2022
Mifanano kati ya Yusufu wa Misri na Yesu Kristo
Machi 2022


“Mifanano kati ya Yusufu wa Misri na Yesu Kristo ,” Liahona, Machi./Aprili 2022

Njoo, Unifuate

Mwanzo 37–50

Mifanano kati ya Yusufu wa Misri na Yesu Kristo

Agano la Kale lina unabii mwingi, hadithi, na ishara nyingi ambazo ni kielelezo cha maisha na huduma ya Mwokozi, Yesu Kristo. Moja ya hadithi hizi ni ile ya Yusufu wa Misri.

Picha
picha tofauti, kama vile kondoo na mkate, kwa ajili ya kuonyesha mifanano kati ya Yusufu wa Misri na Yesu Kristo

Kielelezo na Andrew Colin Beck

Yusufu wa Misri

Yesu Kristo

Yusufu alikuwa mchunga kondoo (ona Mwanzo 37:2).

Moja ya majina ya Kristo ni “mchungaji mwema” (Yohana 10:11).

Yusufu aliuzwa kama mtumwa kule Misri (ona Mwanzo 37:26–28).

Yesu alisalitiwa kwa vipande 30 vya—fedha bei ya mtumwa (ona Kutoka 21:32; Mathayo 26:15).

Kaka zake Yusufu hawakumtambua walipokuja Misri kununua chakula (ona Mwanzo 42:7–8).

Watu wa Kristo hawakumtambua Yeye kama ni Mwokozi (ona Luka 4:22, 28–29; Yohana 1:10).

Yusufu alijionyesha kwa kaka zake walipokuja kuzungumza naye kwa mara ya pili (ona Mwanzo 45:1–5).

Kristo atajionyesha kwa Israeli wakati wa Kuja Kwake Mara ya Pili (ona Mathayo 24:30–31; Mafundisho na Maagano 88:104).

Kwa kufuata maelekezo ya Mungu, Yusufu alikuwa na mikate ya kutosha kuiokoa Misri kutokana na njaa (ona Mwanzo 47:13–19).

Yesu Kristo ni “mkate wa uzima” (Yohana 6:35; pia ona mstari wa 51).