2021
Kuongozwa na Bwana
Machi 2021


Kidijitali Pekee: Sauti za Watakatifu wa Siku za Mwisho

Kuongozwa na Bwana

Bwana anatujua sisi na kile kilicho sahihi kwetu sasa.

Picha
man and woman working together in kitchen

Picha na Cody Bell

Giselle

Kabla ya kufunga ndoa, André alikuwa na shughulikia shahada ya Udaktari wa Falsafa na akapata ajira kufanya kazi katika Chuo Kikuu cha Michigan. Tulifunga ndoa na kuhamia Michigan. Hatimaye, André alianza kupata shida kazini na akataka kubadili kazi.

Tulikuwa vijana, tulikuwa ndio tumefunga ndoa tu, na hatukujua nini cha kufanya. Tuliamua kusali kuhusu jambo hili.

André

Siku moja, nilienda chuoni na kusoma ubaoni ambapo nafasi za kazi zilizokuwepo hutangazwa. Nilituma maombi kwa kazi tatu tofauti. Katika juma moja, nilipata kazi zote tatu.

Giselle

Tulishangaa tutafanya nini. Tukasali Tena Kazi moja ilikuwa Uingereza, lakini tulikuwa tunataka kukaa Marekani,. Moja ilikuwa Texas, na nyingine ilikuwa Maryland karibu na Washington, D.C. Kazi katika Maryland ilikuwa ya NASA André ni mwanasayansi, kwa hiyo NASA ilionekana kama mahali pazuri pa kwenda.

André

Tukiwa njiani kwenda Maryland, nilikuwa ninaendesha gari hali Gisell analala. Iilikuwa mapema alfajiri wakati nilipoona Hekalu la Washington D.C.

“Amka! Amka! Je, unaweza kuona?” Nikamwambia Giselle. “Ni kama Kasri!”

Giselle

Nilimwambia André kwamba labda tunaweza kwenda kulitembelea siku moja. Hatukujua ilikuwa ni nini. Siku chache baada ya kuwasili Maryland, nilienda kwenye maktaba kutumia internet kutuma maombi ya kazi na kuangalia barua pepe.

Mwanamke ambaye alikuwa anafanya kazi hapo alisikia lahaja yangu na kuniuliza natokea wapi. Nikamwambia natokea Brazili na tukaanza kuongea. Jina lake lilikuwa Edna. Nikamwambia tumehamia kutoka Michigan na nikataja mahali tulipoishi.

“Ninaishi katika nyumba hizo hizo,” Edna alisema.

Wakati nilipoenda kwenye maktaba siku iliyofuata, Edna alisema, “Nimefurahia kuwa umerudi tena. Ninataka kuwaalika wewe na mume wako nyumbani kwangu kwa chakula cha jioni.”

Nikafikiria hii si kawaida kwa sababu hakunijua. Kisha akasema, “Nilisali kuhusu ninyi kwa sababu nilihisi kitu maalum sana wakati nilipokutana na wewe jana.”

Tulienda nyumbani kwake na kujua kwamba mume wake alikuwa amefariki dunia hivi karibuni. Baada ya chakula, alipiga kinanda wimbo wa “Lord, I Would Follow Thee,”Nyimbo za Dini, na. 220. Alisema ulikuwa ni wimbo pendwa wa mumewe na ulipigwa katika siku ya mazishi yake. Kisha akatwambia kuhusu mpango wa wokovu na kutualika twende kanisani pamoja naye.

Tulienda kanisani, na watu walikuwa wakarimu sana. Tuliamua kwenda Jumapili iliyopita. Tulikubali kujifunza masomo ya umisionari. Edna alijitolea masomo yafanyike nyumbani kwake. Kwa miezi mitano tulikwenda kanisani kila Jumapili. Mioyo na roho zetu zilikuwa zinaandaliwa kwa ajili ya ubatizo.

André

Wakati ubatizo wetu ulipotangazwa, kila mtu alionekana kushangaa. “Ala, hamkuwa waumini?” walisema. “Lakini mlikuwa hapa kila juma!” Ubatizo wetu ulikuwa maalum. Karibu kata nzima ilihudhuria.

Tuliunganishwa katika Hekalu la Washington D.C. mwaka mmoja baadae. Wakati tulipoenda hekaluni, tuligundua kwamba ndiyo lilikuwa lile kasri tuliyoiona mwaka mmoja kabla!

Giselle

Baada ya sisi kuunganishwa hekaluni, vitu vingi havikuwa vinaenda sawa.

Baada ya Septemba 11, 2001, ilikuwa vigumu kwetu kupata upya visa zetu. Nilihuzunika kwa sababu nilikuwa nimehitimu kutoka kwa chuo cha jumuiya na kuomba msaada wa masomo katika Chuo cha Maryland. Sikupata msaada wa masomo, na maabara ambayo André alikuwa anafanya kazi ilikuwa inafungwa.

Tukafikiria kwamba labda ni wakati wetu wa kurudi Brazili.

André

Askofu wetu alituambia tungeweza kusaidia waumini wengi huko Brazili na kukua katika njia ambazo hatuwezi hapa Marekani. Alitushauri tubaki karibu na Kanisa.

“Nendeni Brazili na mkamtumikie Bwana,” alisema.

Baada ya kuishi Brazili kwa muda, rais wetu wa kigingi alikuja nyumbani kwetu na kuniita nitumikie kama askofu. Kwa njia fulani nilijua nitaitwa. Kwa siku kadhaa kabla ya wito wangu, sikuweza kulala. Mimi nilikuwa nafikiria na kujifunza.

Giselle

Nilijiuliza ni nini kilikuwa kinaendelea. Nilimwona akibadilika kabla ya wito wake.

André

Nilipoanza wito wangu, kata yetu ilikuwa na waumini hai 80. Wakati nilipopumzishwa, wengi zaidi walihudhuria kanisa kila mara, na wamisionari 12 walienda misheni kutoka kata yetu. Ilikuwa nzuri!

Wakati nilipopumzishwa, Rais Dieter F. Uchtdorf, alipumzishwa kutoka katika Urais wa Kwanza. Nakumbuka Rais Russell M. Nelson akisema kwamba Rais Uchtdorf alikuwa na majukumu muhimu mapya katika Akidi ya Mitume Kumi na Wawili.

Miezi mitatu baadaye, nilitwa kama mshauri wa kwanza katika urais wa misheni. Sikutumikia misheni, lakini naupenda wito wangu. Napenda kufanya kazi na wamisionari. Bwana ananijua. Alijua nilihitaji kupumzishwa kama askofu ili niweze kutumikia katika wakati na sehemu iliyokuwa sawa kwangu sasa.