2021
Ulimwengu Unahitaji Wanawake Waaminifu
Machi 2021


Karibu kwenye Toleo Hili

Ulimwengu Unahitaji Wanawake Waaminifu

Picha
illustration of Jane Manning James

Kielelezo na Toni Oka

Tangu siku za kwanza za Mama Hawa, wanawake wamechukua nafasi muhimu katika kusaidia kutimiza mpango wa Mungu kwa ajili ya watoto Wake. Mwezi huu, tuna nafasi kujifunza zaidi kuhusu baadhi ya wanawake ambao walikuwa waanzilishi katika siku za awali za Urejesho wa injili. Kwa mfano, kwenye ukurasa wa 16 tunaweza kusoma kuhusu Jane Manning James na mfano wake wa kushikilia ujasiri. Tunapojifunza Mafundisho na Maagano 25, tunasikia maneno ya Bwana kwa Emma Smith akimuomba atengeneze mkusanyiko wa nyimbo takatifu za dini.

Urejesho unaendelea katika siku yetu, na ulimwengu unahitaji michango mikubwa zaidi ya wanawake walio waaminifu kuliko awali. Kwenye ukurasa wa 12, unaweza kusoma jinsi wale kati yetu ambao wanatumikia kama Maafisa Wakuu katika Kanisa wameona nguvu za ukuhani zikifanya kazi katika maisha yetu. Hii nguvu ya ukuhani, inapatikana kwa wote wanaume na wanawake, ndiyo inayoruhusu kazi ya Mungu kuendelea duniani.

Bila kujali jinsia yetu, umri, kabila, au hali zingine, sisi sote ni watoto wapendwa wa Mungu wenye urithi wa kiungu na uwezekano wa kuwa.

Kwa moyo wa dhati,

Rais Joy D. Jones

Rais Mkuu wa Msingi