uliotolewa kwetu aliposema: “Sahihisha ugomvi Matafute rafiki aliyesaulika. Futilia mbali tuhuma na uaminifu uchukue nafasi yake. Toa jibu laini. Himiza vijana Dhihirisha uaminifu wako kwa maneno na vitendo. Timiza ahadi. Sahau kinyongo. Msamehe adui. Omba radhi. Jaribu kuelewa. Chunguza matakwa yako kwa wengine Fikiria kwanza kuhusu mtu mwingine. Kuwa mkarimu. Kuwa mpole. Cheka kidogo. Elezea shukrani zako. Mkaribishe mgeni. Furahisha moyo wa mtoto. … Ongea kuhusu upendo wako na ongea tena” (Teachings of Presidents of the Church: Howard W. Hunter [2015], 32; imetoholewa kutoka kwa “What We Think Christmas Is,” McCall’s, Dec. 1959, 82–83).

Na tujaze siku zetu kwa msukumo huo utolewao na nguvu ya dhabihu binafsi na dhabihu tunazotoa au kupokea toka kwa wengine . Na katika njia maalum, tufurahie amani na shangwe kwamba dhabihu ya Mwana Pekee anayotoa kwetu; ndio, amani hiyo ambayo imetajwa wakati tukisoma kwamba Adamu alianguka ili wanadamu wawe, na wanadamu wapo—wewe mmoja wapo— kwamba uwe na shangwe (ona 2 Nefi 2:25). Shangwe hiyo hakika ni shangwe ambayo inaweza kutolewa na dhabihu pekee na Upatanisho wa Mwokozi Yesu Kristo.

Ni sala yangu kwamba tumfuate Yeye, kwamba tumwamini Yeye, kwamba tumpende Yeye, na kwamba tuhisi upendo uliodhihirishwa kupitia dhabihu Yake kila mara tunapokuwa na fursa ya kuishi siku moja zaidi. Katika jina la Yesu Kristo, amina