2022
Kubadili Ubishi kuwa Upendo
Machi 2022


“Kubadili Ubishi kuwa Upendo,” Liahona, Machi./Aprili 2022

Karibu kwenye Toleo Hili

Kubadili Ubishi kuwa Upendo

Picha
Yusufu wa Misri akipatana na kaka zake

Yusufu wa Misri, na Michael T. Malm

Wakati mwingine tunapitia migogoro katika mahusiano yetu. Kujua jinsi ya kubadili migogoro yenye uharibifu kuwa migogoro yenye kujenga ni muhimu sana kwa ustawi wetu. Walakini hakika tunahangaika kwenye hilo.

Migogoro ya uharibifu inatulemea sana. Ubishi unaenea haraka sana. Chaguzi zetu huonekana kuwa na ukomo. Tunajihisi tu dhaifu na wenye wasiwasi. mahusiano yaliyovunjika na jamii zilizogawanyika zinaachwa nyuma kwenye kifusi.

Lakini tunaweza pia kujiingiza katika migogoro yenye kujenga, ambapo tunaweza kupata uhuru kutokana na uhasi wa ubishi. Tunaweza kukuza haki na rehema, kuimarisha mahusiano yetu, na kutatua matatizo yaliyokita mizizi. Amani inawezekana—katika mahusiano yetu na jamii zetu.

Kama mpatanishi wa migogoro, mume, na baba, nimegundua kwamba injili ya Yesu Kristo inaweza kutuletea nuru na nguvu inayohitajika kubadili ubishi kuwa upendo.

Katika toleo hili utasoma juu ya jinsi Yakobo, Esau, na Yusufu walivyoweza kupatanisha migogoro katika familia zao na jinsi sisi tunavyoweza kufanya vivyo hivyo katika nyumba zetu na jamii zetu (ona ukurasa wa 20). Utapata pia kusoma makala yenye kugusa moyo ya Mzee D. Todd Christofferson kuhusu jinsi dhiki inavyoweza kututakasa sisi ikiwa tutamwendea Bwana kwa ajili ya msaada (ona ukurasa wa 6).

Wengi wetu tunabeba maumivu mengi juu ya mahusiano yaliyovunjika nyumbani na ulimwenguni. Natumaini toleo hili linatoa tumaini kwa wale ambao wanahisi kama mapatano hayana maana, kwamba linachochea imani kwamba hatuko peke yetu, na muhimu zaidi, ni kwamba tunahisi upendo wa Yesu Kristo kwa njia ambayo inabadilisha sio tu mioyo yetu bali pia mioyo ya wale ambao tunapambana nao pia.

Kwa ukunjufu,

Chad Ford

Profesa katika kozi ya Ukuzaji wa Amani miongoni mwa Tamaduni, Chuo Kikuu cha Brigham Young–Hawaii