2021
Kuwasaidia Watoto Kujitayarisha kwa ajili ya Ubatizo
Januari 2021


Kuwasaidia Watoto Kujitayarisha kwa ajili ya Ubatizo

Tunaweza kuwa wenye sala, wenye kusaidia na wavumilivu tunapowasaidia watoto wetu kuchukua hatua hii kuelekea njia ya agano.

Picha
image showing a family, baptism, and confirmation

Mchoro na Bryan Beach

Kubatizwa na kuthibitishwa ni tukio muhimu la kihistoria lenye kusisimua kwa watoto katika Kanisa. Wakati ambapo wengi huitazamia ibada hizi, pia ni jambo la kawaida kwa watoto kuhisi wasiwasi na kuogopa.

Kama mwandishi wa Rafiki, gazeti la Kanisa kwa ajili ya watoto, nimesikiliza hadithi nyingi ambapo watoto huogopa kuwa hawakotayari kufanya agano hili. Baadhi yao huogopa kwamba hawana ushuhuda imara na wa kutosha. Baadhi wanaogopa maji. Na baadhi huona ni mzigo mkubwa kwa wao kuwa wakamilifu.

Hapa ni njia chache za kumsaidia mtoto wako kujisikia amejitayarisha na mwenye kujiamini kuchukua hatua yao inayofuata kwenye njia ya agano.

Fundisha kwa Kukusudia

Inaweza kuwa rahisi kufikiri ubatizo kama ibada ya mpito au kitu tu ambacho kinatokea wakati mtoto wako anapofikia umri wa miaka minane. Lakini hakika, ubatizo ni uchaguzi mtakatifu, ambao humaanisha kwamba wanahitaji kuelewa kwa nini ni muhimu. Kuwafundisha kwa kukusudia kunaweza kuwasaidia kufanya ubatizo kuwa na maana zaidi (na kuwapunguzia kuogopa). Wafundishe katika njia ambayo ungetumia kwa yoyote ambaye anajifunza kuhusu Kanisa kabla ya kubatizwa.

Ni muhimu kwetu kuwafundisha watoto kuhusu maagano watakayofanya kwenye ubatizo. Na habari njema ni kuwa, hiki siyo kitu fulani tunachopaswa kufanya (au tunachopaswa) kujaribu kufanya siku moja au ndani ya wiki moja. Wakati wa kujifunza injili nyumbani mwako ulio endelevu ni njia nzuri zaidi ya kumsaidia mtoto wako kujitayarisha kwa ajili ya ubatizo. Hata hivyo, kuna mambo machache ambayo ni maalumu ambayo yatasaidia ukifokasi juu yake wakati ubatizo wa mtoto wako unapokaribia:

  • Katika maneno rahisi, jadili jinsi gani kubatizwa kunamaanisha kuahidi kumfuata Yesu Kristo.

  • Soma kuhusu ubatizo katika maandiko, kama vile Mosia 18:8–10. Fafanua mistari hiyo ili mtoto wako aelewe na aweze kufundisha mawazo hayo kwako wewe. Kwa mfano, msichana mmoja aliyebatizwa hivi karibuni huko Hawaii, Marekani, alielezea “kubebeana mizigo” kama “kumsaidia kila mmoja wakati wowote wanapohitaji msaada.”

  • Hakikisha umezungumza nao kuhusu kipawa cha Roho Mtakatifu, na shiriki uzoefu uliokuwa nao wakati Roho Mtakatifu alipobariki maisha yako.

Baadhi ya watoto wanaweza kuwa na wasi wasi kuhusun ubatizo kwa sababu hawadhani kuwa wana ushuhuda imara vya kutosha. Wasaidie watoto wako kukumbuka hisia nzuri walizokuwa nazo wakati walipofanya jambo la ukarimu, wakiimba katika Msingi, au wakizungumza kuhusu injili Wahimize kufikiria njia ambazo kwa hizo wao wanajua kwamba Baba wa Mbinguni anawapenda. Elezea kwamba hivi vyote ni mwanzo wa ushuhuda na kwamba ushuhuda wao utakua muda unavyoenda wanapoendelea kufanya chaguzi nzuri.

Onyesha Kitu cha Kutegemea

Kama mtoto wako ana wasiwasi kuhusu kubatizwa—au hata kama haonekani kuwa hivyo—inaweza kuwa ya msaada kuongelea kuhusu kile kinachotegemewa. Mahali pazuri pa kuanzia ni kuwaandaa kwa ajili ya mahojiano watakayokuwa nayo na askofu au rais wa tawi. Kumsaidia mtoto wako kujibu maswali kama, “Kwa nini ubatizo ni muhimu?” na “Je, ina maanisha nini kujichukulia juu yako jina la Kristo?” inaweza kuwasaidia kujiandaa kwa ajili ya majadiliano haya. Msaidie mtoto wako kukumbuka kwamba askofu yuko pale ili kuwasaidia wao kuwa tayari, siyo kuwahoji wao au kuwaweka sawa. Na kumbuka, wewe daima unaweza kuongozana na mtoto wako katika mahojiano hayo, ukitaka.

Kitu kingine cha kumwandaa mtoto wako kwa ajili yake ni kile anachotarajia kimwili katika siku ya ubatizo. Waonyeshe jinsi ya kusimama wakati wakiwa ndani ya kisima cha ubatizo. Unaweza hata ukamwalika mwenye ukuhani atakaye mbatiza mtoto wako ili wafanye mazoezi ya kimwili wakiwa nje ya maji, ili mtoto wako awe anajua jinsi itakavyokuwa kuzamishwa chini na kuinuliwa tena juu. Mwelezee itakavyokuwa wakati wa kuthibitishwa.

Kama mtoto wako ni mwoga kwenda chini ya maji, kwa sala fikiria njia za kumsaidia kushinda uoga huo kadiri siku za ubatizo wake zinavyokaribia. Labda wewe na mtoto wako mnaweza kumwangalia mtu mwingine anavyobatizwa ili kuona jinsi muda mchache tu wanapokuwa ndani ya maji. Pengine wewe na mtoto wako mnaweza kufanya mazoezi ya kuziba pua zenu na kuingiza sura zenu ndani ya maji kwa pamoja kwa sekunde chache kwa wakati mmoja. Panaweza kuwa na mtu katika eneo lenu anayewafundisha watoto kuogelea ambaye anaweza kuwa na ushauri. Lolote unalofanya, hakikisha unalifanya kwa upendo na subira.

Kadiri mtoto anavyojisikia amejiandaa zaidi kuhusu mambo ya kimwili juu ya ubatizo, ndivyo watakavyokuwa watulivu zaidi na wenye kufokasi juu ya agano hili la kiroho wanalofanya.

Fokasi juu ya Maendeleo, Siyo Ukamilifu

Wakati mwingine, labda kwa sababu tunaongea sana kuhusu kipengele cha kuoshwa cha ubatizo, watoto wanaelewa vibaya na kufikiri wanaaswa kuwa wakamilifu baada ya ibada. Moja ya hadithi za kawaida sana tunazozisikia kwenye Rafiki ni kuingiwa na hofu mtoto anakokusikia wakati wanapofanya makosa kwa mara ya kwanza baada ya kuwa wamekwisha kubatizwa. Kubishana na kaka au dada yake au kusahau kufanya kazi kunawafanya wajisikie kama wameharibu milele hisia nzuri walizokuwa nazo!

Kama wazazi na viongozi, ni muhimu sana tuwasaidie watoto wetu kuelewa kanuni ya toba. Je, watoto wetu wanaelewa kwamba kutambua makosa yetu na kujifunza kutokana nayo ni sehemu ya jinsi tunavyojifunza na kukua hapa duniani? Je, wanajua kwamba wanaweza kuomba msamaha wakati wowote? Na kwamba wakati wanapochukua sakramenti kila wiki, wanafanya upya maagano yale waliyofanya kwenye ubatizo? Shuhudia kwamba nafasi ya kutubu ni baraka na ni zawadi. Ubatizo siyo kuhusu kuwa wakamilifu sasa bali ni kuhusu kuingia katika njia ya agano na kuchukua hatua kila siku za kuwa zaidin kama Yesu Kristo.

Picha
various people in front of a temple

Mwanzo Mzuri

Badala ya kuona ubatizo na uthibitisho kama hatima, tunaweza kuwasaidia watoto wetu kuona huo kama mwanzo mzuri- mwanzo wa maisha mapya kama mfuasi wa agano wa Yesu Kristo. Iwe mtoto wako anahisi amehamasika, mwenye wasi wasi, kidogo ya vyote hivi, unaweza kuhakikisha kuwa hawatembei njia hii pekee yao. Kwa kuwa mwenye kusali, mwenye kukusudia, na mwenye kusubiri, tunaweza kuwasaidia watoto wetu kujisikia shangwe wanapochukua hatua hii kurudi nyumbani kwao mbinguni.