2022
Mpangilio Imara kwa ajili ya Uzazi
Septemba 2022


“Mpangilio Imara kwa Ajili ya Uzazi,” Liahona, Sept. 2022.

Mpangilio Imara kwa Ajili ya Uzazi

Kutokana na kanuni za injili na msaada wa utafiti, mpangilio huu kwa ajili ya uzazi unaweza kusaidia kukuongoza katika kutengeneza uhusiano wa maana, kulea imani na ukuaji, na kujenga umoja na uthabiti ndani ya familia yako.

Picha
baba akisoma maandiko pamoja na binti yake

Kuwa mzazi kuna kusudi la milele na kunaweza kukupa thawabu, kukuelimisha, na kuwa shangwe. Lakini kwa sababu familia huja katika maumbo yote na ukubwa na zinakabiliana na changamoto zake za kipekee, kulea watoto kunaweza pia kuonekana kuzidiwa au ya kuchosha wakati mwingine

Bahati nzuri, hatupaswi kufanya haya pekee yetu.

Kwa mwongozo wa Baba wa Mbinguni, msaada wa Mwokozi na injili Yake, na matumizi kwa sala ya msaada wa ushauri wenye mwongozo wa kiungu, tunaweza kupata msaada na matumaini kwa ajili ya safari yetu ya uzazi.

Mpangilio Unaosaidiwa na-Injili kwa ajili ya Uzazi

Kuchota kutoka kwenye injili ya Yesu Kristo na msaada wa utafiti juu ya uzazi tumeweza kuzitambua kanuni tatu zenye kuongoza kwa ajili ya kulea maendeleo ya mtoto kimhemko na kiroho. Zinapoletwa pamoja, maeneo haya yanayohusiana ya msisitizo yanaunda mpangilio imara ambao unaweza kusaidia familia kote ulimwenguni.

Mpangilio huu ni wenye nguvu kwa sababu inaunganisha pamoja kweli za injili na mawazo yanayotokana na utafiti wa uzazi na maendeleo ya mtoto. Kutafuta ufunuo binafsi juu ya jinsi ya kutumia kanuni zilizomo katika mpangilio huu kunaweza kukusaidia kujenga uthabiti wa familia na kukuza nyumba ambayo Yesu Kristo ni kitovu chake.

Kanuni hizo tatu zinazoongoza ni:

  1. Tengeneza uhusiano wa upendo katika familia

  2. Kuza kujifunza na ukuaji

  3. Jenga umoja na nguvu kupitia huduma

Mpangilio huu unatusaidia sisi kufokasi kwenye mambo yaliyo muhimu zaidi. Kila sehemu ya mpangilio ni kiungo muhimu sana ambacho kinaiimarisha familia. Kufanya kazi pamoja, kunahimiza uhusiano chanya na uzoefu chanya, husaidia familia zetu kuvumilia dhiki, na kujenga uwezo na uthabiti.

Tunapokua kama wazazi, mpangilio huu unaweza kutumika kama mwongozo wenye msaada kwa ajili ya kugundua jinsi bora ya kufundisha na kumlea kila mtoto.

Hapa chini kuna muhtasari mfupi wa kila sehemu ya mpangilio na mfano kutoka katika maisha ya Mwokozi ili kutuongoza sisi katika kuutumia mpangilio huu katika maisha yetu. Taarifa zaidi za uzazi, vidokezo vilivyozoeleka, na majibu kwa maswali ya kila mara ya uzazi yanapatikana kwenye family.ChurchofJesusChrist.org.

Tengeneza Uhusiano wa Upendo katika Familia

Kanuni hii inatukumbusha sisi kuupa kipaumbele uhusiano wa upendo na Baba wa Mbinguni, na Mwokozi, mwenza wetu, na watoto wetu. Uhusiano huu wa kifamilia ni muhimu zaidi Utambulisho wa milele na uhusiano wa watoto wetu vinakua kutokana na ukweli muhimu kwamba “kila mmoja ni mwana na binti mpendwa wa wazazi wa mbinguni, na hivyo basi, kila moja ana asili na hatima ya kiungu.”1

Tunaweza kuwatia moyo ili waje wamjue Mungu na Yesu Kristo kupitia imani, sala, kujifunza maandiko, na ufunuo binafsi kutoka kwa Roho Mtakatifu (ona Yohana 17:3). Tunaweza kukuza imani kwa kustawisha “hamu ya kuamini” ya watoto wetu (Alma 32:27) na kwa kuwasaidia wauone upendo wa Mungu. Ni muhimu kwa watoto wetu kutambua kwamba Baba wa Mbinguni na Mwokozi wanawaelewa kikamilifu kabisa, wanawapenda kikamilifu, na wanataka kuwasaidia ili wafaulu (ona Warumi 8:38–39).2

Kama wazazi, ni muhimu kutengeneza uhusiano wa upendo na kila mtoto upendo ambao umejawa na uvuguvugu na uwezo wa kuhisi maono ya mwingine. Kuelewa mitazamo ya watoto wetu na kwa heshima kusikiliza yale wanayosema kunatengeneza uhusiano ulio salama na wenye wa upendo. Watoto wetu wanahitaji kujua kwamba sisi tunapendezwa na wao, tunajali jinsi wanavyojisikia, na tuko hapo ili kuwasaidia. Mwingiliano wetu wenye kujali na watoto wetu unawasaidia wao kukuza mtazamo chanya juu yao wenyewe, kutambua thamani yao ya milele, na kuunda uhusiano wa kuaminika na Mungu na Yesu Kristo.

Kwa nyongeza, wanafamilia wanaweza kuwa msaada mkubwa mmoja na mwingine. Tunaweza kukuza uhusiano wa kifamilia tunapokusanyika pamoja ili kuunganika, kusali, kushauriana na kuwa na burudani.

Mtazamie Kristo

Yesu Kristo anashiriki upendo Wake, na mmoja mmoja, kupitia uhusiano ambao unatoa kukubalika, matumaini, na uponyaji Baada ya Mwokozi kuwa amemaliza kuzungumza na Wanefi, kwa huruma Yeye aliwafikia na kuwahudumia kibinafsi kwa kuwaponya na kumbariki kila mmoja. Kwa upendo “aliwachukua [watoto] wadogo, mmoja mmoja, na kuwabariki, na akaomba kwa Baba kwa ajili yao” (3 Nefi 17:21).

Kama mzazi, unaweza kubariki watoto wako kwa kutengeneza uhusiano wa upendo pamoja nao—muunganiko mmoja wa maana kwa wakati.

Mawazo kwa ajili ya Kutengeneza Uhusiano wa Upendo katika Familia

  • Wasiliana na watoto wako kwa kuwa msikilizaji makini, jibu kwa upendo,fuata vidokezi vyao ili kukidhi mahitaji yao.

  • Stawisha imani katika Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo na himiza sala na ufunuo binafsi ili kuimarisha uhusiano huu mtakatifu.

  • Jijali wenyewe na ndoa yako. Hii itakusaidia wewe kuunganika vyema na watoto wako na kuwa mzazi pamoja na mwenza wako kwa umoja na upendo, kama wabia mlio sawa. Kama hujaolewa au kuoa, ongoza familia yako kwa imani na kujiamini. Tafuta msaada wa ziada kutoka kwa wale unaowaamini.

  • Kuza usalama, kukubalika, na shangwe nyumbani mwako.

2. Kuza Kujifunza na Ukuaji

Picha
wazazi wakiongea na binti yao

Kuza ukuaji wa watoto wako kwa kuthamini utu wao wa kipekee, ukiwapa upendo usiotingishika, na unga mkono jitihada zao. Gundua mahali walipo watoto wako katika maendeleo yao na fuatisha msaada wako ili utosheleze mahitaji yao maalumu. Mfano wako, maelekezo, mwongozo na kuwatia moyo kwako ni muhimu ili kulea uwezo na kujiamini kwa watoto wako. Uwe mdadisi na mwenye huruma kwa watoto wako wanapojifunza kupitia uzoefu.

Wazazi wanaolea pia waepuke kuwa wenye kudai sana, wenye kuruhusu sana, au wawezeshaji sana. Kutoa mipaka sahihi, ratiba za kila siku, na matarajio yenye kukubalika yatahamasisha ukuaji wa mtoto wako. Kama Baba yetu wa Mbinguni, wazazi wanapaswa kufokasi zaidi katika kuwezesha ukuaji wa watoto wao kuliko faraja yao (ona 2 Nefi 28:30; Mafundisho na Maagano 50:24, 40).

Onyesha njia, ongoza, na tembea kando ya watoto wako wanapokuwa wanajifunza kumfuata Yesu Kristo.3 Wafundisheni jinsi ya kumgeukia Mwokozi na kutegemea Upatanisho Wake ili kuwasaidia kukua. Watoto wako hatua kwa hatua watagundua kutokana na mfano wako na uzoefu wao wenyewe kwamba “ wanayaweza mambo yote katika Yeye(Kristo),” ambaye anawasamehe na kuwaimarisha (Wafilipi 4:13). Ukuaji na badiliko inaweza kuwa vigumu na inachukua mazoezi mengi. Wazazi wenye haki na wenye kukusudia wanajitahidi kuwafundisha watoto wao sio tu jinsi ya “kutembea katika njia ya kweli” (Mosia 4:15) bali pia kwa nini wanapaswa kufanya hivyo. Kuza uelewa wao na unga mkono matumizi yao ya haki ya kujiamulia kwa kila hatua wanayochukua

Mtazamie Kristo

Yesu Kristo anawezesha ukuaji wako kwa kutazama matamanio yaliyo ya haki ya moyo wako na kukusaidia kuyakamilisha (ona 1 Samweli 16:7; Enoshi 1:12). Bwana aliwauliza wanafunzi Wake “mmoja mmoja … : Ni kitu gani ambacho mnahitaji kutoka kwangu?” (3 Nefi 28:1; ona pia 1 Nefi 11:1–3). Kutafakari swali hili kunaweza kukusaidia kugundua na kukuza kile unachokithamini zaidi. Zingatia jinsi Mwokozi alivyokuza kujifunza na ukuaji ndani ya kaka wa Yaredi kwa kuheshimu haki yake ya kujiamulia na kumwuliza, “Ungetaka nifanye nini?” (Etheri 2:23). Bwana alimsaidia kwa kumpa maelekezo mahususi, yalipohitajika, lakini pia kwa kumtia moyo kufikiria mwenyewe kwa baadhi ya vitu yeye mwenyewe. Mwokozi hakulazimishi au kukudhibiti wewe lakini badala yake anakufundisha na kukushawishi utumie haki yako binafsi ya kujiamulia kwa manufaa yako (ona Mafundisho na Maagano 58:26–28).

Himiza ukuaji wa watoto wako kwa kuunga mkono matamanio ya haki ya mioyo yao—swali moja la utambuzi kwa wakati mmoja.

Mawazo kwa ajili ya Kukuza Kujifunza na Ukuaji

  • Waelekeze watoto wako kwa Yesu Kristo na wafundishe jinsi ya kuzifikia nguvu za Upatanisho Wake.

  • Muige Yesu Kristo kwa kutoa upendo, mwongozo, msaada, na huruma watoto wako wanapojifunza kumfuata Yeye.

  • Kuza ukuaji wa watoto wako kwa kusaidia uelewa, uwezo, haki ya kujiamulia, na kujiamini kwao.

  • Njoo kwa Kristo kwa kujifunza injili Yake na kufanyia mazoezi ya kuiishi kwa pamoja mnapoendelea mbele kwenye njia ya agano.

Jenga Umoja na Nguvu kupitia Huduma

Picha
familia wakipeleka chakula kwa familia nyingine

Yesu Kristo aliwafundisha wanafunzi Wake “pendaneni; kama nilivyowapenda ninyi” (Yohana 13:34). Mnapofarijiana, kuinuana,na kuhudumiana, mnaeneza upendo safi wa Kristo na mnakuwa zaidi kama Yeye. Mungu pia anatoa fursa nyingi za thamani kwa watoto wako kujifunza na kukua kwa kujiunga katika kazi Yake na kutimiza ahadi zao za kuwahudumia wengine (ona Musa 1:39; Mosia 18:7–11). Kushiriki upendo wa Kristo na kunururisha nuru Yake kunawabadilisha wao na wale wanaowahudumia.

Familia yako pia inafaidika kutokana na kuwa wa kata au tawi ambako watoto wako wanatoa na kupokea upendo na msaada. Kufuma mioyo yenu “pamoja katika umoja na upendo” (Mosia 18:21) kunasokota mtandao wa uhusiano wa kusaidiana na uzoefu chanya ambao unaimarisha familia yako. Unapowahudumia wengine kwa upendo kama wa Kristo, unaweza kusaidia kujenga Sayuni katika familia yako na katika jamii kwa ujumla (ona Musa 7:18).

Wafundishe watoto wako kwamba huduma inaweza kuwa kitu cha kila siku badala ya kuwa mradi uliotengwa. Kujitahidi kutumikiana kutawasaidia watoto na vijana kupata maisha yaliyo ya kutosheka zaidi wanapoangalia nje ya mahitaji yao wenyewe badala kuangalia mahitaji ya wengine. Ni ya kushangaza jinsi ilivyo kujenga Sayuni kunavyowajenga watu wa Sayuni.

Mtazamie Kristo

Mwokozi alimwalika kila mmoja wetu kuwapenda na kuwahudumia wengine (ona Yohana 13:34–35). Kushiriki katika kazi ya wokovu ya Baba yetu wa Mbinguni kunatuimarisha na kutubadilisha sisi. Kuwa “katika kazi ya Baba [Yake]” (Luka 2:49) ilikuwa sehemu ya ukuaji Yesu aliyopitia katika ujana Wake alipokuwa “akizidi kuongezeka katika hekima na kimo, akimpendeza Mungu na wanadamu” (Luka 2:52).

Familia yako inajiingiza katika kazi ya Mungu ya wokovu na kuinuliwa kwa kuishi injili ya Yesu Kristo, kuwasaidia maskini, kuwaalika wote kupokea injili, na kuziunganisha familia kwa milele yote.4

Kuza ukuaji wa watoto wako kwa kuungana katika “kazi kuu” ya Mungu (Mafundisho na Maagano 64:33)—tendo moja la upendo kwa wakati mmoja.

Mawazo kwa ajili ya Kujenga Umoja na Nguvu kupitia Huduma

  • Onyesha upendo wako kwa Mungu na uje kumfahamu Yeye vyema zaidi kwa kuwapenda na kuwahudumia watoto Wake.

  • Pendaneni kwa kuwatumikia wale wanaowazunguka na kuwasaidia wenye shida.

  • Wakusanye Israeli kwa kushiriki injili, kufanya utafiti wa historia ya familia yako, kuhudumu hekaluni, na kuwasaidia wengine kufanya na kushika maagano matakatifu.

  • Jenga umoja na nguvu ya pamoja kwa kutoa upendo, kutengeneza hali ya kuwa wa, na kusaidiana.

Kutumia Mpangilio ndani ya Nyumba Yako

Kanuni hizi za mwongozo zinaweza kukusaidia wewe kufokasi katika kuwa mzazi kila siku. Kwa mfano, leo wewe unaweza kufikiria kuzingatia jinsi kwa kukusudia unavyoweza kutengeneza uhusiano wa upendo zaidi, kukuza kujifunza, au kuwajenga wengine. Kutumia mpangilio huu kunaweza kuboresha kujifunza injili, kustawisha ukuaji binafsi wa mtoto wako, na kuhimiza fokasi angavu zaidi ya nje ambayo itaiinua na kubariki familia yako. Kutumia kanuni hizi kunaweza pia kuboresha matumizi yako ya nyenzo za Kanisa lenye kitovu-chake nyumbani kama Njoo, Unifuate na programu ya Watoto na Vijana.

Kuna njia nyingi za kutumia kanuni za mpangilio huu. Kuwa mwenye kunyumbulika na tafuta ufunuo binafsi ili utumie kwenye familia yako Mpangilio wa “tengeneza, kuza, jenga” si lazima kuhusu kufanya zaidi. Wakati yawezekana kukawa na vitu unahisi kuongozwa kuongeza kwenye kile ambacho kwa sasa unafanya, mpangilio unamaanisha kukusaidia wewe kutumia muda wenu pamoja vizuri zaidi.

Unapofanya kitu cho chote ili kutengeneza uhusiano wa upendo, kukuza kujifunza na ukuaji, au kujenga umoja na nguvu kupitia huduma, unaweka msingi imara kwa kitu cho chote unachofanya katika nyumba yako.

Wazazi Wazuri Ni Wakutegemewa, Siyo Wakamilifu

Ni muhimu kukumbuka kwamba hauhitaji kuwa mkamilifu ili kuwa mzazi mzuri Badala yake, tafuta kuwa chanzo cha kutegemewa cha upendo na msaada kwa watoto wako. Kwa kujiunganisha tu na watoto wako katika njia ndogo kunaweza kufanya tofauti kubwa.

Kuwa mzazi kunapokuwa kwa kukatisha tamaa, kumbuka kupumua, jipe mapumziko kidogo, na endelea kujaribu. Unaweza kusonga mbele kwa imani ukijua kwamba Mwokozi anajali sana kukuhusu wewe na watoto wako na anakuza jitihada zako za dhati na matamanio yako ya haki.

Tumaini katika Kristo

Unapojitahidi kuwa thabiti katika kufanya yote uwezayo kupenda, kukuza, na kuimarisha kila mtoto, mmoja mmoja, wewe na familia yako mnaweza kuwa na matumaini katika Kristo kwa sababu ya ahadi Yake ya milele kwako: “Msiogope, watoto wadogo; kwani ninyi ni wangu, na mimi nimeushinda ulimwengu” (Mafundisho na Maagano 50:41).