2021
Wanawake na Nguvu ya Agano
Januari 2021


Wanawake na Nguvu ya Agano

Tunaweza kushangilia katika heshima na nguvu tulizonazo kupitia ukuhani.

Picha
illustration of woman

Vielelezo na Amber Eldredge

Rais Russell M. Nelson alifundisha kwamba mbingu ziko wazi kwa wanawake waliopewa endaumenti ya nguvu za Mungu ikitiririka kutokana na maagano yao ya ukuhani kama ilivyo kwa wanaume ambao wana ukuhani.

“Ninaomba kwamba ukweli uweze kujiandika juu ya mioyo ya kila mmoja wenu kwa sababu ninaamini utabadili maisha yenu,” alisema. “Ningependa kuacha baraka juu yenu, kwamba muweze kuelewa nguvu ya ukuhani ambayo kwayo mmepokea endaumenti na kwamba mtaongeza nguvu hiyo kwa kufanyia kazi imani yenu katika Bwana na katika nguvu Yake.”

Ninapenda kwamba nabii wetu aliye hai alitualika kila mmoja wetu, kujifunza na kupokea ufunuo na vyema zaidi “kupata, kuelewa, na kutumia nguvu ambayo kwayo [tume]pewa kupitia endaumenti.”1

Mara nyingi katika maisha yangu yote, nimepata baraka hizo zilizoahidiwa ambazo huja kutokana na kufuata ushauri wa manabii. Mwaliko huu haukuwa tofauti. Katika kufikiria kuhusu mwaliko wa Rais Nelson, akili yangu mara moja iligeukia hekaluni—mahali ambapo nilipewa endaumenti kwa nguvu za ukuhani—na kipawa cha nguvu hizo zimekuwa nami katika maisha yangu yote. Imenichukua miaka mingi kutambua jinsi gani nguvu hizo zinajionyesha katika maisha yangu.

Nguvu ya ukuhani, zaidi kama kipawa cha Roho Mtakatifu, huja kutoka kwa mpendwa Baba yetu wa Mbinguni na kutokana na uadilifu wetu binafsi. Katika kushika maagano yetu na Bwana, tunayo fursa kupokea ufunuo kuhusu maisha yetu, kuhusu familia zetu, kazi, shule—kila kitu ambacho kwa ajili yake tunaomba mwongozo. Hakuna kitu kilicho muhimu kwetu ambacho sio muhimu kwa Bwana. Na tunapomwalika Roho kuwa pamoja nasi, tunaweza kuja kwenye ufahamu mkubwa zaidi juu ya nguvu ya ukuhani kupitia mwongozo wa Roho Mtakatifu.

Kadiri nilivyojifunza zaidi kuhusu nguvu ya ukuhani na kuguswa, ndivyo nilivyoelewa zaidi jinsi inavyohusika katika vipengele vyote vya maisha yetu. Nguvu ya ukuhani inatusaidia kupokea ufunuo kwa ajili ya changamoto zetu za kila siku.

Katika miito yangu, kwa sababu ya kuhudumu kwa mamlaka ya ukuhani niliyopewa na mtu mwenye funguo, pametokea na nyakati zisizohesabika wakati nilipokuwa na mawazo au maneno niliyopewa ambayo ndiyo msichana au dada wa Muungano wa Usaidizi wa Wakina Mama au mtoto wa Msingi alihitaji kusikia. Ninajua kuwa maneno yale yalikuja kwa sababu ya mamlaka ya ukuhani niliyokuwa nimepewa wakati nilipotengwa kwa ajili ya wito ule.

Katika ndoa, kama katika uhusiano mwingine wowote watu huenda kupitia ngazi na awamu za kujifunza na kukua. Nimejifunza kwamba ninapokumbuka mume wangu ni nani, mimi ni nani, na nini tunapaswa kufanya pamoja kama watoto wa Mungu, imebadilisha moyo wangu. Kuunganishwa pamoja kupitia mamlaka ya ukuhani kumetupa nguvu na kutuhamasisha sote wawili kuwa wamoja zaidi. Wakati Mwokozi aliposema, “Kama hamna umoja ninyi sio wangu” (Mafundisho na Maagano 38:27), Yeye hamaanishi tu katika mkao wa Kanisa. Yeye anamaanisha katika uhusiano wa familia zetu pia.

Na kama mama, nakumbuka kuwa na hofu kuhusu mtoto kijana mkubwa ambaye alikuwa akifanya mambo ambayo yasingemfanya kijana yule awe mwenye furaha. Tulikuwa tumeamua kujadiliana kuhusu jambo hilo na tukapanga muda wa kuongea. Kabla ya muda tuliokubaliana kwa ajili ya kupigiana simu, makaripio yangu yalikuwa tayari; nilijua hasa kile nilichokuwa nakwenda kusema. Niliomba ili Roho awe pamoja nami. Kile kilichotoka kinywani mwangu kuanzia mwanzo wa maongezi yetu na hadi mwisho wa simu ile kilikuwa tofauti kabisa na kile nilichopanga kusema Lakini kilikuwa ndicho kitu sahihi kabisa yule mtoto alichohitaji. Kipawa cha Roho Mtakatifu kilifanya iwezekane kwa mioyo kulainishwa na ufumbuzi bora zaidi ulionekana. Hilo ni onyesho la jinsi nguvu ya ukuhani inavyofanya kazi katika maisha yetu.

Picha
illustration of a couple holding up the walls of their home in a storm

Mara nyingi sana, wanawake hujilinganisha wenyewe na watu wengine. Lakini hakuna kati yetu anayejisikia vyema wakati tunapojilinganisha wenyewe na watu wengine. Kila mwanamke anayo aina ya kipekee ya uwezo na vipaji, na hivi vyote ni zawadi zilizotolewa na Mungu. Kwa sababu tu mimi na wewe hatuko sawa—au idadi yo yote ya wanawake sio ile ile—hii haitufanyi sisi kuwa wapungufu au zaidi. Tunahitajia kutafuta vipawa vyetu na kuvikuza, tukikumbuka ni nani aliyetupatia, na kisha tuvitumie kwa madhumuni Yake. Tunaposhiriki vipawa vyetu ili kuwabariki wengine, tutaona nguvu ya ukuhani katika maisha yetu.

Nimepata nafasi ya kukutana na wanawake wengi maarufu ambao wameonyesha imani na nguvu kupitia matendo yao. Wanawake wanatoa vipaji vyao na uwezo wao katika njia za kushangaza na za namna mbali mbali. Wanafanya tofauti kubwa katika maisha ya wale wanao wazunguka—katika familia zao, sehemu zao za kazi, kanisani, shuleni, au mahali pengine po pote wanapoutumia muda wao.

Moja ya vitu nilivyojifunza kuhusu ukuhani ni kwamba tunafanya vyema wakati tunapofanya kazi kwa kutegemeana na wengine. Hivyo ndivyo jinsi Bwana alivyopanga; huo ndio mpangilio mtakatifu. Hatuhitaji kushindana kwa sababu vipawa hivi vyote vilivyo tofauti na vipaji na uwezo vinahitajika—kutoka kwa wanaume na wanawake. Bwana anatuongoza pole pole pembeni mwa njia ile ili sisi sote tuweze kupata uelewa mzuri wa jinsi ya kufanya kazi pamoja na jinsi ya kuthamini mchango wa kila mmoja. Hakika hii ni njia bora ya kukamilisha kazi yake.

Wanawake hawahitaji kusubiri mtu awaambie kitu cha kufanya na vipawa , vipaji na nguvu zao. Tunao uwezo wa kupokea ufunuo kwa ajili yetu wenyewe. Hatupaswi kusubiri ili kutendewa, tunahitaji kuwa na ujasiri ili kutendea kazi ufunuo ambao tumepokea. Kutafuta na kuitikia mwongozo huo wa kiroho ni kithibitisho kwamba tunapokea toka kwenye nguvu za ukuhani ambazo tumeahidiwa wakati tunapoishi maagano tuliyoweka na Mungu.

Kama Rais Nelson alivyofundisha, “Ni kipi kingeweza kuwa cha kufurahisha zaidi ya kile cha kufanya kazi pamoja na Roho kuelewa nguvu za Mungu-ngvu za ukuhani?” Aliahidi “Wakati uelewa wako unaongezeka na wakati unapotumia imani yako katika Bwana na nguvu Yake ya ukuhani, uwezo wako wa kutoa toka hazina hii ya kiroho ambayo Bwana ameiandaa utaongezeka.”2 Ninajua ahadi hizi toka kwa nabii wetu aliye hai ni za uhakika.

MUHTASARI

  1. Russell M. Nelson, “Hazina za Kiroho” Liahona, Nov. 2019, 77.

  2. Russell M. Nelson, “Hazina za KIroho” 79.