Misaada ya Kujifunza
TJS, Luka 17


TJS, Luka 17:21. Linganisha na Luka 17:20–21

Ufalme wa Mungu umekwisha kuja.

21 Wala wao hawatasema, Lo, hapa! au Lo pale! Maana, tazama, ufalme wa Mungu umekwisha fika kwenu.

TJS, Luka 17:36–40. Linganisha na Luka 17:37

Yesu alielezea mfano wa tai ili kufafanua kuhusu kukusanyika kwa watakatifu Wake katika siku za mwisho.

36 Nao wakajibu na kumwambia, Ni wapi, Bwana, watakakopelekwa?

37 Naye akawambia, Popote kundi kinapokusanyika; au, katika maneno mengine, kokote watakatifu wakusanyikapo, ndipo watakapokusanyika tai; au ndipo waliosalia watakapokusanyika pamoja.

38 Hili alizungumza, ili kuonyesha lile kusanyiko la watakatifu wake; na juu ya kushuka na kukusanyika wao waliosalia; mmoja kutoka kitandani, na mwingine kutoka kusaga na mwingine kutoka kondeni, na kutoka kokote yeye apendako.

39 Maana amini kutakuwepo mbingu mpya, na dunia mpya, ambamo ndani yake hukaa wenye haki.

40 Nako hakutakuwa na kitu kichafu; maana dunia itachakaa, hata kama vazi, na kwa sababu imeongezeka katika uharibifu, kwa hiyo itatoweka, na mahali pa kuwekea miguu patabaki pametakaswa, pameoshwa kutokana na dhambi zote.