2022
Mwanzo na Agano la Kale
Januari/Februari 2022


Karibu kwenye Toleo Hili

Mwanzo na Agano la Kale

Picha
Jesus Christ with stars in background

Kristo na Uumbaji, na Robert T. Barrett

Ni mwanzo wa mwaka mpya, ambapo inaonekana kama vile ni muda muafaka hasa kufikiria kuhusu mwanzo.

Mwaka huu, Agano la Kale na Lulu ya Thamani Kuu vitatupeleka kwenye safari ya baadhi ya mwanzo muhimu na wenye kupendeza ujulikanao kwa mwanadamu.

Tunaweza kumjua Yesu Kristo vizuri zaidi, ambaye alikuwa pamoja na Baba “hapo mwanzo” (Ibrahimu 4:1). Tunaweza kusoma kuhusu Uumbaji wa ulimwengu na mwanzo wa maisha ya duniani. Tunaweza kujifunza kuhusu mwanzo wa toba, familia, amri na ibada za hekaluni hapa duniani. Tunaweza kujifunza mwanzo wa maagano matakatifu ambayo yanaendelea kuyapa umbo maisha yetu leo.

Na ikiwa bado hatulipendi Agano la Kale, leo inaweza kuweka mwanzo wa msimu mpya wa kujifunza na utafiti. Kwenye ukurasa wa 20, ninashiriki baadhi ya kweli ambazo zilinisaidia mimi kuwa na shauku zaidi kuhusu kitabu hiki cha maandiko na kutazama mafundisho yake kwa nguvu mpya na lengo jipya. Kwenye ukurasa wa 26, Rais Mark L. Pace, Rais Mkuu wa Shule ya Jumapili, anaainisha baraka zenye nguvu tunazoweza kupokea ikiwa tuko radhi kusoma “kwa dhamiri na kwa sala.”

Zaidi ya kingine chochote, acha tukumbuke kwamba maisha yenye mwanzo mpya yanawezekana kwa sababu ya Yesu Kristo. Katika makala ya Mzee Quentin L. Cook kwenye ukurasa wa 6, anashuhudia kwamba “yote kamwe hayajawahi kupotea” kwa sababu Mwokozi wetu anatungojea kwa mikono iliyokunjuliwa. Kupitia neema yake, tunaweza kuendeleza safari ya kiroho waliyoianza mababu zetu miaka mingi iliyopita.

Ninatumaini mwaka huu umejaa mwanzo wa kupendeza kwa kila mmoja wetu!

Marissa Widdison

Mhariri Mtendaji Msaidizi, App ya Kuishi Injili

Picha
view of the earth from space

“Mimi ni Mwanzo na Mwisho, Mungu Mwenyezi; kwa njia ya Mwanangu wa Pekee niliviumba vitu hivi; ndiyo, hapo mwanzo niliumba mbingu, na dunia ambayo juu yake wewe umesimama.”

Picha kutoka Adobe Stock