2021
Kufuatilia Utimilifu wa Kristo
Machi 2021


Kufuatilia Utimilifu wa Kristo

Kutoka katika hotuba ya ibada ya vijana wakubwa kutoka maeneo mengi, “Cheo cha Kimo cha Utimilifu wa Kristo,” ilitolewa huko Stanford, California, Marekani, Februari 8, 2020.

Msimu huu wa Pasaka, mwendee Yesu Kristo na utafute sauti Yake yenye sauti ya uhakikisho wa amani.

Picha
Jesus with arms outstretched

Usiogope, na Michael Malm

Naomba nitoe mawazo machache kuhusu swali binafsi la kila mmoja wenu mtakalofanya katika kutafuta “Cheo cha Kimo cha Utimilifu wa Kristo,” (ona Waefeso 4:13). Natumaini yatakuwa ya thamani fulani kwenu katika wakati huu wa ukuaji katika maisha yenu na katika hali mtakazojikuta.

Baadhi yenu mpo pale mnapotaka kuwa, au angalau mnajua pale mnapotaka kwenda katika maisha yenu. Baadhi yenu mnaonekana kuwa na baraka nyingi na chaguzi za kupendeza mbele yenu. Wengine wenu mnahisi, kwa muda na kwa sababu yoyote ile, hamna bahati na kuna njia chache za kuvutia zilizoko mbele yenu.

Lakini popote mnapoenda na vyovyote mtendavyo kupitia changamoto zenu katika kufika hapo, nawaomba mje kwa Mwokozi, Yesu Kristo, kama hatua muhimu ya kwanza katika kufika mwisho wa safari yenu binafsi, katika kupata furaha ya kibinafsi na nguvu, na katika kufikia hatima yenu na mafanikio (ona 1 Nefi 10:18; 2 Nefi 26:33; Omni 1:26; Mafundisho na Maagano 18:11).

Hayo yote yanaweza kuwa yenu kama jibu la swali “Umeenda wapi wewe?” (Musa 4:15) litakuwa “Popote ulipo, Bwana.”

Maisha yanaweza kuwa na changamoto. Tunayo maumivu na majuto na taabu halisi za kufanyia kazi. Tuna masikitiko na huzuni, panda shuka za kila aina. Lakini Bwana na manabii wameongea maneno ya kutia moyo ya kutosha kuhusu jinsi ya kukabiliana na shida hizo za kujaza shajara kubwa mno.

“Amani Ninawaachieni”

Maombi ya kufunga ya Mwokozi kwa wanafunzi Wake alipokuwa anasonga mbele kuyaendea maumivu na machungu ya Gethsemane na Kalvari ni ya kusisimua sana. Usiku huo, usiku wa mateso makubwa zaidi ambayo yamepata kufanyika katika ulimwengu au kamwe hayatapata kutokea, Mwokozi alisema: “Nawaachieni amani, nawapeni amani yangu. … Msifadhaike mioyoni mwenu, wala msiwe na woga.” (Yohana 14:27).

Ni mtazamo wa kushangaza wa maisha ulioje katika saa za mateso makali sana! Ni kwa jinsi gani Yeye anaweza kusema hivyo, Akikabiliana na kile Anachojua Anakabiliana nacho? Yeye anaweza kusema hivyo kwa sababu Yeye ndiye Kanisa na injili ya miisho yenye furaha! Kwetu sisi, ushindi tayari umepatikana. Yeye huchukua mtazamo mpana, Yeye anatushirikisha ile picha kubwa.

Nafikiria baadhi yetu, hata hivyo, bado tuna mtazamo wa asili wa urithi wa Kipyuritani unaosema ni makosa kwa namna fulani kufarijiwa au kusaidiwa, kwamba tunapaswa kuwa wenye huzuni kwa kitu fulani maisha yetu yote. Mimi nasema kwamba “kujipa moyo” (Yohana 16:33) katika utafutaji wa “cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo” (Waefeso 4:13) kunaweza kuwa amri ambayo hata katika mioyo ya Watakatifu wa Siku za Mwisho ikiwa haifuatwi karibia ulimwenguni kote; na bado kwa hakika hakuna kitu kinachoweza kuhuzunisha sana moyo wenye rehema wa Bwana.

Ninao wasiwasi kama ambavyo ningekuwa kama mahali fulani katika maisha yao, mmoja wa watoto wangu angekuwa kwenye shida au kukosa furaha au kutokuwa mtiifu, hata hivyo ningevurugwa sana milele kama ningehisi kwamba wakati kama huyo mtoto hangeweza kuniamini nisaidie au angefikiria masilahi yake si muhimu kwangu au asingekuwa salama mikononi mwangu.

Katika roho hiyo hiyo, ninaamini kwamba hakuna yeyote kati yetu anayeweza kuthamini jinsi inavyouumiza sana moyo wa Mungu Baba au Mwanawe, Mwokozi wa ulimwengu, wanapojua kwamba watu hawajisikii kujiamini mikononi Mwao au hawako salama mikononi Mwao au hawaamini katika amri Zao. Rafiki zangu, kwa sababu hiyo pekee, tunao wajibu wa kuwa na furaha!

“Neema Yake Inatosha”

Kipande kingine cha ushauri kuhusu kumtafuta Kristo na cheo cha utimilifu Wake kilitokea baada ya Yesu kutenda muujiza wa kuwalisha watu 5000 kwa vipande vitano vya mikate na samaki wawili (ona Mathayo 14:13–21). (Zaidi ya hayo, usijali kuhusu Kristo kupungukiwa na miujiza ya kukusaidia wewe. “Neema yake inatosha” [2 Wakorintho 12:9]. Hilo ni somo la milele, la muujiza huu wa kiroho. Yeye ana baraka nyingi za kutolewa na mabaki ya vikapu tele kadhaa. Kuwa mwenye kuamini na ufurahie toleo Lake la “mkate wa uzima”! [Yohana 6:35].)

Baada ya Yesu kulisha umati, Aliwaaga na kuingia na wafuasi Wake kwenye mashua ya kuvua samaki kuvuka ng’ambo nyingine ya Galilaya. Kisha Yeye “alipanda mlimani faraghani kwenda kuomba” (Mathayo 14:23).

Wanafunzi walipokuwa wakipanda chombo chao, ilikuwa jioni, usiku ulikuwa na tufani. Upepo lazima ulikuwa mkali kuanzia mwanzoni. Kwa sababu ya upepo, hawa watu yawezekana labda walikuwa hawajatweka matanga bali walipiga makasia tu—na ilikuwa kazi ngumu kweli.

Tunajua haya kwa sababu ya muda wa “zamu ya nne ya usiku” (Mathayo 14:25)—kati ya saa 9:00 na 12:00 alfajiri—walikuwa wamesafiri maili chache tu (ona Yohana 6:19). Wakati huo chombo kilitaabishwa na tufani kali sana.

Lakini, kama kawaida, Kristo alikuwa anawachunga. Alipoona shida yao, Mwokozi kwa urahisi alichukua hatua ya moja kwa moja kuelekea kwenye chombo chao, akitembea juu ya mawimbi ili kuwasaidia.

Picha
Jesus Christ helping Peter up out of the stormy seas

Mkamilishaji wa Imani na J. Alan Barrett

“Msiogope”

Katika wakati wa mfadhaiko mkuu, wanafunzi walitazama na wakaona gizani joho likipepeapepea likiwajia juu ya matuta ya bahari. Wakapiga yowe kwa hofu ya walichokiona, wakifikiria ilikuwa ni zimwi juu ya mawimbi. Kisha, katika tufani na giza—wakati bahari ilionekana kuwa kubwa sana na chombo kuonekana kidogo sana—hapo ikaja sauti kwa mbali na yenye uhakika ya amani kutoka kwa Bwana wao: “Ni mimi; msiogope” (Mathayo 14:27).

Hadithi hii ya kimaandiko inatukumbusha kwamba katika kuja kwa Kristo, kutafuta utimilifu Wake, au katika kuja kwetu Kwake ili kutuletea utimilifu huu, hatua ya kwanza inaweza kutujaza na kitu fulani kama vile taharuki kuu. Haipaswi kuwa hivyo, lakini wakati mwingine hufanyika. Mojawapo ya kinyume kikuu cha injili ni kwamba chanzo chenyewe cha msaada na usalama tunachopatiwa ni kitu ambacho tunaweza, katika upofu wetu wa kidunia, kukikimbia.

Kwa sababu iwayo yoyote ile, nimewaona wachunguzi wakitoroka ubatizo. Nimeshawaona wazee wakitoroka wito wa kwenda misheni. Nimeshawaona wapenzi wakitoroka ndoa. Nishawaona waumini wakitoroka miito yenye changamoto. Na nimeshawaona watu wakitoroka uumuni wao wa Kanisa.

Mara nyingi tunatoroka vitu vile vile ambavyo vitatuokoa na kutupoza. Mara nyingi tunafikiria masharti ya injili kama kitu cha kuogofya na kushindwa kutelekeza.

Mzee James E. Talmage (1862–1933) alisema: “Katika kila maisha ya mwanadamu mkubwa huja matukio kama vile kupambana kwa wasafiri kwenye tufani kukiwa na mawimbi kinzani na bahari zinazotisha; mara nyingi usiku wa mapambano na hatari unasonga mbele kabla muokoaji hajatokea; na hivyo basi mara nyingi sana msaada okozi huonekena kimakosa kama tishio kubwa zaidi. [Lakini,] kama ilivyowajia [wanafunzi hawa] katikati ya maji yaliyochafuka, vivyo hivyo huja kwa wale wanaofanya kazi kwa bidii katika imani, sauti ya Mkombozi—‘Ni Mimi; msiogope.’”1

Njooni Kwake

Jambo la ajabu kuhusu huu mwaliko wa kumpokea Mwokozi, kuja Kwake na kutafuta utimilifu wa cheo Chake, ni kwamba kila mtu anaweza. Hii haimaanishi kila mtu unayemjua anataka kuzishika amri, au kwamba kila mtu unayekutana naye atazishika amri. Bali kile inachomaanisha ni kwamba inawezekana kuzishika amri bila kipawa maalumu au urithi wa kufanya hivyo.

Ninasii kwa upendo kwa ajili ya imani ambayo “inaangaza kwa uangavu na safi na imara,” kwa Mwokozi kuletwa “katika kila chembe ya utamaduni [wetu],”2 na kwa ajili ya kimo cha Kristo kuwa cheo kamili katika maisha yetu (ona Waefeso 4:13).

Maisha yatakupatia changamoto. Magumu yatakuja. Kuvunjika moyo kutatokea. Wapendwa watakufa. Kwa hiyo, popote uendapo, mwendee Yesu Kristo kwanza. Kumbukeni kwamba kuteseka na Kufufuka Kwake kunawezesha ushindi wetu juu magumu na kifo. Fanyeni maagano yenu Naye na myashike mnaposafiri.

Katika udhaifu wangu wote, ambao nimeukubali kabisa, natamani sisi tupokee “cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo.” Nataka Nije Kwake. Namtaka Yeye, kama inawezekana, aje kwangu. Na kwa kweli nawatakieni hiyo baraka ninyi nyote.

Muhtasari

  1. James E. Talmage, Jesus the Christ (1916), 337

  2. Eric Metaxas, Bonhoeffer: Pastor, Martyr, Prophet, Spy (2010), 248.