Maandiko Matakatifu
Moroni 8


Mlango wa 8

Ubatizo wa watoto wachanga ni uovu wa machukizo—Watoto wachanga wameokolewa na Kristo kwa sababu ya Upatanisho—Imani, toba, unyenyekevu na upole wa moyo, kupokea Roho Mtakatifu, na kuvumilia hadi mwisho yanaelekeza kwa wokovu. Karibia mwaka 401–421 B.K.

1 Barua ya baba yangu Mormoni, iliyoandikwa kwangu, Moroni; na iliandikwa kwangu mara baada nilipoitwa kwa huduma. Na kwa njia hii aliniandikia, akisema:

2 Mwana wangu mpendwa, Moroni, ninafurahi sana kwamba Bwana wako Yesu Kristo amekuwa mwangalifu kwako, na amekuita kwa huduma yake, na kwa kazi yake takatifu.

3 Ninakukumbuka wewe kila siku katika sala zangu, siku zote nikisali kwa Mungu Baba katika jina la Mtoto wake Mtakatifu, Yesu, kwamba yeye, kupitia kwa uzuri wake na neema usio na mwisho, atakulinda kupitia uvumilivu wa imani kwa jina lake milele.

4 Na sasa, mwana wangu, ninakuzungumzia kuhusu lile ambalo linanisikitisha sana; kwani ninasikitishwa kwamba ugomvi unaweza kutokea miongoni mwenu.

5 Kwani, ikiwa nimejulishwa ukweli, kumekuwa na ugomvi miongoni mwenu kuhusu ubatizo wa watoto wenu wachanga.

6 Na sasa, mwana wangu, ninataka ufanye kazi kwa bidii, ili hili kosa kubwa litolewe miongoni mwenu; kwani, kwa kusudi hili nimeandika hii barua.

7 Kwani mara moja nilipojua vitu hivi kuwahusu nilimwuliza Bwana kuhusu jambo hili. Na neno la Bwana lilinijia kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, likisema:

8 Sikiliza maneno ya Kristo, Mkombozi wako, Bwana wako na Mungu wako. Tazama, nilikuja duniani sio kuwaita walio na haki bali wenye dhambi kwenye toba; wenye afya hawahitaji tabibu, bali wale walio wagonjwa; kwa hivyo, watoto wachanga ni wazima, kwani hawana uwezo wa kutenda dhambi; kwa hivyo laana ya Adamu imetolewa kwao ndani yangu, kwamba haina uwezo juu yao; na sheria ya kutahiriwa imeisha kwa ajili yangu.

9 Na katika njia hii Roho Mtakatifu alidhihirisha neno la Mungu kwangu; kwa hivyo, mwana wangu mpendwa, ninajua kwamba ni mzaha wa unadhiri mbele ya Mungu, kwamba mbatize watoto wachanga.

10 Tazama ninakwambia kwamba kitu hiki utafundisha—toba na ubatizo kwa wale ambao wanawajibika wenye uwezo wa kutenda dhambi; ndiyo, fundisha wazazi kwamba lazima watubu na wabatizwe, na wajinyenyeze kama watoto wao wachanga.

11 Na watoto wao wachanga hawahitaji toba yoyote, wala ubatizo. Tazama, ubatizo upo katika toba ili kutimiza amri kwa msamaha wa dhambi.

12 Lakini watoto wachanga ni wazima katika Kristo, hata kutokea mwanzo wa dunia; ikiwa si hivyo, Mungu ni Mungu wa upendeleo, na pia Mungu wa kugeuka, na mwenye kupendelea watu; kwani ni watoto wangapi wachanga wamekufa bila kubatizwa!

13 Kwa hivyo, ikiwa watoto wachanga hawangeweza kuokolewa bila ubatizo, hao lazima wangeenda kwenye jehanamu ya milele.

14 Tazama ninawaambia, yule ambaye anadhani kwamba watoto wachanga wanahitaji ubatizo yuko kwenye nyongo chungu na katika kifungo cha uovu; kwani hana imani, wala tumaini, wala hisani; kwa hivyo, ikiwa atakufa kama bado anafikiria hivyo, ataenda jehanamu.

15 Kwani kutisha ni uovu kudhani kwamba Mungu huokoa mtoto mmoja kwa sababu ya ubatizo, na mwingine lazima aangamie kwa sababu hakubatizwa.

16 Laana iwe kwa wale ambao wataharibu njia za Bwana kwa utaratibu huu, kwani wataangamia wasipotubu. Tazama, naongea kwa ujasiri, nikiwa na uwezo kutoka kwa Mungu; na siogopi kile watu wanachoweza kufanya; kwani upendo ulio kamili hutupa nje hofu.

17 Na nimejaa na hisani, ambayo ni upendo usio na mwisho; kwa hivyo, watoto wote ni kama mimi; kwa hivyo, ninapenda watoto wachanga na upendo ulio kamili; na wote wako sawa na washiriki wa wokovu.

18 Kwani najua kwamba Mungu si Mungu wa kupendelea, wala kiumbe kinachobadilika; lakini habadiliki kutoka milele hadi milele yote.

19 Watoto wachanga hawawezi kutubu; kwa hivyo, ni uovu wa kutisha kukana rehema safi ya Mungu kwao, kwani wote ni wazima ndani yake kwa sababu ya rehema yake.

20 Na yule anayesema kwamba watoto wachanga wanahitaji ubatizo anakana huruma za Kristo, na huweka bure upatanisho wake na nguvu ya ukombozi wake.

21 Ole kwa hawa, kwani wako katika hatari ya kifo, jehanamu, na maumivu ya milele. Ninazungumza kwa ujasiri; Mungu ameniamrisha. Yasikilize na uyafuate, au yatatumiwa kwako kwa kiti cha hukumu cha Kristo.

22 Kwani tazama kwamba watoto wote wachanga ni wazima katika Kristo; na pia wale wote ambao hawana sheria. Kwani nguvu ya ukombozi huja kwa wote ambao hawana sheria; kwa hivyo, yule ambaye hahukumiwi, au yule ambaye hayuko chini ya hukumu yoyote, hawezi kutubu; na kwa hao ubatizo hauleti chochote—

23 Lakini ni mzaha mbele ya Mungu, kukana huruma za Kristo, na nguvu za Roho Mtakatifu wake, na kuweka tumaini katika kazi zisizo na uhai.

24 Tazama, mwana wangu, kitu hiki kisifanyike; kwani toba ni kwa wale ambao wako chini ya hukumu na chini ya laana ya sheria iliyovunjwa.

25 Na matokeo ya kwanza ya toba ni ubatizo; na ubatizo huja na imani kwa kutimiza amri; na kule kutimiza amri huleta kusamehewa kwa dhambi;

26 Na kusamehewa kwa dhambi huleta unyenyekevu, na upole wa moyo; na kwa sababu ya unyeyekevu na upole wa moyo huja Roho Mtakatifu, Mfariji ambaye hujaza tumaini na upendo kamili, upendo ambao huvumilia kwa sala ya bidii, mpaka mwisho utakapokuja, wakati watakatifu wote watakapoishi na Mungu.

27 Tazama, mwana wangu, nitakuandikia tena ikiwa sitaenda nje tena mapema dhidi ya Walamani. Tazama, kiburi cha taifa hili, au watu wa Wanefi, kimeleta uangamizo wao isipokuwa watubu.

28 Waombee, mwana wangu, kwamba toba ije kwao. Lakini tazama, ninaogopa isiwe Roho amekoma kujitahidi nao; na katika sehemu hii ya nchi wanataka kuweka chini nguvu zote na mamlaka ambayo inatoka kwa Mungu; na wanamkana Roho Mtakatifu.

29 Na baada ya kukataa elimu kubwa hivyo, mwana wangu, lazima waangamie karibuni, kwa kutimiza unabii ambao ulizungumzwa na manabii, na pia maneno ya Mwokozi wetu mwenyewe.

30 Kwaheri, mwana wangu, mpaka nitakapokuandikia, au nitakapokutana nawe tena. Amina.