2022
Phnom Penh, Kambodia
Januari/Februari 2022


Kanisa Liko Hapa

Phnom Penh, Kambodia

Picha
photograph of Phnom Penh, Cambodia

Kushoto: picha na Leslie Nilsson; kulia: picha na Cody Bell

Watoto wakicheza na boti zikielea kando ya Mto Mekong, pamoja na anga la Phnom Penh kwa nyuma. Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho lilipata utambulisho wa kisheria huko Kambodia mnamo 1994. Leo, Kanisa katika nchi hii lina:

  • Waumini 15,200 (kwa makadirio)

  • Vigingi 2, misheni 1, mikusanyiko 28

  • Hekalu 1 lililotangazwa

Inayolenga Nyumbani, Inayosaidiwa na Kanisa

Picha
husband and wife sitting in front of house

“Mtaala wa Njoo, Unifuate unatusaidia kuwa na majadiliano ya mara kwa mara katika nyumba zetu,” anasema Kem Chhoeun wa Krong Ta Khmau. “Tunajikuta tukizungumza kuhusu injili kila siku,” anasema mkewe, Tep Saroeun.