2021
Haraka za kwenda Mkutano wa Sakramenti
Machi 2021


Haraka za kwenda Kwenye Mkutano wa Sakramenti

Nilidhania tutakosa sakramenti—tena.

Picha
loaf of bread

Picha kutoka Getty Images

Tulipohama kutoka Marekani kwenda Vietnam, mume wangu na mimi tuliazimia kutokosa kuhudhuria kanisa. Baada ya mwaka, hatukuwa tumekosa hata mkutano mmoja wa Jumapili, lakini mara nyingi tulichelewa na mara kwa mara kukosa sakramenti. Mkutano wetu wa sakramenti ulianza 2:30 asubuhi. Tukiwa na watoto watatu wadogo, kuwa tayari kwenda kanisani mara nyingi ilikuwa vigumu.

Kama familia tuliamua kwamba tulihitaji kuwahi kanisani kila wakati na kupokea sakramenti. Ilikuwa vigumu, lakini tuliwahi kwa Jumapili nne mfululizo. Nikaona tofuati iliyoletwa na juhudi zetu. Tulipata uzoefu mwingi wa kiroho katika juma.

Jumapili iliyofuata, hata hivyo, tuliamka kwa kuchelewa. Ilikuwa tayari ni saa 1:30 asubuhi. Nilimwambia mume wangu hapakuwa na tumaini la kuwahi, lakini nikafikiria kuhusu jinsi ambavyo tungeweza kubarikiwa kama tungefanya bidii kujiandaa vyovyote vile. Kwa hivyo, tulifanya upesi upesi!

Tulipofika kanisani, tulikuwa tumechelewa dakika 20. Nilihisi kwamba tulikuwa tumeanguka. Tulisikia watu wakiimba tulipoingia ndani, na nilipofungua mlango, mtu alikuwa anasimama kusali.

“Je, huo ulikuwa wimbo wa kufungua?” Nilimnog’onezea mmisionari aliyesimama mlangoni.

“Ndio,” alisema. “Tumechelewa kuanza leo.”

Nilishangaa. Nilifikiria tulikuwa tumeshindwa tena, lakini tulikuwa tumewahi kanisani! Machozi yalitiririka usoni mwangu nilipohisi upendo wa Baba wa Mbinguni kwa ajili ya familia yangu ndogo pamoja nami.

Baadaye tulijua kwamba wamisionari walipofika kanisani Jumapili hiyo, waligundua hakuna aliyebeba mkate wa sakramenti. Hakukuwa na duka karibu, na mkate ni vigumu kuupata huko Vietnam. Baada ya hofu ghafla, wamisionari walikumbuka kuwa walikuwa na mkate nyumbani.

Siku chache kabla, wazee walikuwa wamekuja nyumbani kwetu kwa chakula cha jioni. Jioni hiyo, niliwatengenezea mkate. Kanisa lilikuwa limechelewa kuanza Jumapili asubuhi hiyo kwa sababu wazee walikimbia kuleta mkate ambao niliwatengenezea.

Mungu huona juhudi zetu tunapojitahidi kutii amri Zake. Ingawa sisi wakati mwingine tunashindwa, Yeye anatupenda na ataandaa njia kwa ajili ya kufanikiwa kwetu—hata kama ni kuwahi kanisani.