2010–2019
Kutumikia kwa Uwezo na Mamlaka ya Mungu
Aprili 2018


Kuhudumu kwa Uwezo na Mamlaka ya Mungu

Tutahudumu katika jina Lake, pamoja na nguvu na mamlaka Yake, na pamoja na huruma wa upendo Wake.

Wapendwa ndugu zangu, asanteni kwa ibada zenu kwa Mungu na kazi yake takatifu. Kwa kweli ni furaha kuwa pamoja nanyi. Kama Urais mpya wa Kwanza, tunawashukuruni kwa sala zenu na juhudi zenu za kutuidhinisha. Tunawashukuru kwa maisha yenu na kwa huduma zenu kwa Bwana. Bidii yenu kwenye kazi na huduma yenu zisizo na uchoyo ni zilizomuhimu katika wito wenu kama zetu zilivyo katika wito wetu. Kupitia kwa huduma ya maisha katika kanisa hili, nimejifunza kwamba kwa kweli haijalishi ni wapi unapohudumia. Kile ambacho Bwana anajali kuhusu zaidi jinsi unavyohudumu.

Ninatoa shukrani ya dhati kwa Rais Thomas S, Monson, ambaye alikuwa mfano kwangu kwa zaidi ya miaka 50. Na kwa washauri wake, Rais Henry B. Eyring na Rais Dieter F. Uchtdorf, ninatoa upendo wa kina. Ninawasifu kwa huduma yao kwa Bwana na Manabii Wake. Wote hawa watumishi waliojitolea wamepokea uteuzi mpya. Wanaendelea kutumikia na nguvu na kujitolea. Ninawaheshimu na kuwapenda wote.

Ni baraka ya ajabu kuhudumia katika Kanisa la kweli linaloishi la Bwana lenye mamlaka na uwezo Wake. Urejesho wa ukuhani wa Mungu, pamoja na funguo za ukuhani, zinafungua kwa Watakatifu wa Siku za Mwisho wanaostahili baraka kubwa mno kati ya zote za kiroho. Tunaziona baraka hizo zikitiririka kwa wanawake, wanaume, na watoto ulimwenguni kote.

Tunawaona wanawakee waaminifu wanapelewa uwezo wa asili katika wito wao na katika endaumenti zao na ibada zingine za hekaluni Wanawake hawa wanajua jinsi ya kuziita nguvu za mbinguni kuwalinda na kuwaimarisha waume wao, watoto wao, na wengine wanaowapenda. Hawa ni wanawake imara kiroho wanaoongoza, kufundisha, na kuhudumia bila hofu katika miito yao kwa nguvu na mamlaka ya Mungu!1 Ni shukrani iliyoje niliyo nayo kwa ajili yao!

Kadhalika, tunawaona wanaume waaminifu wanaoishi kulingana na heshima zao kama wenye ukuhani. Wanaongoza na kuhudumu kwa kujitoa dhabihu, katika njia ya Bwana kwa upendo, upole, na utulivu. Wanabariki, wanaongoza, wanalinda, na kuwaimarisha wengine kwa uwezo wa ukuhani walio nao. Wanaleta miujiza kwa wale wanaowahudumia wakati wanaweka ndoa zao na familia salama. Wanaepukana na uovu na ni wazee wenye nguvu katika Israeli.2 Nina shukrani kubwa kwa ajili yao!

Sasa, wacha niseme hofu yangu? Ni hii: wengi sana wa ndugu zetu na dada zetu hawaelewi kikamilifu dhana ya nguvu na mamlaka ya ukuhani. Wanatenda kama angalau tu wangeridhisha tamaa zao za ubinafsi na hamu kuliko kutumia nguvu za Mungu kubariki Watoto Wake.

Ninaogopa kwamba wengi wa ndugu zetu na dada ng’amui heshima ambazo zingeweza kuwa zao.3 Baadhi ya ndugu zetu, kwa mfano, wanafanya kama hawaelewi ukuhani ni nini na nini unawawezesha kufanya. Wacha niwapeni baadhi ya mifano dhahiri.

Sio muda mrefu uliopita, nilihudhuria mkutano wa sakramenti ambao mtoto mchanga alikuwa apewe jina na baraka za baba. Baba kijana alimbeba mtoto wake kipenzi mikononi mwake, akampa jina, na kisha akatoa sala mzuri. Lakini hakumpa mtoto yule baraka. Mtoto yule mzuri wa kike alipata jina lakini bila baraka! Yule mzee mpendwa hakujua tofauti kati ya sala na baraka za ukuhani. Kwa mamlaka na nguvu za ukuhani wake, angeweza kumbariki mtoto wake mchanga, lakini hakufanya hivyo. Nikafikiria, “Nafasi iliyoje iliyopotea!

Wacha nitaje baadhi ya mifano mingine. Tunawajua ndugu waliowasimika akina dada kama viongozi wa darasa la msingi, wasichana, au Muungano wa Usaidizi wa Akina Mama na waalimu lakini wakashindwa kuwabariki na uwezo kukamilisha wito wao. Wanatoa tu maonyo na maelekezo. Tunamwona baba mwenye kustahili anaeshindwa kumpa mke wake na watoto wake baraka za ukuhani wakati hicho ndicho haswa wanachokihitaji. Nguvu ya ukuhani zimerejeshwa kwenye dunia hii, na bado ndugu wengi sana na akina dada wanapitia majaribu ya kutisha maishani bila hata kupokea baraka za ukuhani za kweli. Ni janga liliyoje! Hilo ni janga ambalo tunaweza kuliondoa.

Ndugu, tunao ukuhani mtakatifu wa Mungu! Tunayo mamlaka yake ya kubariki watu Wake. Ebu fikiri juu ya ajabu ya ahadi Bwana aliyotupa wakati aliposema, “Yoyote yule mtakayembariki nitambariki.”4 Ni heshima yetu kufanya katika jina la Yesu Kristo kubariki watoto wa Mungu kufuatana na mapenzi Yake kwa ajili yao. Marais wa vigingi na maaskofu, tafadhali hakikisheni kwamba kila mshiriki wa akidi katika uangilizi wenu anaelewa jinsi ya kutoa baraka za ukuhani—pamoja na ustahili binafsi na matayarisho ya kiroho yanayohitajika kuomba nguvu za Mungu.5

Kwa ndugu wote walio na ukuhani, ninawasihi kuwavutia waumini kuweka maagano yao, kufunga na kusali, kujifunza maandiko, kuabudu katika hekalu, na kuhudumu kwa imani kama wanaume na wanawake wa Mungu. Tunaweza kuwasaidia wote kuona kwa jicho la imani kwamba utii na uadilifu vitawavuta karibu sana kwa Yesu Kristo, kuwaruhusu kufurahia wenza wa Roho Mtakatifu, na kupata uzoefu wa furaha katika maisha!

Sifa bainifu ya Kanisa la kweli na linaloishi la Bwana siku zote litakuwa lenye utaratibu, juhudi zilizoelekwezwa kuwahudumia watoto binafsi wa Mungu na familia zao.6 Kwa sababu ni Kanisa lake, sisi kama watumishi Wake tutahudumia kwa mmoja, kama alivyofanya.7 Tutahudumu katika jina Lake, pamoja na nguvu Zake na mamlaka, na pamoja na huruma Zake za upendo.

Uzoefu niliokuwa nao zaidi ya miaka 60 iliyopita huko Boston ulinifundisha jinsi ilivyo na nguvu heshima ya kuhudumia mmoja mmoja inavyowezekana. Nilikuwa wakati huo daktari mpasuaji mkazi kwenye Hospitali Kuu ya Massachusetts—nikiwa kazini kila siku, kila baada ya usiku mmoja, na kila baada ya mwisho wa wiki moja. Nilikuwa na muda mchache kwa ajili ya mke wangu, watoto wetu wanne, na shughuli za Kanisa. Hata hivyo, rais wetu wa tawi alinipangia kutembelea nyumba ya Wilbur na Leonora Cox kwa matumaini kwamba Kaka Cox anaweza kurudi katika shughuli kwenye Kanisa. Yeye na Leonora walikuwa wameunganishwa katika hekalu.8 Bado, Wilbur hajashiriki kwa miaka mingi.

Mwenza wangu namii tulikwenda nyumbani kwao. Tulipoingia, Dada Cox alitukaribisha kwa moyo mkujufu,9 lakini Kaka Cox mara moja aliingia katika chumba kingine na akafunga mlango.

Nilienda kwenye mlango uliofungwa na kugonga. Baada ya muda mfupi, Nilisikia “ingia” ya kunong’ona. Nilifungua mlango na kumkuta Kaka Cox amekaa pembeni mwa mpangilio wa vifaa vya redio usio wa ustadi. Katika hicho chumba kidogo, aliwasha sigaa. Kwa uwazi, ziara yangu haikuwa ya makaribisho.

Niliangalia kwa makini kuzunguka chumba kwa mshangao na kusema,” kaka Cox, siku zote nimekuwa nataka kujifunza zaidi kuhusu kazi isiyo ya ustadi ya redio. Je, utakuwa tayari kunifundisha kuhusu kazi hiyo? Nasikitika siwezi kukaa kwa muda mrefu usiku wa leo, lakini naweza kurudi muda mwingine?”

Alisita kwa muda na kisha akasema ndiyo. Ule ulikuwa mwanzo wa kile kilichokuwa urafiki wa ajabu. Nilirudi na alinifundisha. Nilianza kumpenda na kumheshimu. Katika ziara zetu zilizofuatia, ukuu wa mtu huyu ulijitokeza. Tukawa marafiki wakubwa sana, kama walivyokuwa wenza wetu wapendwa wa milele. Kisha, baada ya kupita kwa muda, familia yetu iliondoka. Viongozi wa pale waliendelea kuelimisha familia ya Cox,10

Takribani miaka minane baada ya ziara ile ya kwanza, Kigingi cha Boston kilianzishwa.11 Unaweza kukisia rais wa kigingi hicho alikuwa nani? Ndiyo! Kaka Cox! Wakati wa miaka iliyoendelea, alihudumu pia kama rais wa misheni na rais wa hekalu.

Miaka mingi baadaye, kama mshiriki wa Akidi ya wale Kumi na Wawili, Nilipangiwa kuanzisha kigingi kipya katika Sanpete wilaya, ya Utah. Wakati wa usahili wa kawaida, kwa furaha nilishangazwa kukutana na tena na rafiki yangu kipenzi Kaka Cox! Nilihisi kuvutiwa kumwita kama baba mkuu wa kigingi kipya. Baada ya kumtawaza, tulikumbatiana na tulilia. Watu katika chumba walikuwa wanashangaa kwa nini hawa wamaume wazima wawili walikuwa wanalia. Lakini tulilia. Na dada Cox alijua. Yetu yalikuwa machozi ya furaha! Kimya kimya tulikumbuka safari ya ajabu ya upendo na toba ambayo ilianza zaidi ya miaka 30 iliyopita, usiku mmoja katika nyumba yake.

Maelezo hayaishii hapo. Familia ya Kaka na Dada Cox ilikua na kuwa na watoto 3, wajukuu 20, na vitukuu 54. Ongeza kwa hilo athari yao kwa mamia ya wamisionari, kwa maelfu zaidi katika hekalu, na kwa mamia zaidi ambao walipokea baraka za baba mkuu mikononi mwa Wilbur Cox. Ushawishi wake na wa Leonora utaendelea kupiga mawimbi kupitia vizazi vingi ulimwenguni kote.

Uzoefu kama huu wa Wilbur na Leonora Cox unatokea kila wiki—kwa matumaini, kila siku—ndani ya Kanisa hili. Watumishi waliojitolea kwa dhati wa Bwana Yesu Kristo wanafanya kazi Yake, kwa nguvu na mamlaka Yake.

Ndugu, kuna milango tunayoweza kufungua, baraka za ukuhani tunazoweza kutoa, mioyo tunayoweza kuponya, mizigo tunayoweza kuinua, shuhuda tunazoweza kuimarisha, maisha tunayoweza kuokoa, na furaha tunayoweza kuleta katika nyumba za Watakatifu wa Siku za Mwisho—vyote kwa sababu tuna ukuhani wa Mungu. Sisi ni wanaume ambao “tumeitwa na kutayarishwa kutoka kwenye msingi wa ulimwengu kufuatana na kujua kabla kwa Mungu, kwa maelezo ya imani [yetu] iliyozidi,” kufanya kazi hii.12

Usiku huu ninawaomba kwa uwazi tusimame pamoja katika undugu wetu mkuu wa milele. Nitapotaja jina la ofisi ya ukuhani wako, tafadhali simama na ubaki umesimama. Mashemasi tafadhali simameni! Walimu, simameni Makuhani! Maaskofu! Wazee! Makuhani Wakuu! Mababa Wakuu! Sabini! Mitume!

Sasa, ndugu, tafadhali mbaki mmesimama na jiungeni pamoja na kwaya katika kuimba aya zote tatu za “Rise Up, O Men of God”?13 Wakati mnaimba, fikirieni kazi yenu kama jeshi lenye nguvu la Mungu kusaidia kutayarisha ulimwengu kwa ajili ya Ujio wa Pili wa Bwana. Hiyo ndio kazi yetu. Hiyo ndio heshima yetu. Mimi nashuhudia hivyo kwa jina la Yesu Kristo, amina.