2019
Yesu Anawapenda Watoto Wetu
Oktoba 2019


Yesu Anawapenda Watoto Wetu

Ninatumia muda mwingi kuwafikiria watoto. Ninawapenda watoto katika mduara wangu wa familia na marafiki. Kwa kuongezea, kazi yangu kwenye majarida ya Kanisa inahusisha kutengeneza na kuhariri kurasa kwa ajili ya watoto wote ulimwenguni. Lakini miaka kadhaa iliyopita, nilitambua kwamba sikuwahi kujifunza kile maandiko matakatifu yalichofundisha kuhusu watoto. Hivyo niliamua kusoma Agano Jipya na Kitabu cha Mormoni na kutoa umakini wa ziada kwenye kile nilichoweza kujifunza kuhusu kundi hili maalumu.

Iilikuwa ni zoezi la kubadili maisha! Kati ya kweli nyingi nilizogundua, moja yenye thamani kubwa ilikuwa ni ongezeko la uelewa wa kiasi gani Yesu anawajali watoto. Aliwahudumia watoto kama kundi maalumu, aliwatenga kutoka kwa wengine, tena na tena. Je, ni kwa jinsi gani sisi tunaweza kufuata mfano Wake?

Makala yangu kwenye ukurasa wa 18 inashiriki baadhi ya masomo niliyopata kutoka kwenye uzoefu huo wa kujifunza maandiko, yakiunganishwa na mawazo na mchango kutoka kwa wataalamu kadhaa katika eneo la kuzuia unyanyasaji.

Watoto wana thamani kubwa. Natumaini tunaweza kushirikiana kuwalinda na kuwawezesha, kuwatendea kama ambavyo Yesu angewatendea!

Kwa upendo,

Marissa Widdison