2019
Onyesha na Sema
Oktoba 2019


Onyesha na Sema

Mkutano mkuu upo mwezi huu! Hapa ni kile baadhi ya watoto hufurahia kuhusu mkutano.

Picha
Show and Tell

Abel C. and Tina S., miaka 10 na 9, kaunti ya Bong, Liberia, ni kaka na dada. Abel anapenda mkutano “kwa sababu huo ndio wakati tunapomuidhinisha nabii wetu kama Rais wa Kanisa kila mwaka.” Tina “anapenda wakati nabii anazungumza kuhusu mahekalu.”

Anna B., miaka 10, Maharashtra, India, aliangalia mkutano pamoja na mama yake. Yeye huja na shajara yake na kalamu kwenye kila mkutano ili kuandika shuhuda na jumbe anazosikia.

David na Juliana M., miaka 4 na 6, South Holland, Netherlands, hujaza mabakuli 15 kwa asusa na kuweka picha ya Mtume au mshiriki wa Urais wa Kwanza kwenye kila moja. Wakati mmoja wa Akina kaka anapozungumza, wanakula kile kilichomo kwenye chombo!

Ninapenda kumsikiliza nabii kwa sababu Bwana huzungumza kupitia yeye.

Andrés C., miaka 12, Valle del Cauca, Colombia

Ninapenda kuangalia mkutano kwa sababu ninapenda kujifunza kutoka kwa manabii, na ninapenda kutumia muda huo pamoja na familia.

David J., miaka 9, Sololá, Guatemala

Ninapenda kusikiliza hadithi na kwaya ikiimba. Ninapenda pia kusikiliza mifano wanayotoa.

Yuri H., miaka 8, Taoyuan, Taiwan