Misaada ya Kujifunza
TJS, Luka 6


TJS, Luka 6:29–30. Linganisha na Luka 6:29–30

Yesu anafundisha kwamba ni bora kuvumilia mateso kuliko kupambana na adui.

29 Na akupigaye shavu moja, mgeuzie la pili, au, kwa maneno mengine, ni vyema kumgeuzia lingine, kuliko kutukana tena. Na akunyangʼanyaye joho lako, usimzuie kuchukuwa na kanzu yako pia.

30 Kwani ni vyema kumruhusu adui yako kuchukuwa vitu hivi, kuliko kushindana naye. Amini ninakuambia, Baba yako wa mbinguni aonae kwa siri atamleta yule muovu wako katika hukumu.