2010–2019
Ripoti ya Idara ya Ukaguzi ya Kanisa, 2017
Aprili 2018


Ripoti ya Idara ya Ukaguzi ya Kanisa, 2017

Kwa Urais wa Kwanza wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho

Ndugu Wapendwa: Kama tulivyoelekezwa na ufunuo katika sehemu ya 120 ya Mafundisho na Maagano, Baraza la Mpangilio wa Zaka, linalojumuisha Urais wa Kwanza, Akidi ya Mitume Kumi na Wawili, na Uaskofu Simamizi—huidhinisha matumizi ya fedha za Kanisa. Mashirika ya Kanisa hugawa fedha kwa mujibu wa bajeti iliyoidhinishwa, sera, na taratibu.

Idara ya Ukaguzi ya Kanisa, inayojumuisha wataalamu walioidhinishwa na ni huru kutokana na idara zingine zote za Kanisa, ina wajibu wa kufanya ukaguzi kwa lengo la kutoa uhakika kuhusu michango iliyopokelewa, matumizi yaliyofanywa, na ulinzi wa mali ya Kanisa.

Kulingana na ukaguzi uliofanywa, Idara ya Ukaguzi ya Kanisa inatoa maoni kwamba, katika mambo yote muhimu, michango iliyopokelewa, matumizi yaliyofanywa, na mali ya Kanisa kwa mwaka 2017 vimerekodiwa na kusimamiwa kwa mujibu wa bajeti iliyoidhinishwa na Kanisa, sera, na utendaji wa uhasibu. Kanisa linafuata utendaji uliofundishwa kwa waumini wake wa kuishi katika mipaka ya bajeti, kuepuka madeni, na kuweka akiba kwa ajili ya wakati wa shida.

Kwa heshima imewasilishwa,

Idara ya Ukaguzi ya Kanisa

Kevin R. Jergensen

Mkurugenzi Mkuu