2010–2019
Vitu Vidogo na Rahisi
Aprili 2018


Vitu Vidogo na Rahisi

Tunahitaji kukumbushwa kwamba kwa ujumla na katika kipindi cha wakati muhimu vitu hivi vinavyoonekana vidogo hutenda vitu vikubwa.

I.

Kaka na dada zangu wapendwa, nawapenda, nimeguswa sana na kuelimishwa na kuinualiwa na jumbe na muziki na hisia za wakati tukiwa pamoja. Nina hakika ninaongea kwa niaba yenu katika kutoa shukrani kwa kaka na dada zetu ambao, kama vyombo katika mikono ya Bwana, wametupatia athari ya kuimarisha ya wakati huu tukiwa pamoja.

Ninashukuru kuzungumza na hadhira hii katika Jumapili ya Pasaka. Leo tunaungana na Wakristo wengine katika kusheherekea Ufufuko wa Bwana Yesu Kristo. Kwa waumini wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho, Ufufuko halisi wa Yesu Kristo ni nguzo ya imani yetu.

Kwa sababu tunaamini matukio kote katika Biblia na Kitabu cha Mormoni kuhusu Ufufuko halisi wa Yesu Kristo, tunaamini pia mafundisho mengi ya maandiko kwamba ufufuko kama huo utakuja kwa wote wenye kufa ambao wamewahi kuishi juu ya dunia hii. Ufufuko huo hutupatia kile Mtume Petro alikiita “tumaini lenye uzima” (1 Petro 1:3). Tumaini hilo lenye uzima ni usadikisho wetu kwamba kifo siyo hitimisho la utambulisho wetu bali tu hatua muhimu katika mpango wa rehema wa Baba yetu wa Mbinguni kwa wokovu wa watoto Wake. Mpango huo hutoa haja ya mageuzi kutoka kufa kwenda kutokufa. Kiini cha mageuzi hayo ni machweo ya kifo na asubuhi tukufu iliyowezeshwa na Ufufuko wa Bwana na Mwokozi wetu ambao tunasherehekea katika Jumapili hii ya Pasaka.

II.

Katika wimbo mkuu ambao maneno yake yaliandikwa na Eliza R. Snow, tunaimba:

Ni mkuu jinsi gani, mtukufu jinsi gani, ni kamili jinsi gani

Usanifu mkuu wa ukombozi,

Pale haki, upendo, na rehema hukutana

Kwenye uwiano wa kiungu!1

Katika ukuzaji wa usanifu huo wa kiungu na uwiano, tunakusanyika katika mikutano, ikiwemo mkutano huu, kufundishana na kutiana moyo.

Asubuhi hii nimehisi kutumia kama ujumbe wangu fundisho la Alma kwa mwanawe Helamani, lililoandikwa katika Kitabu cha Mormoni: “Kupitia kwa vitu vilivyo vidogo na rahisi vitu vikubwa hutendeka” (Alma 37:6).

Tunafundishwa vitu vingi vidogo na rahisi katika injili ya Yesu Kristo. Tunahitaji kukumbushwa kwamba kwa ujumla na katika kipindi cha wakati muhimu vitu hivi vinavyoonekana vidogo hutenda vitu vikubwa. Kumekuwa na mahubiri mengi juu ya mada hii kutoka kwa Viongozi Wakuu Wenye Mamlaka na kwa waalimu wengine wa kuheshimika. Mada ni muhimu kiasi kwamba ninahisi kuendelea nayo tena.

Nilikumbushwa juu ya nguvu ya vitu vidogo na rahisi baada ya muda kwa kitu nilichoona katika matembezi ya asubuhi. Hapa kuna picha niliyopiga. Njia ya miguu ya saruji nene na imara inafanya ufa. Je, hii ni matokeo ya baadhi ya msukumo mkubwa na wenye nguvu kutoka chini? Hapana, ufa huu unasababishwa na ukuaji mdogo wa taratibu, wa mojawapo ya mizizi ukipenyeza nje kutoka kwenye mti uliopakana. Hapa kuna mfano kama huo nilioona kwenye mtaa mwingine.

Picha
Ufa kwenye njia ya miguu
Picha
Ufa mwingine kwenye njia ya miguu

Nguvu ya msukumo iliyoleta nyufa kwenye njia hizi za miguu za saruji ilikuwa ndogo sana kupimika kila siku au hata kila mwezi, lakini athari yake baada ya muda ilikuwa na nguvu ya ajabu.

Ndivyo ilivyo athari yenye nguvu baada ya muda ya vitu vidogo na rahisi tunavyofundishwa katika maandiko na manabii wanaoishi. Fikiria kujifunza maandiko ambako tumekuwa tukifundishwa kushirikisha katika maisha yetu ya kila siku. Au fikiria sala za binafsi na sala za kupiga magoti za familia ambazo ni utaratibu wa kila siku kwa Watakatifu wa Siku za Mwisho waaminifu. Fikiria uhudhuriaji wa seminari kwa vijana au madarasa ya chuo kwa vijana wakubwa. Japo kila moja ya taratibu hizi zinaweza kuonekana kuwa ndogo na rahisi, baada ya muda zinapelekea kwenye kuinuka na kukua kwa nguvu kiroho. Hii hutokea kwa sababu kila moja ya hivi vitu vidogo na rahisi hualika wenza wa Roho Mtakatifu, Mshuhudiaji ambaye hutuelimisha na kutuongoza kwenye ukweli, kama vile Rais Eyring alivyoelezea.

Chanzo kingine cha kuinuka na kukua kiroho ni muendelezo wa utaratibu wa kutubu, hata kwa makosa yanayoonekana madogo. Ushawishi wetu wenyewe wa kujitathmini-kibinafsi unaweza kutusaidia kuona jinsi gani tumepungukiwa na jinsi tunavyoweza kufanya vizuri zaidi. Toba kama hiyo inapaswa kutangulia upokeaji wetu wa sakramenti kila wiki. Baadhi ya mada za kuzingatia katika mchakato huu wa toba zinapendekezwa katika wimbo “Je, Nimetenda Wema Wowote?”

Je, Nimetenda wema wowote ulimwenguni leo?

Je, nimemsaidia yeyote aliye na mahitaji?

Je, nimewachangamsha walio na huzuni na kufanya mtu kuhisi furaha?

Ikiwa sivyo, nimekosea sana.

Je, mzigo wa yeyote umerahisishwa leo

Kwa kuwa Nilikuwa radhi kushiriki?

Je, wagonjwa na wadhaifu wamesaidiwa njiani mwao?

Walipohitaji usaidizi wangu, je Nilikuwapo?2

Kwa hakika hivi ni vitu vidogo, lakini kwa hakika ni mifano mizuri ya kile Alma alifumfundisha mwanawe Helamani: “Na Bwana Mungu hutumia njia zake ili kutimiza kusudi lake kuu na la milele; na kwa njia ndogo sana Bwana … hutimiza wokovu wa roho nyingi” (Alma 37:7).

Rais Steven C. Wheelwright aliwapa hadhira katika Chuo Kikuu cha Brigham Young–Hawaii maelezo haya yenye ushawishi ya fundisho la Alma: “Alma anamthibitishia mwanawe kwamba hakika mpangilio Bwana anaofuata tunapoonyesha imani Kwake na kufuata ushauri wake katika vitu vidogo na rahisi, ni kwamba Yeye hutubariki kwa miujiza midogo kila siku, na kwa muda, kwa kazi za kushangaza.”3

Mzee Howard W. Hunter alifundisha kwamba “mara kwa mara ni majukumu ya kawaida … ambayo yana athari chanya kubwa katika maisha ya wengine, ikilinganishwa na vitu ambavyo ulimwengu mara nyingi huusisha na ukuu.”4

Fundisho la kushawishi la kidunia la kanuni sawa na hii linatoka kwa Dan Coats Seneta wa zamani wa Indiana, ambaye aliandika: “Maandalizi pekee kwa uamuzi ule mmoja mzito unaoweza kubadili maisha, au hata taifa, ni yale mamia na maelfu ya maamuzi ya nusu-kujitambua, kujielezea-kibinafsi, kunakoonekana kusiko na maana kunakofanywa kwa siri.”5

Maamuzi hayo ya siri “yanayoonekana yasiyo na maana” hujumuisha jinsi tunavyotumia muda wetu, kile tunachoangalia kwenye runinga na mtandaoni, kile tunachosoma, sanaa na muziki ambao tunajihusisha nao kazini na nyumbani, kile tunachotafuta kwa ajili ya burudani, na jinsi tunavyotumia msimamo wetu kuwa waaminifu na wakweli. Kitu kingine kinachoonekana kidogo na rahisi ni kuwa waungwana na wachangamfu katika muingiliano wetu kibinafsi.

Hakuna kati ya vitu hivi vidogo na rahisi vya kupendeza vitatuinua kwenye vitu vikubwa isipokuwa vimefanywa kwa dhati na kwa uendelevu. Rais Brigham Young aliripotiwa akisema: “Maisha yetu yameundwa na hali chache na rahisi ambazo hufikia kiwango kikubwa sana zikiletwa pamoja, na hutoa muhtasari wa maisha yote ya mwanaume au mwanamke.”6

Tumezungukwa na ushawishi wa vyombo vya habari na kuharibika kwa utamaduni ambako kutatupeleka chini ya mto katika maadili yetu kama hatuendelei kukataa. Ili kwenda dhidi ya mto kuelekea lengo letu la milele, lazima kwa dhati tuendelee kupiga kasia. Inasaidia kama sisi ni sehemu ya timu ambayo inapiga kasia pamoja, kama wapiga kasia katika utendaji. Kurefusha mfano huo mbali zaidi, mikondo ni imara sana kiasi kwamba kama tutaacha kupiga kasia, tutachukuliwa chini ya mto kuelekea mwisho tusioutafuta lakini ambao hauepukiki kama kwa dhati hatujaribu kwenda mbele.

Baada ya kusimulia tukio linaloonekana dogo ambalo lilikuwa na matokeo makubwa, Nefi aliandika, “Na hivyo tunaona kwamba kwa njia ndogo Bwana anaweza kuleta vitu vikubwa” (1 Nefi 16:29). Agano la Kale hujumuisha mfano wa kukumbukwa wa hili. Hapo tunasoma jinsi Waisraeli walivyosumbuliwa na nyoka wakali. Watu wengi walikufa kutokana na kuumwa na nyoka (ona Hesabu 21:6). Musa aliposali kwa ajili ya usaidizi, alishawishiwa kutengeneza “nyoka wa shaba, na kumuweka juu ya mti.” Kisha, “ikiwa nyoka alimwuma mtu, alipoitazama ile nyoka ya shaba, aliishi” (mstari wa 9). Kitu kidogo kama hicho kwa matokeo ya kimiujiza kama hayo! Bado, kama Nefi alivyoelezea alipofundisha mfano huu kwa wale waliokuwa wakiasi dhidi ya Bwana, hata wakati Bwana alipotayarisha njia rahisi ambayo kwayo wangeweza kuponywa, “kwa sababu ya wepesi wa njia, au urahisi wake, kulikuwa na wengi walioangamia” (1 Nephi 17:41).

Mfano huo na fundisho hilo hutukumbusha kwamba wepesi wa njia au urahisi wa jukumu lililoamriwa haimaanishi kwamba siyo la muhimu kufikia tamanio letu la haki.

Kadhalika, hata matendo madogo ya kutokutii au kushindwa kidogo kufuata matendo ya haki kunaweza kutuvuta chini kuelekea matokeo tuliyotahadharishwa kuyaepuka. Neno la Hekima hutoa mfano wa hili. Huenda athari ya sigara moja katika mwili au kinywaji kimoja cha pombe au dozi moja ya dawa nyingine haiwezi kupimika. Lakini baada ya muda, athari ni kubwa na yaweza kuwa isiyotangulika. Kumbuka kupata ufa kwa njia ya miguu kwa mitanuko midogo ya taratibu ya mzizi wa mti. Kitu kimoja ni hakika, matokeo mabaya ya kupokea kitu chochote ambacho chaweza kuwa cha uraibu, kama vile madawa yanayoshambulia miili yetu au anasa za ponografia ambazo hushusha mawazo yetu, huweza kuepukika kabisa kama hatutapokea kwa mara ya kwanza—hata mara moja.

Miaka mingi iliyopita, Mzee M. Russell Ballard alielezea kwa hadhira ya mkutano mkuu “jinsi vitu vidogo na rahisi vinavyoweza kuwa hasi na vya uharibifu kwenye wokovu wa mtu.” Alifundisha: “Kama vinyuzi dhaifu ambavyo hutengeneza kitani, kisha ncha, na hatimaye kamba, vitu hivi vidogo vikiunganishwa pamoja vinaweza kuwa imara sana kutoweza kukatika. Lazima daima tuwe makini na nguvu ambayo vitu vidogo na rahisi vinaweza kuwa nayo katika kujenga kiroho. Wakati huo huo, lazima tuwe makini kwamba Shetani atatumia vitu vidogo na rahisi kutuongoza kwenye kufa moyo na huzuni.”7

Rais Wheelwright alitoa tahadhari kama hiyo kwa hadhira yake ya BYU–Hawaii: “Ni katika kushindwa kufanya vitu vidogo na rahisi ambapo imani hutetereka, miujiza hukoma, na maendeleo kuelekea kwa Bwana na ufalme Wake yanahairishwa na kisha kuanza kushindwa pale kutafuta ufalme wa Mungu kunapobadilishwa na kutafuta zaidi vitu vya muda na malengo ya ulimwengu.”8

Kujilinda dhidi ya malimbikizo ya madhara hasi ambayo ni angamizi katika maendeleo yetu ya kiroho, tunahitaji kufuata mpangilio wa kiroho wa vitu vidogo na rahisi. Mzee David A. Bednar alielezea kanuni hii katika Mkutano wa Wanawake wa BYU: “Tunaweza kujifunza mengi kuhusu asili na umuhimu wa mpangilio huu wa kiroho kutoka kwenye mbinu ya … maji yanayotona kwenye udongo katika kiwango cha chini,” tofauti na kufurika au kunyunyizia kiasi kikubwa cha maji ambapo kinaweza kuwa hakihitajiki.

Yeye alielezea, “Matone thabiti ya maji huzama ndani kwenye ardhi na kuleta kiwango kikubwa cha unyevu ndani ya udongo ambapo mimea inaweza kustawi. Katika hali kama hiyo, kama mimi na wewe tunazingatia na kila mara kupokea matone ya uthabiti wa virutubisho vya kiroho, ndipo mizizi ya injili inaweza kuzama kwa kina kwenye nafsi zetu, inaweza kuwa imeanzishwa kiuimara na thabiti, na inaweza kuzaa matunda yasiyo ya kawaida na matamu.

Aliendelea, akisema, “Mpangilio wa kiroho wa vitu vidogo na rahisi kuleta vitu vikubwa huleta uimara na uthabiti, huongeza kujitolea, na uongofu kamili zaidi kwa Bwana Yesu Kristo na injili Yake.”9

Nabii Joseph Smith alifundisha kanuni hii katika maneno yaliyojumuishwa sasa katika Mafundisho na Maagano: “Acha mtu yeyote asiyahesabu kama ni mambo madogo madogo; kwani kuna mengine … kuhusiana na watakatifu, ambao wanayategemea mambo haya” (M&M 123:15).

Kwa kuunganisha na majaribio ya mwanzo kuanzisha Kanisa katika Missouri, Bwana alishauri uvumilivu kwani “mambo yote lazima yatakuja kutimia katika wakati wake” (M&M 64:32). Kisha akatoa fundisho hili kuu: “Kwa hiyo, msichoke kutenda mema, kwa kuwa mnaijenga misingi ya kazi kubwa. Na kutokana na mambo madogo huja yale yaliyo makuu” (M&M 64:33).

Ninaamini sote tunatamani kufuata changamoto ya Rais Russel M. Nelson ya kuendelea mbele “katika njia ya agano.”10 Msimamo wetu kufanya hivyo huimarishwa kwa kufuata kwa dhati “vitu vidogo” tunavyofundishwa na injili ya Yesu Kristo na viongozi wa Kanisa Lake. Ninashuhudia juu Yake na kuomba baraka Zake juu ya wote wanaotafuta kuendelea katika njia Yake ya agano, katika jina la Yesu Kristo, amina.

Muhtasari

  1. “How Great the Wisdom and the Love,” Hymns, no. 195.

  2. “Have I Done Any Good?” Wimbo, no. 223,

  3. Steven C. Wheelwright, “Nguvu ya Vitu Vidogo na Rahisi” (Ibada ya Chuo Kikuu cha Brigham Young–Hawaii, Aug. 31, 2007), 2, devotional.byuh.edu.

  4. Teachings of Presidents of the Church: Howard W. Hunter (2015), 165.

  5. Dan Coats, “America’s Youth: A Crisis of Character,” Imprimis, vol. 20, no. 9 (Sept. 1991), 4; see also Elder Wilford Andersen in his column in the Mesa Tribune, May 1996.

  6. Hotuba za Brigham Young, katika Maskani ya Ogden, July 19,1877, kama ilivyowasilishwa katika “Hotuba,” Deseret News, Oct. 17, 1877, 578.

  7. M. Russell Ballard, “Vitu Vidogo na Rahisi,” Ensign, Mei 1990, 7.

  8. Steven C. Wheelwright, “Nguvu ya Vitu Vidogo na Rahisi,” 3.

  9. David A. Bednar, “Kupitia Vitu Vidogo na Rahisi Vitu Vikubwa Hufanyika” (Mkutano wa Wanawake wa Chuo kikuu cha Brigham Young, Apr. 29, 2011), mkutanowa wanawake.byu.edu.

  10. Russell M. Nelson, “As We Go Forward Together,” Liahona, Apr. 2018, 7.