2021
Kuwatumikia Wale Ambao Wamefungwa Jela
Januari 2021


Kuwatumikia Wale Ambao Wamefungwa Jela

Thamani ya nafsi ya mtu haipunguzwi na jinai.

Picha
collage image showing four different pictures of life in prison

Picha kutoka Getty Images

Sasa hivi, zaidi ya watu milioni 10 wanashikiliwa rumande au magerezani ulimwenguni kote.1 Yesu Kristo, ambaye anampenda kila mtu anayeelewa kila gumu, anatuomba sisi tuwatumikie watoto wote wa Baba wa Mbinguni- ikijumuisha wale ambao wamefungwa jela. “Ndipo wenye haki watakapomwuliza, wakisema, Bwana, ni lini tulikuona … kifungoni, na tukakujia?

“Na Mfalme atajibu, akiwaambia, Amin nawaambia, kadiri mlivyo mtendea mmoja wa hao ndugu zangu walio wadogo, mlinitendea mimi” (Mathayo 25: 36-40).

Je, tunawezaje kufanya kitu ambacho Mwokozi ametuomba na kwa usalama tuwatumikie wale ambao wamefungwa jela? Makala hii inatoka kanuni za msingi kama mahali pa kuanzia. Kupitia sala jadiliana na viongozi wa Kanisa wa eneo lako kuhusu kile ambacho kinafaa na cha busara kwa ajili ya eneo lako.

Watoto Wenzetu wa Mungu

Dough Richens anafanikiwa kuwafikia waumini wa Kanisa waliofungwa jela. Pia anaratibu pamoja na makundi mengine ya kiimani na kijamii ili kuwasaidia wale waliathiriwa na kifungo, bila kujali chimbuko lao au mtazamo wao wa kidini.

“Msemo wa kawaida kwa wale ambao wamefungwa jela ni kwamba wote hawaaminiki, wenye vurugu, na watu hatari,” Kaka Richens anasema. “Hata hivyo, nimegundua kwamba wengi wao hawako hivyo. Wengi wanajisikia majuto kwa vitendo vyao. Wanajaribu kujiinua juu ya chaguzi zao mbaya walizochagua wakati uliopita na wanaishi maisha mema.

Katika baadhi ya nchi, wengi karibia nusu ya wakazi wote wanaye mshiriki wa karibu wa familia ambaye amefungwa jela.2 Hawa waliofungwa jela ndugu wa kuzaliwa, wazazi, na watoto ni—mbali na uhusiano wa kufafanuliwa kidunia—watoto wenzetu wa Mungu.

Hukumu ya Duniani na ya Milele

Ingawa maisha yanatuhitaji sisi tufanye maamuzi, Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo ndio pekee wanaoweza kwa ukamilifu kumhukumu mtu kulingana na hali zao, matendo, na matamanio (ona 1 Samueli 16:7). Hukumu hiyo kamilifu hakika itazingatia hali walizozaliwa nazo watu ambazo hufanya kufungwa jela kuwa kitu tarajiwa, kama vile kiwewe katika familia, ufukara wa vizazi na vizazi, utamaduni wa matumizi ya dawa za kulevya, n.k. Sababu nyingine nyingi zinaweza kushawishi uwezekano wa mtu kufanya chaguzi nzuri, ikijumuisha afya zao na ustawi.3 Wakati ni muhimu kwa jamii kuimarisha sheria zenye kuziweka salama jumuiya, tunaweza kufanya hivyo kwa huruma na kwa mtazamo wa milele, tukitambua kwamba kuna mengi tusiyoelewa.

“Fikiria kuhusu jinsi ambavyo wewe ungejisikia kama ungelihukumiwa kwa maisha yako yote yaliyosalia kutokana na kitu kibaya ambacho kamwe haujakifanya,” alisema Tanja Schaffer, muumini wa Kanisa ambaye alifanya kazi kwenye ofisi ya sheria kabla ya kuanzisha kikundi cha kuwatetea wafungwa. “Ni juu ya Mungu kumsamehe atakaye kumsamehe, lakini Yeye anatuamuru sisi tumsamehe kila mtu” (ona Mathayo 18:21–22).

Kanuni ya hukumu kamilifu ya Mungu inaweza pia kuwa chanzo cha faraja kwa waathirika wa makosa ya jinai. Wakati mwingine watu wanaowaumiza wengine katu hawakabiliwi na adhabu hapa duniani. Waathirika wanaweza kuteseka kwa muda mrefu baada kipindi cha mkosaji kuwa jela kwisha. Watu wengi walio athiriwa na kufungwa jela wamekuwa vyote viwili mwaathirika na mkosaji kwa nyakati tofauti, ikitukumbusha sisi kwamba maisha ni mtandao mgumu wa uhusiano na maamuzi ambayo huwaathiri wengine. Tunaweza tukapata faraja kwa kuamini kwamba Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo wanaelewa yote. Hukumu yao itakuwa kamilifu. Uponyaji Wanaotoa—kwa wote asiye na hatia na mwenye kutubu—utakuwa kamili (ona Ufunuo 21:4).

Mfano wa Upendo wa Viongozi

Mzee Gerrit W. Gong wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili anaelezea mkutano ambao kila mmoja kumzunguka yeye alikuwa amevaa mavazi meupe. Kulikuwepo na kuimba na kuomba, na upendo wa Mungu ulikuwa tele.4 Kinyume na kile ambacho wengi wetu tungeweza kupiga picha akilini, huu haukuwa mkutano wa hekaluni. Hii ilikuwa ni maongezi ya utumishi kwenye gereza ambako suti nyeupe ilikuwa ni sare ya wote.

“Viongozi wa Kanisa wanajali kuhusu wote ambao wameathiriwa na jinai na kufungwa jela,” Kaka Richens alishuhudia, akielezea jinsi kiongozi mmoja anatoa nakala yake mwenyewe ya gazeti la Kanisa kwa mtu mmoja anayemtembelea gerezani kila mwezi. “Mara kwa mara wanawatembelea waliofungwa jela, kusaidia familia zao, na kwa upendo wanashughulikia waathirika.”

Huduma za urekebishaji wa tabia ni wajibu wa rais wa kigingi, akifanya kazi kwa pamoja na viongozi wa kata katika kushughulikia shida za wale walio katika eneo lao. Je, viongozi wenu wa kigingi wanafanya nini ili kuwatumikia na kushiriki ujumbe wenye kuwainua waumini waliofungwa jela? Katika mahali pengine, waumini wa Kanisa wanaweza wakaitwa ili kuwatembelea na kuwafundisha watu waliofungwa jela. Kaka Richens alisema kwamba mara nyingi wale waumini walioitwa kutoa msaada wanakuwa na wasi wasi mwanzoni, lakini baadae wanagundua kwamba wito wao ni wa maana sana kiasi kwamba huwa hawataki kupumzishwa.

Ni dini iliyo safi“,” alisema (ona Yakobo 1:27).

Tusijisikie kulazimishwa kuwatembelea watu waliofungwa jela tusiowajua, kuna njia nyingine tunazoweza kutumikia kwa usalama kabisa. Hapa ziko chache:

  • Wajumuishe watu waliofungwa jela katika maombi yako, hususani yeyote unayemjua kwa jina. Maombi yana nguvu sana!

  • Ulizia magereza yaliyo katika eneo lenu au rumande kama wanahitaji misaada ya vitu mbali mbali. Vitu kama vifaa vya kufumia, vitu vya kusoma, sanaa, na utafiti wa historia za familia kama vinaruhusiwa katika majumba hayo

  • Kama unamjua mtu ambaye amefungwa jela, mwandikie barua zenye kumwinua Fanya chaguzi salama na za busara wakati mkiwasiliana. Mfuate Roho na tunza mipaka sahihi.

  • Watende washiriki wa familia za wale waliofungwa jela—hususani watoto—kwa upendo, heshima, na wajumuishe. Kumbuka kwamba washiriki wa familia kimsingi ni waathirika wasio na hatia pia. Roho Mtakatifu anaweza kutusaidia kuelewa namna bora ya kuwatumikia washiriki wote wa familia.

Picha
woman sitting on bed and praying

Roho Mtakatifu Hana Kikomo

Kufungwa jela kunaweza kuwa wakati mgumu sana katika maisha ya mtu. Lakini Roho Mtakatifu hazuiliwi na kuta, vyuma, au minyororo. Maombi, kujifunza maandiko, na unyenyekevu vinaweza kualika uwepo wake wenye kufariji kwa haraka sana ndani ya chumba cha jela kama tu nje. Kwa sababu ya hiyo, kifungoni kunaweza kuwa mahali pa miujiza.

Portia Louder, muumini wa Kanisa aliyeandika tangazo kwenye blogi wakati akiwa amefungwa jela, akielezea wakati wake akiwa gerezani kama safari ngumu ya imani na kujigundua kwake yeye mwenyewe. “Nimepitia matatizo mengi makali katika maisha yangu, lakini naweza kujisikia mwenyewe kuponywa kupitia upendo ambao ni wa maajabu,” “Changamoto yoyote unayokabiliwa nayo sasa hivi, popote ulipo katika safari yako mwenyewe, tafadhali usikate tamaa!”

Garrf Cannon, ambaye alikuwa rais wa tawi aliyewahudumia walio jela, alielezea jinsi Roho alivyomshawishi kuongea kwa ukarimu na mtu aliyefungwa jela ambaye aliyeishi maisha magumu. “Kitu ulichosema hivi punde kwangu yalikuwa maneno ya ukarimu zaidi yaliyowahi kuzungumzwa kwangu katika maisha yangu,” mtu huyu alisema. “Sikumbuki kuwahi kuongelewa kwa ukarimu na upendo. Asante.” Walimaliza maongezi yao kwa maombi ya kwanza mtu huyu kuwahi kusikia katika miaka mingi.

“Ndiyo, Roho Mtakatifu hakika yuko katika majengo ya magereza,” Kaka Cannon alishuhudia. “Watoto wa Mungu wako pale, na anawataka warudi.”

Mungu anafanya ahadi za nguvu kwa wote ambao huchagua kumfuata Yeye, iwe ndio kwanza tunajifunza kuhusu Yeye katika shule ya Jumapili au kifungoni. Kama Ezekieli 36:26 isemavyo, “Nami nitawapa ninyi moyo mpya, nami nitatia roho mpya ndani yenu.”

Kuingia tena kwenye Jumuiya Ni Changamoto Kali

Wakati mtu fulani anatamani kuwa bora, je, tunawaruhusu wao kukua na kusamehewa?

“Neema na huruma ya Mungu ina nguvu mno,” Kaka Richens alisema. “Wakati mwingine mtu aliyefungwa jela anahisi kusamehewa na Bwana mapema kabla ya kusamehewa na serikali, jamii, au hata waumini wa Kanisa.”

Kurudi katika jamii baada ya kufungwa jela ni vigumu. Wale waliofungwa jela mara nyingi wanapata taabu kupata kazi au nyumba. Tunaweza kuwasaidia kupata usalama katika mahali pazuri na kuendelea kufuata mapendeleo yenye afya. Pengine kitu muhimu zaidi tunachoweza kufanya ni kuwa rafiki chanya, mwenye kuimarisha. Wakati Joseph Smith alipozungumza kuhusu marekebisho ya kifungo gerezani wakati akigombea kuwa rais, alifundisha kwamba “ukali na kutenga kamwe hakutafanya zaidi kuliko kurekebisha tabia za watu kama kusikiliza na urafiki.”5

Huruma Hufanya Tofauti

Yuda aliwahimiza Watakatifu “kuwa na huruma” (Yuda 1:22). Maneno yake yanatoa mwangwi wa ombi la Mwokozi la kuwakumbuka wale walio kifungoni. Je, tutajibu namna gani mialiko hii? Acha tufanye jitihada ya kuwalisha wale wanaopitia ufungwa wa jela, na familia zao, kwa wema wa neno la Mungu. Huruma yetu inaweza kuleta tofauti.

Muhtasari

  1. Ona “World Prison Population List: Eleventh Edition,” National Institute of Corrections, nicic.gov.

  2. Ona “Half of Americans Have Family Members Who Have Been Incarcerated,” Dec. 11, 2018, Equal Justice Initiative, eji.org/news.

  3. Ona “Traumatic Brain Injury in Criminal Justice,” University of Denver, du.edu/tbi.

  4. Idara ya Ukuhani na Familia Christmas devotional, Disemba 2019.

  5. “Joseph Smith as a Statesman,” Improvement Era, Mei 1920, 649.