2022
Wana Kitabu cha Mormoni Hapa!
Januari/Februari 2022


Sauti za Watakatifu wa Siku za Mwisho

Wana Kitabu cha Mormoni Hapa!

Nilipokishika Kitabu cha Mormoni katika mikono yangu, nilihisi mizigo yangu imefanywa rahisi katika upendo mkarimu wa Mwokozi.

Picha
hand holding a copy of the Book of Mormon

Picha na Jacob A. Brown

Mnamo Jumamosi katikati ya majira ya baridi, mimi na mke wangu tulitumia vizuri siku yenye jua kali japo yenye baridi kupata kuujua vyema ujirani wetu. Tulikuwa punde tu tumehama maelfu ya maili kutoka kwenye mji wetu kwenda Pwani ya Mashariki ya Marekani kutafuta fursa za elimu na kazi.

Tuliamua kutembea kwenda kwenye chuo kikuu kilicho karibu ambacho hakuna kati yetu aliyewahi kukitembelea. Baada ya muda tulipata maktaba kuu ya chuo kikuu. Tunapenda kusoma, na mke wangu, mwanafunzi mhitimu, alikuwa mdadisi kuona ni rasilimali zipi angepata kwa ajili ya masomo yake. Kwa sababu alikuwa akijifunza historia ya dini, tulivinjari kwenye sehemu ya rundo la vitabu vya dini. Tulipotazama baadhi ya vichwa vya habari vyenye mvuto, kitabu kidogo chenye jalada linalofahamika la samawati kilivuta jicho langu.

“Wana Kitabu cha Mormoni Hapa!” Kwa msisimko nilinong’ona.

Nilichukua kitabu kutoka kwenye rafu. Ilikuwa nakala ya zamani sana na nilijiuliza imekuwepo hapo kwa muda gani. Kilichovuta umakini wangu hasa kilikuwa ingizo dogo lililogundishwa ndani ya jalada la mbele.

Ingizo lilikuwa ushuhuda mfupi wa wanandoa kutoka Blackfoot, Idaho, Marekani. Katika ushuhuda wao, walielezea kitabu cha Mormoni ni nini na kwa nini ni cha muhimu. Walishiriki ushuhuda mfupi lakini wenye nguvu kuhusu kitabu na walimwalika msomaji kuomba ili kujua ikiwa kilikuwa cha kweli.

Maneno yao yalikuwa rahisi, lakini ujumbe wao ulikwenda moja kwa moja ndani ya moyo wangu. Pengine wanandoa hawa walikusudia ushuhuda wao usomwe na wale wasio wa imani yetu. Pengine walimpa nakala hii mtu waliyemfahamu. Nani ajuaye ni mara ngapi imebadilishwa mikononi au maili kiasi gani imesafiri mpaka kufika kwenye maktaba ya chuo kikuu?

Nilipokishikilia kitabu mikononi mwangu, Roho alijaza moyo wangu. Kwa muda, nilihisi mizigo yangu imefanywa rahisi katika upendo mkarimu wa Mwokozi.

Sike ile ndani ya maktaba inaendelea kunikumbusha baraka ninazopokea kwa kusoma Kitabu cha Mormoni na za umuhimu wa kushiriki ushuhuda wangu wa Kitabu cha Mormoni. Shuhuda zetu zinaweza kuanguka “kwenye mwamba” au “kwenye udongo mzuri” (ona Mathayo 13:3–9), lakini ni muhimu tuzishiriki. Mungu atahakikisha zinafika kwa muda sahihi, mahali sahihi na kwa watu sahihi.