Misaada ya Kujifunza
TJS, Luka 3


TJS, Luka 3:4–11. Linganisha na Luka 3:4–6

Kristo atakuja kama unabii ulivyotolewaili kuleta wokovu kwa Israeli na kwa Wayunani, Katika utimilifu nyakati Yeye atakuja tena kuhukumu ulimwengu.

4 Kama ilivyoandikwa katika kitabu cha nabii Isaya; na haya ndiyo maneno yenyewe, akisema, sauti ya mtu aliaye nyikani, Itengenezeni njia ya Bwana, na yanyoosheni mapito yake.

5 Kwani tazama, na lo, atakuja, kama ilivyoandikwa katika kitabu cha manabii, kuzichukua dhambi za ulimwengu, na kuleta wokovu kwa mataifa ya wapagani, kuwakusanya pamoja wale waliopotea, ambao ni wa zizi la Israeli;

6 Ndiyo, hata wale waliotawanywa na kuteswa; na pia kutengeneza njia, na kuwezesha injili kuhubiriwa kwa Wayunani.

7 Na kuwa nuru kwa wote wakaao gizani, hata sehemu za mbali zaidi za dunia; na kuleta ufufuo kutoka kwa wafu, na kupaa juu, kukaa mkono wa kuume wa Baba,

8 Hadi utimilifu wa nyakati, na sheria na ushuhuda vitakapofungwa, na funguo za ufalme zitakaporudishwa tena kwa Baba;

9 Kutoa haki kwa wote; kushuka chini katika hukumu juu ya wote, na kuwathibitishia wote wasio mcha Mungu juu ya matendo yao yaliyo maovu, ambayo wameyatenda; na hii yote itatokea katika siku ile ambayo atakuja;

10 Maana ni siku ya uwezo; ndiyo, kila bonde litajazwa, na kila mlima na kilima vitasawazishwa; palipopinda patanyooshwa, na njia zilizo na mabonde zitasawazishwa;

11 Na wenye mwili wote watauona wokovu wa Mungu.

TJS, Luka 3:19–20. Linganisha na Luka 3:10–13

Masikini wanatunzwa kutokana na wingi wa pesa hazina. (Watoza ushuru) wasikusanye zaidi ya ilivyoelekezwa na sheria.

19 Kwani inajulikana vyema kwenu, Theophilus, kwamba kulingana na tabia za Wayahudi, na kulingana na desturi ya sheria yao katika kupokea pesa kutoka hazina, kwamba kutokana na wingi uliopokelewa, ulipangwa kwa masikini, kila maskini sehemu yake;

20 Na kwa njia hii watoza ushuru walifanya hivyo pia, kwa hiyo Yohana aliwaambia, Kamili sio zaidi ya kile ulichopangiwa.