Misaada ya Kujifunza
TJS, Luka 21


TJS, Luka 21:24–26. Linganisha na Luka 21:25–26

Yesu anasema juu ya baadhi ya ishara za ujio Wake.

24 Na sasa mambo haya aliyanena kwao, juu ya angamizo la Yerusalemu. Na ndipo wanafunzi wake wakamwuliza, wakisema, Bwana, tuambie juu ya kuja kwako?

25 Naye akawajibu, na akawaambia, Katika kizazi ambamo nyakati za Wayunani zitatimia, patakuwapo ishara katika jua, na katika mwezi, na katika nyota; na juu ya dunia dhiki ya mataifa pamoja na mkanganyiko, kama bahari na mawimbi yakinguruma. Nchi pia itahangaika, na maji ya kilindi kikuu yatahangaika;

26 Mioyo ya watu itakufa kwa sababu ya woga, na kwa sababu ya kutazamia mambo yale yajayo juu ya dunia. Maana nguvu za mbingu zitatikisika.

TJS, Luka 21:32. Linganisha na Luka 21:32

Yote yatatimia wakati nyakati za Wayunani zitakapotimizwa.

32 Amini ninakuambieni, kizazi hiki, kizazi cha nyakati za Wayunani kitakapotimia, hakitapita hadi yote yametimizwa.