2021
Likituelekeza Sote kwa Yesu Kristo
Januari 2021


Likituelekeza Sote kwa Yesu Kristo

Maisha ni safari Liahona linaweza kusaidia

Picha
line drawing of Liahona

Mchoro wa Liahona na Beth M. Whittaker

Katika nyakati za Kitabu cha Mormoni, Bwana aliandaa Liahona ili kumsaidia Lehi na familia yake kuendelea katika safari yao. Ilikuwa ni “dira, ambayo ingewaonyesha njia iliyonyooka kwenda kwenye nchi ya ahadi” (Alma 37: 44).

Kama Lehi, sisi tumo safarini. Tutakuwa na kupanda na kushuka. Jua na dhoruba. Amani na maumivu. Lakini kupitia hayo yote, kuna kusudi la kiungu kwa sababu sisi tunao uwezo wa kiungu. Baba yetu wa Mbinguni hataki tu turudi kuwa pamoja Naye; Anataka sisi tuwe zaidi kama Yeye kupitia kwa Mwanawe, Yesu Kristo. Lakini wakati mwingine tunahitaji msaada.

Chini ya maelekezo ya manabii wanaoishi, lile gazeti la Liahona katika siku zetu limeudwa ili kutusaidia kujua njia na jinsi ya kuitembea. Kujifunza na kuishi injili ya Yesu Kristo kunatubadilisha. Na tutakapokuwa tumevuka majangwa yetu na bahari zetu, tutagundua kuwa kumfuata Yeye kupitia vyote jua na dhoruba kumemruhusu Yeye kutufanya sisi kuwa kile ambacho siku zote alijua tunaweza kuwa.

Endelea kusoma ili kujifunza zaidi kuhusu Liahona hii mpya.

Picha
photo collage of eight people

Picha ya mwanamke akiandika kutoka Picha za Getty; picha: safu ya pili kutoka juu (kushoto) na safu ya tatu kutoka juu (kulia) kutoka Picha za Getty

Gazeti kwa ajili ya Kila Moyo na Nyumba

Iwe unatoka Slovenia au Uhispania, Madagaska au Massachusetts, gazeti hili ni kwa ajili yako. Iwe unazungumza Kikorea au Kikribati; iwe nyumba yako ni ya matofali au mianzi; iwe ulibatizwa miaka 80 iliyopita au jana tu. Wenye ndoa, wasio na ndoa, wazee, vijana — kurasa hizi zinakuzungumzia na kukuakisi wewe. Ushuhuda wako, uzoefu wako, kaya yako ya imani. Hiyo ni baraka kubwa ya kuwa na gazeti moja la ulimwengu kwa ajili ya watu wazima. Linatuunganisha na kutukumbusha kwamba sisi sote ni wa familia ya ulimwengu wote na kanisa la ulimwenguni kote.

Basi njoo uungane nasi wakati sisi sote tunaposogea karibu zaidi na Yesu Kristo. Toleo moja kwa wakati, ukurasa mmoja kwa wakati. Pamoja na manabii na mitume wakituongoza, na Mwokozi mwenye upendo akitusaidia. Sisi sote. Pamoja.

Nini cha Kutarajia Kutoka kwenye Liahona hii mpya

Ujumbe kutoka kwa Manabii na Mitume

Picha
First Presidency

Gazeti la Liahona litaonyesha ujumbe kutoka kwa viongozi wa Kanisa katika wakati unaofaa zaidi. Ujumbe huu, uliochapishwa na ulio mtandaoni, utatuelekeza wote kwa Mwokozi.

Msaada zaidi kwa Waumini Wote

Hapo awali, baadhi ya waumini walipokea gazeti hilo mara chache tu kwa mwaka, kutegemeana na lugha yao. Sasa magazeti matatu ya Kanisa la ulimwenguni kote yatachapisha kila mwezi au kila mwezi mwingine kwa lugha zinazozungumzwa na asilimia 97 ya waumini.

Maudhui Zaidi ya KIDIJITALI

Picha
phone screen with Gospel Library

Ili kukusaidia wewe upate yaliyomo uyatakayo yenye kuvutia, tutakupatia katika njia unayopendelea. Tafuta matukio ya kidijitali yaliyoboreshwa kwenye liahona.ChurchofJesusChrist.org, katika app za Gospel Living na apps za Gospel Library, kupitia barua pepe, na kupitia chaguo nyingine ambazo bado zinakuja.

Kujifunza Injili ambayo Kitovu chake niNyumbani

Kila mwezi tutashiriki matukio, shughuli, na mafundisho ili kusaidia Watakatifu wa Siku za Mwisho kujifunza injili nyumbani na kuyafundisha kwa watoto na wapendwa wao.

Hadithi Halisi kutoka kwa Waumini Halisi

Picha
girl writing in notebook

Picha ya mwanamke akiandika kutoka Picha za Getty; picha: safu ya pili kutoka juu (kushoto) na safu ya tatu kutoka juu (kulia) kutoka Picha za Getty

Unaposoma matukio yenye kukuza imani kutoka kwa waumini kote ulimwenguni, imani yako mwenyewe itaimarishwa. Na utakumbushwa kwamba sisi ni wa kitu kikubwa zaidi kuliko kata yetu au tawi. Shiriki matukio yako kwenye liahona.ChurchofJesusChrist.org au tutumie barua pepe kwenye liahona@ChurchofJesusChrist.org.

Hadithi na Ujumbe kutoka Karibu na Nyumbani

Liahona inachapisha matoleo zaidi ya 60 ya kieneo ambayo ni pamoja na kurasa zilizoingizwa maalum kwa maeneo na lugha tofauti za kijiografia. Kurasa hizi za maeneo zinasaidia kukuunganisha wewe na Watakatifu, viongozi, na masuala simulizi, yaliyo karibu na nyumbani.