2021
Je, Kufagia Kulinifundisha Nini Mimi kuhusu Hali ya Kuwa Mzazi
Machi 2021


Msaada wa Malezi

Jinsi Kufagia Kulivyonifunza Kuhusu Uzazi

Mwandishi anaishi Utah, Marekani.

Kazi za watoto wangu zilisaidia kujibu maombi yangu.

Picha
children cleaning a floor with brooms and a mop

Kielelezo na David Green

Niliamka asubuhi moja nikihisi kuzidiwa. Wajibu wangu kama mzazi ulionekana kuwa mzito, na nikaelewa wazi madhaifu yangu. Kulionekana kuwepo kwa pengo kubwa kati ya matamanio yangu ya awali ya kuwa mzazi na jinsi hasa nilivyokuwa kwa sasa.

Nilipiga magoti na kusali na kumwambia Baba wa Mbinguni jinsi ninavyompenda Yeye. Nilimwambia jinsi ninavyowapenda watoto ambao Yeye ameibariki familia yetu kuwa nao. Na nilianza kumwambia Yeye jinsi nilivyokuwa nikijaribu kuwa mzazi mwema, lakini nilihisi kama sikuwa nikifanya kazi nzuri vya kutosha. Nilipokuwa nikisali, nilifikiria kuhusu jinsi watoto wangu wangekuwa wazuri kama Mungu angewalea Yeye Mwenyewe.

Kisha picha ikaja akilini mwangu. Nikawaona watoto wangu wakifagia sakafu ya jikoni. Hii ilikuwa mojawapo ya kazi nyingi walizokuwa wamepatiwa kufanya kusaidia familia yetu. Wakati mwingine kuwatazama wakifanya kazi hiyo kunanifanya nijikunyate kwa sababu wao bado wanajifunza na wanaruka sehemu nyingi. Lakini ninawaacha wafanye, pamoja na zile kazi zingine za kila siku, kwa sababu ninalo ono kubwa zaidi kwa ajili yao. Najua kwamba kupitia haya mazoezi yasiyo kamili, watajifunza na kukua. Hatimaye, wataweza kufanya upesi na kwa ustadi kama ninavyoweza mimi. Hilo ono kwa ajili yao la kuwa wenye kuwajibika na kujitegemea linaridhisha sana kuliko kama ningefanya kila kitu mwenyewe. Silei watoto wa ufanisi wa muda mfupi—ninajaribu kuwasidia kuwa na ufanisi wa maisha marefu.

Na nilishangaa kama labda kitu kama hiki ni kweli kwa wazazi wetu wa mbinguni pia. Baba wa Mbinguni anajua sisi hatuwezi kufanya kazi kamilifu ya kuwa wazazi. Vitu vingine tunavyofanya pengine humfanya Yeye ajikunyate, lakini Yeye huruhusu kwa sababu Anajua tunajifunza na kukua. Yeye ana mtazamo mkubwa na wa muda mrefu . Yeye hutuona siku moja tunakuwa mzazi kama Yeye, tukiweza kupenda kikamilifu, kufundisha kwa ufanisi, na kuwa mfano kwa ukamilifu. Tunapobabaisha, Yeye anajua tunakuza sifa kama vile subira na hisani. Na hivyo, katika hekima Yake, Yeye hutuacha tufanye na kushindwa na kujaribu tena.

Jinsi gani natamani ningekuwa mzazi kamili tayari! Kama Joseph Smith alivyoandika, kila mara najikuta nikianguka “katika makosa mengi ya kipumbavu” (Joseph Smith—Historia 1:28). Lakini napata faraja katika kujua kwamba Mungu anaelewa moyo wangu, ambayo inamaanisha Yeye anajua ninajaribu kuwa mwenye kufundishika. Ninahisi furaha wakati watoto wangu wanapouliza, “Ninawezaje kufanya vyema zaidi?” Na inaonekana kuwa wanataka kuwa bora. Angalau ninaweza kuwa hivyo kwa Baba wa Mbinguni.

Haya mawazo yote yakicheza akilini mwangu, nilikuwa na wakati mmoja wa kuvunjika moyo. “Lakini itakuwaje kama makosa yangu ya kuwa mzazi yanawaumiza watoto wangu?” Niliuliza. “Mimi sitaki kuwazuia, hata kama nitakuwa kitu cha ajabu katika mchakato huu.”

Tena, picha ya watoto wangu wakifagia ikaja akilini. Baada ya binti kujikakamua kupiga deki sakafu na kisha kuharakisha kwenda kucheza au kumalizia kazi nyingine, kwa kawaida mimi huosha sehemu zilizobaki zenye kunata. Na nikafikiria rehema na nguvu za Yesu Kristo zisizo na mwisho, ambazo Upatanisho wake unafunika kila moja ya hali za kunata za maisha. Neema Yake hufunika mapungufu yangu kama mzazi, kama vile neema Yake inavyofunika maumivu watoto wangu wanayopata kwa sababu ya mapungufu yangu. Katika njia ambayo hakuna kati yetu anayeweza kuelewa, Upatanisho Wake unaweza kuponya yote haya.

Napata faraja kubwa katika ufunuo binafsi niliopokea siku hiyo. Nilihisi Roho akinifundisha kwamba juhudi zangu bora, katika ubia na Bwana, zinatosha. Najua kwamba Baba wa Mbinguni ataendelea kufanya kazi katika maisha ya watoto wangu kidogo kidogo, kufanya kwa ukamilifu kile nisichoweza kufanya kwa ukamilifu. Kwa msaada Wake, watoto wangu siku moja wanaweza kung’ara wenyewe, na kwa uangavu kama vile Baba wa Mbinguni ndiye amewalea mwanzoni. Isipokuwa mpango Wake pia uweze kunibadilisha mimi katika mchakato huu—kunitakasa na kunifinyanga ili niwe kama Yeye. Ee jinsi gani ilivyo hekima ya Mungu wetu!