Misaada ya Kujifunza
TJS, Luka 9


TJS, Luka 9:24–25. Linganisha na Luka 9:24–25

Kupata utajiri wa kidunia hakustahili kuipoteza nafsi yako.

24 Kwani yeyote yule atakaye okoa maisha yake, lazima awe tayari kuyapoteza kwa ajili yangu; na yeyote yule atakaye kuwa tayari kuyapoteza maisha yake kwa ajili yangu, huyo atayaokoa.

25 Kwa kuwa inamfaa nini mtu kuupata ulimwengu wote, na bado hampokei yule aliyetawazwa na Mungu, na anapoteza nafsi yake mwenyewe, na yeye mwenyewe kutupiliwa mbali?