2022
Je, Maandishi ya Isaya Yananifundisha Nini Mimi kuhusu Yesu Kristo?
Septemba 2022


“Je, Maandishi ya Isaya Yananifundisha Nini Mimi kuhusu Yesu Kristo?,” Liahona, Sept. 2022.

Njoo, Unifuate

Isaya 13–14; 24–30; 35

Je, Maandishi ya Isaya Yananifundisha Nini Mimi kuhusu Yesu Kristo?

Picha
Picha ya mchoro wa Yesu Kristo kutoka kwenye video za Biblia

Yaliandikwa takribani miaka 2,700 iliyopita, maneno ya Isaya nyakati zingine yanaweza kuonekana kutuzidi au yenye kutuchanganya. Lakini hakika, kusoma kutoka kwenye kitabu cha Isaya ni moja ya njia zilizo bora zaidi ambayo tunaweza kujifunza zaidi kuhusu Yesu Kristo. Nefi alimnukuu Isaya ili kwamba aweze “kwa ukamilifu zaidi kuwashawishi [Wanefi] ili waamini katika Bwana Mkombozi wao” (1 Nefi 19:23). Ili umwelewe vizuri zaidi Isaya, jaribu kufokasi kujifunza kwako juu ya mafundisho ya Isaya kuhusu Mwokozi

Fikiria maswali yafuatayo unapojifunza sura hizi:

  • Ni kwa jinsi gani Eliakimu anamwakilisha Yesu Kristo? (Ona Isaya 22:20–25.)

  • Yesu Kristo atafanya nini kwa ajili yetu sisi kwenye Ufufuko? (Ona Isaya 25:8.)

  • Je, ni kwa jinsi Kristo anawafundisha watu Wake? (Ona Isaya 28:10.)

  • Je, ni kwa jinsi gani Isaya anaelezea Urejesho wa injili ya Yesu Kristo katika siku za mwisho? (Ona Isaya 29:14.)

  • Je, itakuwaje wakati Kristo atakapokuja tena? (Ona Isaya 35:10.)

“Isaya alizungumzia mara kwa mara juu ya nguvu ya Bwana ya uponyaji, ushawishi wa utulizaji. … Roho wake anaponya; anatakasa; anafariji; anapulizia pumzi ya uhai mpya kwenye mioyo isiyo na matumaini. Ana nguvu ya kubadilisha vyote ambavyo ni vibaya na viovu na visivyofaa katika maisha kuwa kitu fulani chenye mamlaka na fahari ya utukufu. Yeye anayo nguvu ya kubadilisha majivu ya mwili wenye kufa na kuwa watu wazuri wa milele” (Tad R. Callister, Upatanisho Usio na Mwisho [2000], 206–7).