2022
Kufanya Kuhudumu Kuwe na Tija
Januari/Februari 2022


Kanuni za Kuhudumu

Kufanya Kuhudumu kuwe na Tija

Ikiwa unajiuliza kama kuhudumu kwako kuna tija, fikiria mawazo haya.

Picha
woman hugging a young woman in a wheelchair

Ni rahisi kujiuliza ikiwa kuhudumu kwetu kunaleta tofauti, hasa wakati tunapokabiliana na changamoto zetu wenyewe.

Katika hatua yangu ya maisha kabla ya kuwa na kiti mwendo, nilipenda kuona karatasi ikipitishwa katika Kikundi cha Usaidizi. Mara nyingi nilijiandikisha kutoa huduma. Ilikuwa ni njia ya kuonesha utayari wangu wa “kubeba mizigo ya mmoja na ya mwingine” (Mosia 18:8.)

Halikuwa kosa la karatasi kwamba nisingeweza kujiandikisha tena. Kwa kweli, sikuweza kuandika kabisa jina langu. Kwa sababu ya ulemavu wangu, sikuweza hata kushikilia karatasi. Hakuna aliyetarajia mimi niandike jina. Lakini, oh, jinsi gani nilitaka kufanya hivyo! Huduma inatufunganisha na upendo wa Mungu na kutuunganisha kwa wengine. Nilihitaji sana hisia hiyo ya muunganiko mimi mwenyewe.

Kwa sababu nilihitaji watu wa kusaidia kunihudumia, huduma yangu haikuonekana kustahili juhudi ambayo ingehitajika kwa wengine kunisaidia. Karatasi ile ilikuwa ukumbusho wa kile ambacho nisingeweza tena kufanya—angalau mpaka dada yangu mhudumiaji alipoona tamanio langu.

Aliniuliza kile ambacho ningependa kufanya ili kuhudumu, si tu kile nilichohitaji nifanyiwe. Kisha aliandika jina langu kwenye karatasi. Alikuja nyumbani kwangu na kunisaidia kutengeneza vyakula ambavyo ningejitolea kuviandaa kwa ajili ya wengine. Kamwe hakuwahi kupendekeza kwamba nilikuwa na uhitaji mkubwa wa usaidizi mimi mwenyewe kiasi kwamba sikupaswa kujaribu kuwasaidia wengine. Alikuwa mwenye furaha kutumia muda pamoja nami.

Mwishowe, nilitambua juhudi zangu zilikuwa za kustahili. Kwa msaada wa dada yangu mhudumiaji, niliweza kufanya jambo. Ikiwa jambo hilo lilimaanisha kitu chochote kwa mtu mwingine au la, lilileta tofauti kwangu. Japokuwa halikunufaisha familia yangu moja kwa moja au kuponya mwili wangu, lilisaidia kuuponya moyo wangu.

EmRee Pugmire

Utah, Marekani

Kwa Msaada Wake, Wewe Ni Zaidi ya Unayetosha

Picha
the Old Testament prophet Enoch and people from the city of Zion

Mji wa Sayuni Ulitwaliwa, na Del Parson; picha ya lenzi ya kukuza vitu kutoka Getty Images

Ni kawaida kuhisi kutotosha kufanya kazi ya Bwana. Nabii Henoko alihisi hivyo pia. Wakati Bwana alipomwamuru awaite watu kwenye toba, alikuwa na hofu kwa sababu alikuwa “kijana mdogo, na watu wote wanichukia kwa maana mimi si mwepesi wa kusema” (Musa 6:31).

Lakini Bwana aliahidi kwamba angekuwa pamoja na Henoko na kwamba Roho Wake angekuwa juu yake na “maneno yako yote nitayahesabia … kuwa haki,” Bwana alitoa mwaliko, “tembea pamoja nami” (Musa 6:34).

Henoko alikuwa mtiifu kwenye kile Bwana alichoamuru na alikuwa ushawishi mkubwa kwa watu, si kwa sababu ya nguvu yake mwenyewe bali kwa sababu ya “nguvu, na lugha ambayo Mungu alimpa” (Musa 7:13).

Kanuni za Kuzingatia

Ikiwa unajiuliza kama kuhudumu kwako kuna tija, fikiria kanuni hizi:

  1. Kuelewa kuhusu kuhudumu na malengo yake kutatusaidia kutathmini juhudi zetu kwa usahihi zaidi.

    • Kuhudumu ni zaidi ya kujenga mahusiano imara; ni kuhusu kuwasaidia wengine kuimarisha uhusiano wao na mwokozi.1

    • Kuhudumu si tu jukumu; ni jinsi tunavyoishi maagano yetu ya kumtumikia Yeye kwa kujaliana.

    • Kuhudumu hakufuati mfumo ulioainishwa kabla. Kunatuvuta pale tunapoendana na hali na kutafuta mwongozo wa kiungu wa kuhudumu jinsi ambavyo Mwokozi angehudumu.

  2. Kuelewa jinsi Mungu anavyotazama kuhudumu kwetu kunaweza kubadili mtazamo wetu.

Ni Kipi Tunaweza Kufanya?

Badala ya kuhofia kuhusu kile usichoweza kufanya, kwa sala fikiria kile unachoweza kufanya. Kisha tenda. Unapotenda katika jina la Bwana, Yeye anaweza kukuza juhudi zako na kuzitumia kukubariki wewe pamoja na wengine (ona 2 Nefi 32:9).

Muhtasari

  1. Ona Russell M. Nelson, “Kuhudumu kwa nguvu na Mamlaka ya Mungu,” Liahona,, Mei 2018, 69–70.

  2. Kujifunza zaidi kuhusu Oliver Granger na jinsi Mungu anavyopima mafanikio yetu, soma Boyd K. Packer, “Wadogo wa Hawa,” Liahona, Nov. 2004, 86–88.

  3. Henry B. Eyring, “Inuka kwenye Wito Wako,” Liahona, Nov. 2002, 77.