2010–2019
“Kuwa Nao na Kuwaimarisha”
Aprili 2018


“Kuwa Nao na Kuwaimarisha”

Sala yetu leo ni kwamba kila mwanaume na mwanamke ataondoka katika mkutano huu na msimamo wa kina wa kujaliana kwa moyo wa dhati.

Kufafanua maneno ya Ralph Waldo Emerson, nyakati za kukumbukwa sana katika maisha ni zile tunazohisi mfulululizo wa ufunuo.1 Rais Nelson, Mimi sijui ni “mifululizo” mingi kiasi gani tumaweza kustamili wikiendi hii. Baadhi yetu tuna mioyo dhaifu. Lakini ninapofikiria hilo, mnaweza kustamili hilo pia. Ni nabii kweli!

Katika roho ya ushuhuda na matangazo ya ajabu ya Rais Nelson usiku wa jana na asubuhi hii, ninatoa ushahidi wangu kwamba marekebisho haya ni mifano ya ufunuo ambao unaogoza Kanisa hili kutoka mwazno wake. Bado kuna ushahidi zaidi kwamba Bwana anaharakisha kazi Yake katika wakati wake.2

Kwa wale wote ambao wana hamu ya kujifunza utondoti wa mambo haya, tafadhali jueni kwamba punde baada tamati ya kikao hiki cha mkutano mkuu, utaratibu utaanza ambao unajumuisha, sio tu mpango huu, kutumwa kwa barua kutoka kwa Urais wa Kwanza hadi kwa kila muumini wa Kanisa ambaye tuna barua pepe yake. Hati ya kurasa saba ya maswali na majibu zitaambatishwa kwa viongozi wote wa ukuhani na makundi saidizi. Mwisho, vifaa hivi vitawekwa katika ministering.lds.org. “Ombeni, nanyi mtapewa tafuteni, nanyi mtaona.”3

Sasa kazi ya ajabu ambayo Rais Russell M. Nelson ametupatia mimi na Dada Jean B. Bingham. Kina kaka na kina dada, jinsi kazi ya akidi na makundi saidizi inakomaa kitaasisi, inafuata kwamba tunapaswa kibinafsi tukomae—kibinafsi tusimame zaidi ya hali yoyote ya kimashini, kazi-bila-hisia isiyobadilika katika uanafunzi wa dhati ulioelezewa na Mwokozi wakati wa kumalizika kwa huduma Yake duniani. Wakati akijiandaa kuliacha kundi Lake dogo la wasio kuwa na hatia na kwa kiasi fulani waliokuwa wamechanganywa, hakuorodhesha dazeni za hatua za maongozi walizotakiwa kufuata au kuwapa kifungu cha ripoti zilizohitajika kujazwa katika nakala tatu. Hapana, alitoa muhtasari wa kazi yao katika amri moja muhimu: “Mpendane, kama mimi nilivyowapenda nyinyi … “Hivyo watu wote watatambua ya kuwa ninyi mmekuwa wanafunzi wangu, mkiwa na upendo ninyi kwa ninyi.”4

Katika juhudi za kutusogeza katika wazo hilo la injili, dhana hii mpya ya kuhudumu kwenye ukuhani na Muungano wa Usaidizi wa Akina Mama itajumuisha miongoni mwa vitu vingine vipengele vifuatavyo, ambavyo baadhi yake Muungano wa Usaidizi wa Akina Mama tayari umeshafanyia kazi kwa mafanikio ya kupendeza.5

  • Hatutatumia tena lugha ya ufundishaji wa nyumbani nyumbani na ualimu wa kutembeleana Hii ni kwa sababu juhudi zetu nyingi za kuhudumu zitakuwa kwa mazingira mengine tofauti na nyumbani na kwa sababu kwa sehemu mawasiliano yetu hayatatambulika kwa kufundisha somo lililoandaliwa, ingawa somo hakika linaweza kutolewa kama kutakuwa na hitaji katika hilo. Dhumuni la msingi la dhana hii ya kuhudumu litakuwa, kama ilivyosemwa na watu wakati wa Alma, “kuwalinda watu wao, na … kuwalisha vitu vilivyohusu utakatifu.”6

  • Tutaendelea kutembelea nyumba kama ikiwezekana, lakini hali za sehemu husika kama vile idadi kubwa, umbali, usalama binafsi na changamaoto katika hali zingine vinaweza kuzuia utembeleaji wa nyumbani kila mwezi. Kama Urais wa Kwanza ulivyoshauri miaka iliyopita, fanya uwezavyo.7 Katika nyongeza ya ratiba ambayo unatengeneza kwa ajili ya utembeleaji, kalenda hiyo inaweza kuongezewa ikiwa na namba za simu, muhtasari ulioandikwa, ujumbe mfupi, barua pepe, maongezi kwa njia ya video, maongezi katika mikutano ya Kanisa, huduma za kushiriki, shughuli za kijamii na uwezekano mwingi katika mitandao ya kijamii. Hata hivyo, lazima nisisitize kwamba hii twasita mpya pana haujumuishi kauli ya kusikitisha niliyoiona kwenye karatasi iliyopbandikwa kwenye gari. Inasomeka, “Kama nikikupiga honi, umeshafundishwa.” Tafadhali, tafadhali (kina dada kamwe hawawezi kuwa na hatia ya hilo—mimi naongea na ndugu Kanisani), kwa marekebisho haya tunataka utunzaji zaidi, kujali zaidi, wala si chochote chini ya hivyo.

  • Kwa hii dhana mpya, zaidi za kiinjili za kuhudumu, ninahisi mnaanza kuwa na wasiwasi kuhusu nini kinajumuishwa kwenye ripoti. Basi, tulieni, kwa sababu hakuna ripoti yoyote—angalau si tarehe 31 ya mwezi “niliweza kuingia mlangoni kwa ngozi ya meno yangu” ripoti. Hapa pia tunajaribu kukomaa. Ripoti pekee ambayo itaandaliwa ni ya idadi ya usahili ambayo viongozi walikuwa nayo na wahudumu wenza katika kata kwa robo hiyo. Rahisi kama inavyonekana, marafiki zangu, hizi sahili ni muhimu kabisa. Bila habari hizo askofu hatakuwa njia yoyote ya kupokea habari anazohitaji kuhusu hali ya kiroho na kimwili ya watu wake. Kumbuka: kaka wahudumu wanamwakilisha uaskofu na urais wa akidi ya wazee; wala wao sio mbadala. Funguo za askofu na rais wa akidi ni zaidi ya hii dhana ya hudumiaji.

  • Kwa sababu ripoti hii ni tofauti sana chochote mlichowasilisha hapo awali, wacha nisisitize kwamba sisi hapa makao makuu ya Kanisa hatuhitaji kujua jinsi au wapi au lini umewasiliana na watu wako; sisi tunahitaji tu kujua na tunajli kwamba utatenda hilo na kwamba utawabariki wao kwa kila njia unayoweza.

Kina kaka na kina dada, sisi tuna fursa ya mbinguni kama Kanisa lote kuonyesha “dini ya kweli … isiyo na mawaa mbele za Mungu”8— “kubeba mziigo wa mmoja na mwingine, ili iew miepesi” na kuwafarij wale walio na mahitaji,”9 kuwahudumia wajane na yatima, walioowa/kuolewa na walio waseja, walio na nguvu na waliofadhaika, waliokanyagwa na walio imara, walio na furaha na walio na huzuni—kwa ufupi, sisi sote, kila mmoja wetu, kwa sababu tunahitaji kuhisi mkono wa urafiki wa upendo na kusikia tangazo dhabiti la imani. Hata hivyo, nawaonya, jina jipya, urahisi mpya, na ripoti chache havitaleta tofauti hata kidogo katika huduma zetu isipokuwa tuone huu kama mwaliko wa kujaliana katika njia mpya ya haki na dhabiti, kama vile Rais Nelson alivyosema. Tuinuapo macho yetu ya kiroho kuelekea kuishi sheria ya upendo kwa upana zaidi, tunaonyesha shukrani kwa vizazi vilivyohudumia kwa namna hiyo kwa miaka mingi. Acha nionyeshe mfano wa hivi karibuni wa kujitolea kwa namna hiyo katika tumaini kwamba majeshi zaidi yatachukua amri ya Bwana kwa “kuwa nao na kuwaimarisha”10 kaka zetu na dada zetu.

Januari iliyopita tarehe 14, Jumapili, muda kidogo baada ya saa 11 jioni, rafiki zangu vijana Brett na Kristin Hambling walikuwa wakizungumza nyumbani kwao huko Tempe, Arizona, baada ya siku ya kazi ya nyingi ya Brett ya kuhudumu katika uaskofu na siku ya kazi nyingi kwa Kristin ya kuhudumia watoto wao watano.

Ghafla Kristin, aliyeonekana kufanikiwa kuishi licha ya saratani ya titi mwaka uliopita, alihisi kutokuwa sawa. Simu kwenda namba 911 iliwaleta timu ya dharura wakijaribu bila tumaini kumrudisha katika hali ya kawaida. Wakati Brett akisali kwa dhati, haraka alipiga simu mbili zingine: moja kwa mama akimuomba msaada wake kuwahudumia watoto, nyingine kwa Edwin Potter, mwalimu wake wa nyumbani. Maongezi mengine katika ukamilifu wake yalikuwa kama ifuatavyo:

Edwin, akiona namba ya utambulisho, alisema, “Brett, habari?”

Jibu la Brett la sauti kubwa lilikuwa “Ninakuhitaji hapa—sasa hivi!”

Ndani ya dakika chache ambazo Brett hakuweza kuhesabu, mwenzake katika ukuhani alikuwa pembeni mwake, akimsaidia watoto na kumwendesha kaka Hamblin hospitalini nyuma ya gari ya wagonjwa iliyombeba mke wake. Hapo, chini ya dakika 40, alikuwa amefumba macho yake, na daktari alitamka kwamba Kristin amefariki.

Wakati Brett akilia, Edwin alimshika tu mikononi mwake na kulia pamoja naye—kwa muda mrefu sana. Kisha, akimwacha Brett kuomboleza na wana familia wengine ambao walikuwa wamekusanyika, Edwin aliendesha gari mpaka nyumbani kwa askofu kumwambia nini kilichokuwa kimetokea. Askofu wa ajabu mara moja akaanza kwenda hospitali wakati Edwin akiendesha kuelekea nyumbani kwa Hamblin. Hapo yeye pamoja na mke wake, Charlotte, ambaye pia alikuja akikimbia, sasa alikuwa akicheza na watoto watano wa Hamblin-wasiokuwa na mama, wa kuanzia miaka 12 mpaka miaka 3. Aliwalisha chakula cha jioni, alifanya nao mazoezi ya muziki ya papo kwa papo na kuwasaidia kujiandaa kulala.

Brett alianiambia baadaye, “Sehemu ya kushangaza ya habari hii si kwamba Edwin alikuja tu pale nilipomwita. Katika dharura, mara zote kuna watu ambao wako tayari kusaidia. Hapana, sehemu ya kushangaza ya habari hii ni kwamba alikuwa ni mmoja niliyemfikiria. Kulikuwa na watu wengine kunizunguka. Kristin ana kaka yake na dada yake ambao wote wanaishi si zaidi ya maili tatu toka hapa. Tuna askofu mzuri, mzuri sana. Lakini uhusiano kati ya Edwin na mimi ni ule kwamba nilihisi kwa hamu kumpigia simu wakati nilipohitaji msaada. Kanisa hutupatia njia iliyoundwa ya kuishi amri ya pili vizuri zaidi—kupenda, kutumikia na kuanzisha mahusiano na kaka zetu na dada zetu ambayo hutusaidia kusonga karibu na Mungu.”11

Edwin alizungumza kuhusu uzoefu huu, “Mzee Holland, kikubwa katika yote haya ni kwamba Brett amekuwa mwalimu wa nyumbani wangu kwa zaidi ya mimi nilivyokuwa wao. Kwa muda, ametutembelea zaidi kama rafiki kuliko kama kutimiza jukumu. Amekuwa mfano mkuu, mfano wa jinsi gani mwenye ukuhani anatakiwa kuwa katika uwajibikaji na kazi. Mke wangu, wavulana wetu, sisi hatumwoni kama mwenye jukumu la kutuletea ujumbe kila mwisho wa mwezi; tunamfikiria kama rafiki ambaye anaishi tu mtaa unaofuata wa karibu, ambaye angefanya lolote katika dunia hii kutubariki. Ninafurahi ningeweza kumlipa kiasi kidogo cha deni analonidai.”12

Akina kaka na akina dada, ninaungana nanyi kutoa heshima kwa kila mwalimu wa mtaa, mwalimu wa kata na mwalimu wa nyumbani na mwalimu mtembeleaji ambaye anahudumu kwa uaminifu sana katika historia yote. Sala zetu leo ni kwamba kila mwanaume na mwanamke—na vijana wetu wakubwa wa kiume na wa kike—wataondoka toka mkutano huu na msimamo mkuu la kujaliana kwa moyo wa dhati, wakihamasishwa tu na upendo wa kweli wa Kristo katika kufanya hivyo. Licha ya kile sisi sote tunahisi ni kikomo na mapungufu yetu—na sisi sote tuna changamoto—hata hivyo, na tufanye kazi bega kwa bega pamoja na Bwana katika shamba la mzietuni,13 tukimpa Mungu na Baba yetu sote mkono wa usaidizi katika hii Kazi yake kuu sana ya kujibu maombi, kuleta faraja, kufuta machozi, na kuimarisha magoti yaliyolegea.14 Kama tutafanya hivyo, tutakuwa zaidi kama wanafunzi wa Kristo ambao tulitakiwa kuwa. Katika hii Jumapili ya Pasaka, acha tupendane mmoja kwa mwingine kama alivyotupenda sisi,15 mimi naomba katika jina la Yesu Kristo, amina.