2019
Mzee Stevenson Anazuru Chile
Oktoba 2019


Mitume kote Ulimwenguni

Mzee Stevenson Anazuru Chile

Mitume wanasafiri kote ulimwenguni kuwahudumia watu na kuwafundisha kuhusu Yesu Kristo.

Picha
Elder Stevenson Visits Chile

Mzee Gary E. Stevenson na Dada Lesa Stevenson walisafiri pamoja na Rais Russell M. Nelson na Dada Wendy Nelson kwenda Chile kwa ajili ya tukio muhimu sana. Hekalu jipya lilikuwa likiwekwa wakfu katika jiji la Concepción!

Hekalu hili jipya la kupendeza ni la pili kujengwa Chile na ni hekalu la 18 katika Amerika ya Kusini.

Matetemeko mengi hutokea Chile. Hekalu la Concepción Chile lina msingi maalumu kulilinda kutokana na uharibifu ikiwa tetemeko litapiga.

Laura na Alicia O. walisaidia kuweka jiwe la mwisho nje ya hekalu. Hili linaitwa jiwe la pembeni la hekalu. Hatimaye hekalu lilikuwa tayari kuwekwa wakfu.

Watoto walikuja na wazazi wao kumsikiliza Rais Nelson akitoa sala maalumu kuweka wakfu hekalu.

Sasa waumini wenye kustahili wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho wanaweza kuingia ndani ili kuunganishwa na familia zao na kutumikia kwa kufanya ubatizo wa hekaluni!

Hapa ni kile Mzee Stevenson alichosema kuhusu kuweka wakfu: