Misaada ya Kujifunza
Mpango wa Ukombozi


Mpango wa Ukombozi

Utimilifu wa injili ya Yesu Kristo, iliyo kusudiwa kumletea mwanadamu kutokufa na uzima wa milele. Unajumuisha Uumbaji, Anguko, na Upatanisho, sambamba na sheria zote zilizotolewa na Mungu, ibada, na mafundisho. Mpango huu hufanya uwezekano kwa watu wote kuinuliwa na kuishi pamoja na Mungu milele (2 Ne. 2; 9); Maandiko pia huonyesha mpango huu kama mpango wa wokovu, mpango wa furaha, na mpango wa rehema.