2022
Mpangilio wa Kuepuka Kujisikia Kukwama
Septemba 2022


“Mpangilio wa Kuepuka Kujisikia Kukwama,” Liahona, Sept. 2022.

Mpangilio wa Kuepuka Kujisikia Kukwama

“Yesu akazidi kuendelea kukua katika hekima na kimo, akimpendeza Mungu na wanadamu” (Luka 2:52), na vivyo hivyo sisi tunaweza.

Picha
mwanamume akiangalia machweo ya jua

Picha na Judith Ann Beck

Kujisikia Kukwama

Wakati akijitahidi kuishi injili kama kijana mkubwa mseja, inawezekana kuwa vigumu kutofokasi kwenye maeneo fulani ya maisha yetu ambayo tungependa ingekuwa tofauti. Nyakati zingine tunajisikia kama tumegonga uwanda tambarare katika maendeleo yetu. Kwangu mimi, hisia hizo za kukwama kwenye maeneo fulani inaonekana kupungua na kutiririka, na kuambatana na mimi siku nyingi, miezi, na pole pole hadi miaka. Daima nimekuwa na sababu nyingi za kuwa na furaha na kujisikia vizuri kuhusu maisha, lakini wakati fulani, hisia hizi za kukwama zilinigonga vibaya sana.

Katika wakati huo, mpwa wangu kijana aliomba kutumia muda pamoja nami. Alitambua uhitaji wa kuwa na malengo katika maisha yake na akaomba ushauri. Sikujisikia ulazima wa kuhisi kuwa nilikuwa katika nafasi yenye nguvu kutoa hekima kubwa, lakini nilisikiliza. Nilijua ningeweza “kumlilia” Mungu kwa ajili ya msaada (ona Alma 34:17–27) na kuomba kuweza kusema jambo ambalo lingekuwa na maana kwake. Katika kujibu, nilikumbuka Luka 2:52: “Yesu akazidi kuendelea katika hekima na kimo, akimpendeza Mungu na wanadamu.”

Nilipojitahidi kufokasi katika mahitaji ya mpwa wangu badala ya mahitaji yangu mwenyewe, kitu fulani kilianza kubadilika ndani yangu. Mpwa wangu na mimi tukaanza kuongea kuhusu jinsi Kristo alivyokua kiroho, kijamii, kimwili, na kiakili na vivyo hivyo sisi tunaweza. Ingawa mahitaji ya mpwa wangu yalikuwa tofauti na ya kwangu, maeneo haya manne ya ukuaji yalikuwa yanafungamana kwetu sote. Wakati tukiongelea kuhusu maandiko haya, nitambua kuwa lilikuwa likijibu maswali yangu mimi mwenyewe kuhusu tunawezaje kutokukwama.

Kubadilisha Fokasi Yangu, Kuifanyia Kazi Mipango

Nilipojitahidi kukua kama Mwokozi alivyokua, fokasi yangu ilibadilika, na badiliko hilo lilileta baraka za nyongeza. Kama Rais Russell M. Nelson alivyosema: “Furaha tuliyoisikia haichangiwi na hali ya maisha yetu na kitu chochote kinachuhusiana na fokasi ya maisha yetu.”1 Jitihada zangu za kukua zaidi kama Mwokozi zilisaidia kuondoa fikra zangu kutoka kwenye hali ambayo ilichukua fokasi yangu na kuelekeza upya kwenye maeneo ambayo ningeweza kuyafanyia kazi kwa ufanisi zaidi. Niliweza kuondoka kutoka kutafakari moyoni na kufanya matendo ya nje.

Kwa dhati nilitafakari jinsi ninavyoweza kukua katika kila eneo lililotajwa katika Luka 2:52, kutoka kuhudhuria kwa mfululizo hekaluni kwenda kukamilisha mbio ndefu za baiskeli.

Picha
Hekalu la Memphis Tennessee

Picha ya Hekalu la Memphis Tennessee na James Whitney Young

Katika kila eneo la malengo yangu, nilifanya uchunguzi:

  1. Nilipokuwa nikilifanyia kazi lengo moja, mara kwa mara nilihisi Kristo akiniimarisha kiroho, kijamii, kimwili, na kiakili vyote ndani ya lengo lile.

  2. Mara chache, kama iliwahi kutokea, lengo lo lote kutokea likiwa limejitenga na maeneo mengine ya ukuaji—yalionekana kuathiri na kujenga juu ya jingine Maboresho katika eneo moja yaliongoza kwenye maeneo mengine yote. Kupuuzia eneo moja kuliathiri maeneo mengine yote. Nilitambua kwamba kila eneo lilistahili usikivu.

  3. Karibia kila lengo lilijumuisha watu wengine—ama kujifunza kutoka kwao au kushiriki mawazo na uzoefu pamoja nao—na kuimarisha uhusiano wetu.

Kutafuta na Kushiriki Shangwe katika Kristo

Daima ninayo fursa ya kuona na kuvutiwa na ukuaji wa wengine, na natumaini ninaweza kufanya vivyo hivyo kwao. Hivi karibuni niliongea na rafiki yangu mseja ambaye anajisikia kuwa amekwama na kuchanganyikiwa na hali fulani za maisha. Nilimsikiliza ili kuelewa, na kisha nikawa na uwezo wa kushirikiana matukio ambayo yamenisaidia mimi na pia kumwonyesha kila eneo la ukuaji kurudi kwa Mwokozi.

Wakati sio maeneo yote ya maisha ambayo yaliniacha mimi nikijisikia nimekwama miaka mingi iliyopita yamebadilika, nimebadilika nilipojifunza kufokasi zaidi juu ya Mwokozi na kujitahidi kukua kama Yeye. Kama Rais Nelson alivyoshiriki, “Kuna mambo mengi sisi tunaweza kudhibiti. Tunaweka vipaumbele vyetu na kuamua jinsi tunavyotumia nguvu, muda na nyenzo. … Tunawachagua wale ambao kwao tutawageukia kwa ajili ya ukweli na mwongozo.”2 Vyo vyote hali zetu zilivyo, maeneo ya ukuaji katika Luka 2:52 yanaweza kutusaidia kubadili fokasi zetu na kupata shangwe ya ziada na kuendelea kupitia kwa Baba wa Mbinguni na Mwokozi.

Mwandishi anaishi huko Tennessee, Marekani.